Ninachofarijika ni kwamba ama kwa hakika watanzania tumemuombolezea Magufuli wetu inavyopasa
Dunia nzima imetambua Magufuli alikua nani kwa watanzania, haijawahi kutokea Africa nzima mtu kuombolezewa kama Magufuli, watanzania hakika tumempa heshima yake stahiki
Kingine nimefarijika zaidi ni namna katika uhai wake tulimuonesha wazi wazi kwamba tunampenda sana na kutambua wazi thamani yake kwetu, hatujamsifia mema yake akiwa tayari mfu bali angali anaishi hivyo aliondoka akijua moyoni watanzania wananipenda
Kaondoka Jina lake likiwa tayari linaenziwa kama Magufuli Bridge kule Morogoro, JPM Bridge Busisi, Magufuli City Dodoma, Magufuli Terminal Dar, Magufuli Annex Chamwino etc
Binafsi Mungu anijalie wa kiume na mimi niweze kumuenzi kwa aina yangu
Magufuli utabaki moyoni mwangu daima sababu toka nimepata akili sijawahi kumlilia binadamu mwenzangu namna nimekulilia, nimempoteza mama yangu mdogo niliekua nikimuuguza juzi kati lakini sijadondosha hata tone la chozi ila Magufuli nimekulilia toka nimepokea taarifa mpaka dakika hii.
Hujafa wala hutokaa ufe, unaishi kwenye fikra zetu Daima.