joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
China ni "Communist state" na haitokaa ibadilike, kufungua masoko na kufanya biashara huo sio ubepari, bado china na Tanzania zinafuta misingi ya kijamaa inayosisitiza kwamba dola(Serikali) ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kila raia ana haki ya kupata huduma bora za msingi za kibinadamu bila kujali kipato chake.China ilikuwa ni nchi ya kijamaa but nowadays it's no longer a communist state, ujamaa ulisaidia kwa wakati wake lkn kwa sasa haiwezekani ku exist, ni ngumu sana, kwa kipindi kile ulifaa hasa ktk kujenga misingi ya utu, lkn kwa sasa haiwezekani mkuu tukubali tukatae, hata hapa Tanzania umeshaanza kututoka japo ile misingi bado tunayo but ule ujamaa umeondoka miongoni mwetu, ukitaka kuamini angalia hata kwa ngazi ya familia, unakuta chao chao chetu chetu iko hvyo, alafu mkuu ubepari kwa Afrika unafeli kwasababu ya ulafi wa viongozi wetu, lkn ukimpata kiongozi dizain ya Magu hamuwezi shindwa, btw even our president amejipambanua kwmb yy ni bepari.
Serikali katika misingi ya Communist/Ujamaa, lazima iwe na mamlaka kamili katika umiliki na matumizi ya ardhi, kuhakikisha kila mwenyekuhitaji ardhi kwa ajili ya kujipatia mahitaji ya kibinadamu kama chakula na malazi anaipata bila kunyonywa na matajiri, na kuhakikisha kwamba ardhi ya nchi inatumika kwa manufaa ya watu wengi.
Communist/Ujamaa unazingatia kwamba wale matajiri wanakatwa kodi kubwa ili kuwasaidia masikini, kwamba Afya ya msingi(Primary health care), elimu ya msingi ni haki ya kila raia na lazima vipatikane bure bila malipo.
Hayo ndio mambo ya msingi yanayotofautisha Communism/ Ujamaa vs Capitalism. China na Tanzania bado wanafuata hayo yote, Tofauti na nchi za Kibepari ambako ardhi ni bidhaa sawa na bidhaa yoyote ile, Leo hii ukiwa na pesa unaweza kwenda Marekani ukajinunulia kisiwa chako bila hata kuwa raia.
