Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

ichoboy01 lazima ulikua msumbufu na mjanja kuanzia shule ya chekechea., uko na ka utundu flani ya kijanja janja., Mwehu, mkora., stubborn asie kubali kushindwa, unapigana hadi kufa
 
Wadau Gold last year imeingiza $2.7B imezidi hadi revenue ya watalii kwa mara ya kwanza ambao ulikua $1.9B...

Ni suala la miaka miwili tu pale gold itapozidi $3B na utalii $3B Ndio mtanielewa kwann nilisema Ghana tunawakalisha soonView attachment 1689472
Screenshot_2021-01-29-22-23-19.jpg
 
Have been following this thread for the past 5yrs and I can say it used to be very informative on infrastructure development matters on both countries. All i can say is kudosto the EAC region. Despite that nowadays this thread is becoming so boring with dick measuring contexts topics whereby both Patriots wa KE & Tz end up with misleading information to the masses. I believe when Annael started this thread it was to showcase the uniqueness & positivities of our beautiful cities not the ugly toxic topics zenye huwa zimejaa huku sikuizi. Kuna Baadhi ya watu huku mnaturudisha nyuma sana kwa kurushiana maneno mingi za upuzi. Uzi huu Penye umetoka ni mbali na unaelekea mbali zaidi. So please let's brothers have some decorum on how we exchange ideas.Kumbuka Kuna 1milion plus spectators always behind the keyboard ambao ufuatilia uzi despite them commenting. Mwisho ningempongeza sana Annael you must be proud where you are. Those are my two sentiments
Wacha uongo huu uzi hauna hiyo miaka unayosema, km unafuatilia endelea kufuatilia ukiona panapokupendeza sawa twende pamoja ila panapo ku bore pia pita kmy kmy.

Nyie mmetutukana sn so nowadays kibao kimebadilika mnaanza porojo hapa, btw nimependa narration yako ya kistaarabu ila wacha uwongo.
 
Hiyo kujenga dual carriage kwa mbeya from Uyole to Mbaliz ndio nimekisikia wewe
Umemsikiliza mara Ngapi Magu akiwa ziarani mkoa wa Mbeya au wakati wa kampeni? Ukizipata hizo hotuba zake zina maelezo mazuri. Pia ukisoma bajeti za wizara ya ujenzi kuanzia 2016 nadhani kila mwaka wamelielezea hilo. Ndiyo sababu pia yakufanya bomoa bomoa kuanzia Sai mpaka Ilomba.

Kwa maelezo ya Magu (2019 akiwa Uyole kwa mfano) waliamua kuiunganisha na mradi wa Igawa-Tunduma ili kurahisisha utekelezaji.
 
Hii habari si encouraging one, inaonyesha negotiations zita-drag ukizingatia breaking even price ikiwa juu ya Equinor portfolio na ndo maana wame-write down expenses for pre TLNG costs in other words wame-absorb the over the board costs!
The good thing ni kuwa bro Magu kawabana vizuri sana kwenye kona. Kaamua ku-drill visima viwili kwenye vitalu vyetu viwili tunavyomiliki. Ikiwa mradi wa LNG plant una mauzauza mengi ni afadhali tukajiongeza wenyewe mdogo mdogo tukaanza kuwauzia majirani wanaotuzunguka kwa kutumia pipelines kuliko kokomaa na kitu ambayo tunapigwa.
 
hii habari ya kenya kuwa in recession maana yake nn, generally to GDP.. watu wa uchumi
View attachment 1689396
Tafsiri yake siyo nzuri hasa zikizingawa hatua ambazo nchi inazichukua kushughulikia corona.

Simply said ni kwamba uzalishaji/mauzo vinashuka. Sasa kwa kawaida inapotokea recession hatua sahihi za kuchukua ni kuhimiza uzalishaji na si kuukwaza kwa kutumia maujinga ujinga kama "cafew" au sijui partial lockdown.

Kwa jinsi Kenya inavyoenenda na pia kuzingatia mambo yanayoendelea kwenye ulimwengu mwingine lakini unaohusiana na Kenya huenda recession hii ikawaingiza kwenye mgogoro wa kiuchumi.

Mambo hayo ni kama vile kuanguka kwa soko la maua Ulaya ambapo Kenya inakosa mauzo. Kutokana na corona sasa hivi maua hayauziki Ulaya na tuliona mwanzoni mwa janga hili mwaka jana shehena za maua yakitupwa.

Pia mwenendo wa Tanzania kuuza bidhaa zake za mbogamboga, matunda na minofu ya samaki, ng'ombe na mbuzi moja kwa moja kwenye masoko ya ng'ambo bila kupitishwa Kenya (ambako mengi yalikuwa yakifanyiwa packaging/repackaging) kunaendelea kuinyima mapato Kenya.

Lakini tusisahau vilevile kuwa sasa hivi Tanzania ambayo ilikuwa soko kubwa la bidhaa za Kenya iko kwenye njozi za ongezeko la viwanda. Viwanda ambavyo vingi huzalisha bidhaa ambazo awali zilikuwa zikiingizwa kutoka Kenya.

Hapo hatujaihusianisha hiyo recession na ukopaji holela unaofanywa na serikali ya Kenya kwa mgongo wa corona. Madhara yake hayaonekani mara moja ila katika kipindi kirefu yanaweza kuonekana kwa kuirefusha recession na hivyo kupelekea mgogoro wa kiuchumi.
 
Back
Top Bottom