Sijakataa kuwa nyie mnapanua port yenu. Lakini nina swali. Kenya ikisign deal na Maersk kuwa Maersk itakuwa inabeba mizigo yake kutoka Uchina kwa meli kubwa ya post-panamax na kutia nanga Lamu port. Kisha maersk haitalipishwa chochote kufanya transhipment hapo Lamu port. Meli kubwa ikitia nanga Lamu inapakua mizigo inayokwenda Djibouti port, Mombasa port na Dar port kisha meli inaendelea na safari yake kushusha mizigo barani Europa. Kumbuka geography ya dunia inafavour Lamu maana Lamu ipo karibu na hizo port tatu. Ni kweli kuwa Maersk ikishapakua mizigo Lamu pia inaweza kuja hadi Dar kupakua mizigo ya Dar kwa kutumia post-panamax ila that will be costly. Meli kubwa kama hio inatumia mafuta mengi per kilometre kushinda meli ndogo, halafu pia itapoteza muda mwingi sana kutia nanga katika ports mbili badala ya kutia nanga katika port moja. Sasa kama wewe ungekuwa business manager wa Maersk, ungeamua kuleta post-panamax ipakue Kenya kisha ipakue Tanzania au ungeileta ipakue Kenya tu kisha iendelee na safari yake barani Europa? Ni swali tu.
Halafu swali lingine, Maersk ikiamua kufanya transhipment Lamu port (maana imeshatia saini na KPA), halafu itumie meli ndogo kuleta mizigo Dar port, Rais wenu Magufuli ataiban Maersk company? Atailazimisha kuleta meli kubwa ya post-panamax hadi Dar? Hii yote eti kwa sababu hataki trans-shipment ifanyike Kenya? Halafu akiban Maersk ndio itakuwaje? Au akiilazimisha Maersk walete post-panamax Dar, Maersk itakubali hata kama it is less economical kuleta meli kubwa hadi Dar? Haya ni maswali tu sio lazima uyajibu. Magufuli ni mtu anayefanya vitu kwa fujo kwa hivyo sitashangaa akithreaten Maersk ifanye anavyotaka yeye la sivyo isikanyage Tanzania. Maersk nayo hatujui itareact vipi kwa vitisho hivyo.