Uko myopic kwenye mambo ya uchumi. Hili Ndio jambo ninalolizungumzia. Ni furaha kuonekana kuwa kodi zinakusanywa nyingi kupita miezi mingine lakini unafahamu biashara ngapi zinakufa kutokana na ukusanyaji huo wa kodi? Na biashara zikifa unadhani ukusanyaji wa kodi utaendelea kuwa mzuri au mbaya?
Halafu kuhusu bomba la mafuta, unafahamu ni sababu gani bomba lilihamishiwa kutoka Kenya kuja Tanzania? Kwasababu route ya Tanzania ina gharama ndogo za ujenzi kuliko route ya Kenya na Tanga port tayari inafanya kazi tofauti na Lamu port ambayo bado inajegwa. Halafu pia bandari ya Lamu ipo karibu na Somalia, kulikuwa kuna hofu ya uvamizi wa Al-Shabab!