Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Hawaa ndo majiran tulio nao mpaka sasa hiv oneni walivyo waajabu
IMG_20210320_074428.jpg
 
Ashakumu sio matusi, naomba kulonga na WATANZANIA wenzangu.

Vifo vingi vikiambatana kwa pamoja huwa kunaleta maswali na taharuki kwa wananchi na kila mtu anaweza kusema lake. Na mimi naomba niliseme langu japo linaweza kuwa gumu kidogo lakini naomba tuvumiliane.

Kila Jambo linakuwa na theory, kila theory inakuwa na conspiracy yake. Naomba nitumie moja ya hizi conspiracies.

Conspiracy theory.

Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, yaani kuanzia leo hadi tarehe kama ya leo mwaka jana, ilianza tukio la Mzee wetu Philip Mangula kuwekewa sumu, hii issue ili_trend sana na ikakaliwa kimya as if hakuna kilichotokea.

Ilikuwa Februari 29, 2020 Rais wa Tanzania, John Magufuli alimjulia hali Mangula aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka ghafla Ijumaa Februari 28, 2020.

Taarifa ya Mangula kuugua ilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa huku video zikimuonyesha Magufuli akizungumza naye, baadaye kusali pamoja.

Mangula alionekana akiwa amelala kitandani huku akiwa na plasta juu ya jicho lake la kushoto.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mangula ambaye alishiriki kikao cha kamati kuu ya chama hicho sambamba na Magufuli kilichofanyika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba Februari 28, 2020, baada ya kuanguka alilazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU).

“Mangula aliugua ghafla jana na kisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu,” inaeleza taarifa hiyo.

“Utapona na Mungu atakusimamia katika tatizo hili, sisi tulipoona jana (Ijumaa Februari 28, 2020) umeanguka ilitushtua,” alisema Magufuli na Mangula kujibu, “sijui nimeangukaje.”

“Huwezi ukajua ila sisi tunamkabidhi Mungu na Mungu atakusimamia, Mungu akujalie sana,” alisesema Rais Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa CCM.

Hayati Dr John Magufuli aliliingilia kati hadi mzee Mangula akapona, baadae Jeshi la Polisi kupitia Mambosasa (RPC wa Dar es salaam lilithibitisha kwamba Mangula alipewa sumu na kuanzisha msako wa kumtafuta aliyempa sumu hiyo Mzee Mangula.

April 30, 2020 tukampoteza aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, Balozi Dr Augustine Mahiga. Lilikuwa pigo na muendelezo wa mbaya ukaanzia hapo, ndani ya muda mfupi akafariki Mzee wetu mpendwa, Benjamin Mkapa.

Ilikuwa Tarehe 23 July 2020, lilikuwa pigo si tu kwa taifa bali kwa watu wanaomzunguka Dr Magufuli. Utasemaje haya mambo yanatokea tuu? Hapana, lazima ujiulize kwanini kipindi hiki? Mzee Mkapa taarifa ya kifo chake ilieleza kwamba alikuwa amekaa na alipojaribu kusimama akaanguka na baada ya kumpeleka hospitalini ikajulikana kuwa amefariki kwa mstuko wa Moyo.

Tarehe 17 Februari 2021 tukampoteza Maalimu Seif Sharif Hamad, huyu alikuwa ametoka Chato akiambatana na Dr Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar, Maalimu Seif alionesha njia ya kuutaka umoja wa Wazanzibar, aliukataa ubinafsi na kuamua sasa iwe ni kwa ajili ya Zanzibar na watu wake, wasiolitakia mema taifa hili wakamuita msaliti.

Tukapewa taarifa za kifo chake hata kabla hajafariki, hujiulizi kulikuwa na nani nyuma ya kifo chake? Ilikuwaje kukawa na taarifa za akina Kigogo katika uhai wa Makamu wa Rais wa Zanzibar? Taarifa hizo zilitoka wapi?

Tunaambiwa tena mitandaoni kuwa Mheshimiwa Philip Mpango anaumwa na ikafikia hatua ikazushwa taharuki kuwa amefariki hadi ikamlazimu kujitokeza hadharani kuondoa uvumishi huo. Bado hamjiulizi?

Sakata la mitandaoni halikuishia hapo, tarehe hiyohiyo 17 February 2021 ikaja habari ya Katibu Mkuu kiongozi, taarifa za kifo chake zikatangazwa, Hayati Balozi Kijazi, ni watu wanaomzunguka Rais wetu, tukaambiwa tujiandae kwa Jambo kubwa zaidi, taarifa zote hizo anazitoa Kigogo kule Twitter, Kigogo ni nani? Kigogo yuko wapi? Ameshindikana kupatikana?

Tundu Lissu akaandika katika ukurasa wake kwamba mwisho wa utawala wa Dr Magufuli hauko mbali, baada ya muda mfupi akaanza kuhoji yuko wapi Magufuli? Kigogo, Zitto Kabwe, wote hao wanahoji alipo Magufuli, nikajiuliza, ni tangu lini utaratibu wa kuulizana haya maswali? Kuna nini ndani yake? Ni Nani kati yao alienda ikulu akamkosa ofisini kwake?

Ukiunganisha "dots" katika haya matukio ya viongozi wetu kuondoka ghafla inatia shaka, inatia shaka zaidi kwa sababu kipindi hiki migogoro na jirani zetu zinaibuka kila mara kama kupoteza maboya vile. Tukio fulani likitokea, Kenya anazua Jambo lake aidha kuzuia bidhaa zetu kuingia nchini kwake ama wananchi wetu kuingia nchini kwao.

Hayati, Dr John Magufuli alisema kwamba Vita vya kiuchumi ni Vita vigumu kuliko Vita vya moto, kwa sababau kwenye hivi Vita humuoni adui yako kwa macho, unakuwa kama unapigana na kiza.

Kuna watu wako kimya mno hawasemi chochote tangu walipoguswa maslahi yao na wengine kufukuzwa katika nafasi za uongozi walizokuwa nazo mwanzoni, Mzee Mangula alianguka masaa kadhaa baada ya kutoka kwenye kikao cha kuwahoji viongozi kadhaa wa CCM ambao Kuna wengine walifukuzwa uanachama wao kabisa. Sijui kama tunaelewana lakini. Sisemi kwamba theory yangu ni proof ila inaweza kuwa theory of conspiracy yenye maana kidogo.

Ningeulizwa kipi kifanywe hivi Sasa, kwa maoni yangu ningesema naomba miili ya Marehemu hawa ifanyiwe "postmortem" kujiridhisha vifo vyao. Sijui ni kipi kimenipa ujasiri wa kuyaandika haya ila ni Mwenyezi Mungu pekee ndo anaejua, maana watu wote waliokuwa na ukaribu zaidi na wenye nafasi nyeti katika taifa hili wameondoka na wengine ni dhaifu kiafya. Hii tuiiteje?

Naandika haya nikiwa siijui kesho yangu bada ya andiko hili lakini WATANZANIA tujue kuwa tuko vitani na tunaepigana nae hatumjui, aidha yuko hapahapa tunae au yuko nje ya mipaka ya nchi yetu.

Mungu atupe nguvu na ustahimilivu.
Rest Easy Champion, utaishi mioyoni mwa WATANZANIA kwa vizazi na vizazi.

Abdoulquarim Malisa

 
Bandiko limekaa kipropaganda sana. Hizi propaganda na utoto inabidi tuachane nao sasa. Nani amuue Magufuli wakati tayari alikuwa na matatizo yake kitambo tu. Kuimba vita vya kiuchumi kwenye majukwaa ya kiasa kila mara ni propaganda za marehemu sababu vita vya kiuchumi vinapigwa kwenye sera ya uchumi wa nchi na espionage. Kila nchi ina vita vya kiuchumi inapigana ndomaana huoni viongozi wengine wakiimba hiyo vita sababu sio kitu cha kushangaza.
Hapana mzee,kuna jambo linaendelea katika hii nchi,sio bure huu ni mkakati uliosukwa kwa lengo maalum...tutaona huko mbele,kwanza tutaanza kuangalia baraza la mawaziri atakaloliunda mh
 
Magufuli failed miserably on foreign policies 2/10. Alipaswa kutenganisha nchi na yeye binafsi. Mara nyingi alifanya maamuzi kutokana na hisia zake~ mfano ni sera zake kwa nchi ya kenya. Uhuru nilimpendea kitu kimoja tu! Anajua kudeal na viongozi vichwa mbovu wanaoangalia short term gains pekee. Natumai huyo mama ataipa EAC intergration kipaombele.
Tanzania interest before East afrika interest that's what we do.
 
Hapana mzee,kuna jambo linaendelea katika hii nchi,sio bure huu ni mkakati uliosukwa kwa lengo maalum...tutaona huko mbele,kwanza tutaanza kuangalia baraza la mawaziri atakaloliunda mh
Lengo gani wakati waliofariki wote ni watu wazima na walishakuwa na matatizo yao ya kiafya. Mwandishi anasema kuna kundi lenye nia ovu dhidi ya magufuli lakini wote hao walio kwenye hilo kundi hakuna hata mmoja aliekuwa na taarifa za kueleweka alipo magufuli ndomaana naona bandiko lake limejaa uzushi tu.

Huyo mwandishi anavyomzungumzia kigogo2014 kama vile huyo kigogo alitoa taarifa sahihi, kifupi anampa cheo ambacho hana. Kigogo ametuambia sabaya kafariki wakati uongo, mpango kafariki ukawa uongo, mpango kapelekwa nairobi ukawa uongo kubwa kuliko yote ni alipo magufuli, alianza kusema kapelekwa nairobi, akaja kazidiwa kapelekwa india, akaja kikwete na mwinyi wamemuona magufuli akiwa katika pumzi zake za mwisho, akaja magufuli akiwa taabani kenya akarudishwa Tanzania na jana ameweka gazeti la kenya kuthibisha madai yake , binafsi naona habari nzima ya kwenda kenya ni ya kupikwa sababu matukio hayana muungano, mgogoro wa mahindi magufuli akiwa mgonjwa, mahusiano ya Hayati na kenya kipindi akiwa na afya. Ukijumlisha yote hayo ni wazi kigogo amewalisha watu matango pori.
 
Nipo online nalia na watanzania wenzangu, nalia na wanawake na wanaume wanaomlilia Magufuli huko barabarani 😭😭😭😭😭😭😭
 
SITARAJII WAKENYA WAMPENDE RAIS MAGUFULI.

Na Thadei Ole Mushi.

Katika list ya Marais ambao waliwahi kuiongoza Tanzania, Rais Magufuli anaongoza kwa kuwa Rais anayeleta athari Hasi kwenye Uchumi wa Kenya. Ndio maana hizi chokochoko za kuchunguza JPM yupo wapi ana Hali gani vyombo vya habari vya Kenya navyo vinaimba na kufuatilia sana.

Twende sawa.....

1. UKUTA WA MERERANI

Kabla ya kujenga ukuta wa Mererani Kenya na India zilikuwa ndizo nchi zilizoongoza kwa kuuza madini ya Tanzanite. Mwaka 2013 kwa mfano India pekee iliuza madini ya Tanzanite yenye Thamani ya USD 300 Milioni Hadi Marekani ikawa inahoji Kama madini hayo yanachimbwa India au Tanzania.

Mwaka huo huo Kenya ilisafirisha na Kuuza nje Tanzanite yenye Thamani ya USD 100 Milioni. Wakati hayo yakifanyika Tanzania haikuweza hata kufikia mauzo ya USD 50 Milioni kwa mwaka 2013.

Toka ukuta huo ujengwa Kenya haijauza madini hata ya Buku ya Tanzanite nje ya nchi. Kenya inafahamu kuwa Kama Magufuli hatakuwepo Tanzania Basi huenda fursa hii ikafunguka Tena. Tumuombee Rais wetu... Fuata link ifuatayo kusoma athari za ukuta wa Mererani.


2. UJENZI WA RELI YA SGR.

Kuna watakaojiuliza Reli ya SGR inawahusu nini wakenya au ina athari gani kwa wakenya? Ni swali zuri Sana na kila anayejiuliza ni haki yake ajiulize.

Kama Kuna kitu kinawasumbua Kenya ni Mradi huu wa SGR. Tukumbuke kuwa issue hapa sio mataruma ya Reli Bali issue kubwa hapa ni bandari zetu Mombasa na Daresalam hili niliwahi kuwaambia na narudia Tena na Tena huenda hatuelewi Nini maana ya hii Vita tunayoizungumza.

Ipo hivi

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

"Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika....

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki Tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC - The East African - Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC

Hili Ni Gazeti la Kenya sio la Tanzania katika Hali Kama hii hawawezi kutufurahia sisi kupaa kiuchumi.

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.


3. MRADI WA STIGLERS GORGE.

Huu ni Mradi wa umeme ambao kufikia 2022 tunatarajia uwe umekamilia kabisa.

Mradi huu utatupatia megawatt 2,100 sawa na bwawa la Aswan la Misri ambalo nalo linatoa megawatt hizo 2,100.

Stiglers itakuwa bwawa Namba Moja Afrika yeye na Aswan kwa pamoja kwa kutoa megawatt nyingi na zinazolingana. Mabwawa Mengine yote yaliyobakia Afrika hayawezi kufikia kiwango hicho Cha Stiglers.

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga.

Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira....

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais wetu. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.


Linapokuja suala la kiuchumi kwa Dunia ya Sasa ni Vita. Na Kama hutoruhusu akili yako kufanya kazi Basi utajikuta ukiitikia chorus za nyimbo za mabeberu.

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?.....

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Sisi kujenga Stiglers tu imekuwa kelele kubwa. Nafikiri unaelewa Sasa na Kuna haja kubwa Sana ya kumuombea Rais wetu.

4. UJENZI WA VIWANDA NCHINI.

Sera ya Rais Magufuli toka ameingia madarakani Ni ujenzi wa Viwanda. Tafsiri ndogo tu Ni kwamba tunakwenda kuingia kwenye ushindani mkubwa Sana na Kenya kwenye kuuziana bidhaa. Maana yake Ni kuwa Kuna baadhi ya viwanda vya Kenya vitakufa kutokana na ujenzi wa viwanda nchini. Tukumbuke Soko kubwa la Kenya kwa bidhaa zake za viwandani Ni Kenya. Ingia supermarket kagua bidhaa nyingi zinatoka Kenya.

Kwa miaka ya karibuni Tanzania imeanza kuharibu dili hili la Kenya. Hata Panadol Sasa hatununui toka Kenya. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa Kenya ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda. Hii ni Vita.

Haya Ni mchache Kuna Mengine si ya kuyasema hapa. Na ndio maana huwa nasemaga Marais Kama JPM huwa hawapatikani Mara kwa Mara.

Ole Mushi
0712702602

Mkulu kwa heshima na taadhima, naomba hii uianzishie uzi.
Natanguliza shukrani.
🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Back
Top Bottom