Magufuli ameonesha njia jinsi gani viongozi wa Afrika wanapaswa wawe naamini huko alipo Mwenyezi Mungu amemuweka panapo stahili japo ana makosa km binadamu lkn naamini alikuwa na mapenzi makubwa dhidi ya wananchi, wiki yote hii nmekuwa naumia moyo wangu ulikuwa unauma sana nilishahisi kuna kitu kibaya kinatuzunguka Watz.
Asante Magufuli, asante Mungu kwa haya yote kwani wewe hukosei na hujawahi kukosea, nimelia lkn hii haiondoi ukweli kwamba Magufuli hatupo naye tena, asante baba kwa zawadi hii uliyotupa na asante pia kwa kila ulilolifanya kwa nchi yetu.
Watanzania naomba tuungane na tujikaze katika kipindi hiki kigumu tusitetereke mana katika kila gumu kuna njia, hakika tusijibishane na mtu yeyote zaidi tu tuseme asante.
Asante Magufuli, Mungu akuweke baba, wewe ni zaidi ya mwamba, miaka yako sita uliyoongoza imetosha kujipambanua kwamba uliletwa duniani kupigania haki, asante sana baba.
Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi Amina.