Nikiangalia vizuri nahisi kama mama anaiangalia 2025 so anatengeneza mazingira kwanza ya kurudi, lazima apambane kuwafurahisha wapiga kura, na atawafurahishaje?
1. Atahakikisha pesa zinarudi mifukoni kwa kuwapa kipaumbele wafanyabishara na investors ili kivyovyote pesa irudi katika mzunguko na zijae mtaani wananchi wawe na imani naye.
2. Ataruhusu uhuru wa habari ili kutengeneza trust kwa mabeberu waweze kumsaidia mikopo ili kumalizia miradi iliyobaki cz hawezi kuruhusu pesa iingie mtaani na at the same time akafanya miradi mikubwa ni ngumu sana.
3. Kwenye kutengeneza trust kwa mabeberu ataruhusu baadhi ya mambo ambayo mtangulizi wake aliyapinga hususan katika suala zima la covid, na hata baadhi ya mikataba iliyokuwa ikiwabana waende 50% na nchi especially kwenye madini.
Hayo ni machache tu ambayo naona yanaenda kutekelezwa ili kuhakikisha anarudi 2025.
My Take: Siasa inarudisha nyuma sana maendeleo ya Afrika kwa kigezo cha democracy but hakuna namna cz tulishachelewa waafrika na kufika walipo wenzetu ni ndoto.