We jamaa unafikiri uraia ni pipi unatoa tu kirahisi hivyo. Hao jamaa wengi wao wanaokuja huku wana hela ya kawaida tu sio potential investors ambao wanaweza kujenga viwanda na kuajiri watu. Wengi ni youtubers tu ambao wanakimbia maisha magumu ya marekani na ubaguzi lakini sio kusema wana kitu kikubwa wanaweza kuongeza kwenye uchumi.
Uraia ili upewe lazima ukidhi vigezo ikiwa pamoja na kujua na kuingiliana na wananchi sasa hawa wamekuja juzi leo unasema tuwape uraia haraka haraka, alafu pia kumbuka Tanzania hakuna uraia wa nchi mbili.
Sheria ya uwekezaji ni nzuri sana kama wanakuja kuwekeza waungane wawe na dola laki tano wapewe eneo la uwekezaji na visa zinaongezwa tu muda kirahisi. Hii sheria pamoja na ya uraia zilitungwa kulinda ardhi kubaki kwa wazawa. Kenya, ghana na nigeria hawana ardhi kubwa ambayo mgeni anaweza kuhodhi hivyo wao na sisi ni tofauti sana.
Mbona husemi wakenya wapewe uraia kirahisi hivyo na ndio wamewekeza mtaji mkubwa au kwakuwa ni wamarekani?