Hizo ni executive orders anazotia saini ambazo ni tofauti na file. Unajua siku hizi mambo mengi tunayafanya kwenye tarakilishi. Badala ya mafaili tunadeal na softwares. File bado zinatumika lakini sio sana kama zamani. Hata wewe ofisini najua unatumia tarakilishi sasa itakuwaje huyu mzee wenu haitumii?
Huku Kenya many govt services zimepelekwa online. Kwa mfano ukitaka ku-apply for passport una-apply online, malipo unafanya through Mpesa au credit cards e.t.c. Hata taxes siku hizi unalipia tu through Mpesa hata saa nne usiku sio kama zamani ambapo tulikuwa tunakwenda kulipa taxes kwenye benki na kupanga foleni kwa muda mrefu. Yaani teknolojia inarahisisha mambo. Mambo ya kupanga foleni kwenye benki imekuwa nadra. Kuna online banking pia. Lakini TZ najua hamuwezi kukosa kupanga foleni maana services za kiserikali hazipo online na pia pengine services za online banking za benki zenu sio nzuri.