Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,016
- 16,433
Kwa mfano ukitumia expenditure method kucalculate uchumi wa Tanzania na mimi nitumie income method, tunastahili kupata the same amount. Lakini in reality ni ngumu kufanyika. Kwa sababu nikicalculate income ambayo watu wamepokea katika uchumi fulani ni ngumu itoshane na expenditure ambayo watu wamespend katika uchumi huo. Hii ni kwa sababu ninaweza kosa kuinclude income fulani au expenditure fulani.Unaposema zinakaribiana how!!?
Mimi huwa naprefer kutumia production method ambayo tunaangalia value of goods and services produced in an economy. Lakini hapa pia tunaweza kosa kucalculate some goods. Kwa mfano nipo sure kabisa wakati Tanzania inacalculate value of goods produced, huwa hamuhesabu informal sector, yaani sufuria inayotengenezwa na watu wa juakali au wamachinga. Hata wheelbarrow zinazotengenezwa na watu wa juakali huwa hamuhesabu. Hata Kenya tupo hivyo, huwa hatuhesabu vijiko na sufuria zinazotengenezwa na watu wa juakali. Hii ni kwa sababu industries zetu ni ndogo yaani informal. Na hizi small industries huwa nchi za Africa tunazipuuza. Marekani au Ulaya, vijiko vinatengenezwa na viwanda vikubwa na pia serikali inahesabu ni vijiko vingapi vimeundwa mwaka fulani na bei yao ni pesa ngapi, sufuria ngapi ziliundwa, gari ngapi ziliundwa, meli ngapi ziliundwa na value yao ni pesa ngapi?
Hizi methods tatu zinastahili kukupa the same amount lakini kwa sababu binadamu huwa tunasahau kuhesabu kila kitu au tunapuuza kuhesabu vitu basi hazitakupa the same amount.
