Hiyo ndio shida na ugumu wa uongozi katika inchi hizi za dunia ya tatu. Kumbuka kwamba, kazi mojawapo ya Serikali ni kuhakikisha pesa inazunguka katika uchumi kwa njia mbalimbali, moja wapo ni kuiwezesha sector binafsi kwa kuzipa tenda za kazi.
Serikali isingeshindwa kuukabidhi mradi wa BRT kusimamiwa na SUMA JKT, au kuamua kusiwepo na Private security Companies badala yake wakatengeneza kitengo ndani ya jeshi kwa ajili ya kufanya kazi ya kulinda, kwa kufanya hivyo tusingesikia wizi wa pesa zinazohamishwa kutoka Benk, na jeshi lingepata pesa nyingi sana.
Hivi kwanini hizi kazi za ujenzi wa reli ya SGR na ukarabati wa reli za Zamani, Serikali haikuamua kutumia wanajeshi na JKT ambao wapo katika kambi na hawahitaji kulipwa kwasababu tayari wanaomshahara wao, huoni kwamba tungepunguza sana gharama za ujenzi na ukarabati?.
Lazima Serikali itoe kazi kwa sekta binafsi ili kuchochea uchumi, kinachohitajika ni kuyasimamia hayo makampuni binafsi ili yafanye kazi yenye ubora unaokubalika, mbona hiyo barabara ya Kibaha inafanywa na kampuni la kitanzania lakini ipo vizuri sana, mbona Stendi mpya ya Dodoma imejengwa na watanzania, mbona Songoro marine ni watanzania?