Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

jamani nipo hapa na update list ya Baraza la Mawaziri kwani iliyoko mzungokoni inakosa majina na baadhi ya wizara hazijatajwa. Angalia KLH News nikiwa nafanya update news live... nikimaliza nitaikopy hapa.
 
JK kweki hayuko serious- bado ni usanii tuu??

A: Out so far ni hawa!

1. Kingunge
2. Mungai
3. Msolwa
4. Mapachu
5. Mramba
6. Meghji
7. Karamaji
8. Msabaha
9. Lowasa

B: Wapya (In)
1. Mama Nkya- (Naibu)
2. HAMISI KAGASHEKI (naibu)
3. Malima (Naibu)

C: Manaibu walifanywa Mawaziri kamili
1. Mustafa Mkulo
2. Kamala
3. Ngeleja
4. Chikawe

D: Wengine wamebadilishwa tu wizara

However- are these major changes?


Yes those are major changes!!! BUT the question is, are those changes, EFFECTIVE????
 
Mbona hili si baraza jipya la mawaziri,Ni viraka vimebandikwa kwenye lile vazi la zamani!! Adam MALIMA???Mbunge wa Mukuranga???Tunasubiri maajabu na miujiza ya maisha bora!!
This might b the weakest cabnet ever,Is this what we are waiting so long??woe to Tanzania,The way of uprightness is like the light of early morning, getting brighter and brighter till the full day.
This has shown how ruling party decides in critical situation itching the nations.
DR.Mwinyi na DR Nchimbi wizara ya ulinzi??hawa vijana wataweza kusimamia maswala ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama??
Sitaki kuamini sasa hivi kwamba kuna jipya,Time will tell

Watanzania mtapigwa migumi na mateke na kuwa hoi bin taabani lakini mkibembelezwa kwa pipi tu!!Mnaanza kumpigia makofi mtu aliyewakudunda na kusahau kila kitu.
Watu husema Oooh upinzani ukipewa nchi wataunda vipi baraza la mawaziri.Wapinzani watakapoweza kushinda kwanza watakuwa na watu wa wabunge wa kutosha tena ambao ni makini na wenye uwezo.Pili hakuna haja ya kuwa na baraza kubwa namna hii.CCM pamoja na kuwa na wabunge wengi,wengi wao ni wabovu na hawafai kuwa mawaziri.Matokeo ndo haya ya kuwachukua akina Malima,Nchimbi etc.Uwanja wa kutafuta watu wenye uwezo na wasio na matatizo uko very limited.

Kwa kweli ndani ya hili baraza wengi wao siwafahamu vizuri uwezo wao kiutendaji na hivyo nakuwa mzito kuamini kama kutakuwa na maboresho katika utendaji na uadilifu.
 
Hakuna lolote hapo...majina yaleyale kila siku. Hivi hakuna mtu anayeweza kufanya kazi nzuri zaidi ya Wassira au Kapuya? What the hell....
 
kweli wabunge wa ccm hamna kitu....kiasi cha kuwa JK anapata tabu ya kuchagua watendaji na anatufanyia recycle za pale kwa pale kila siku
 
JF, let us fortify ourselves with weapons,The battle has been declared to our fate,Tutegemee kipi kutokana na baraza hili??
Hata chenge naye kashika kaba rofu?
 
Kwa mtazamao wangu, nchi yetu kwa sasa inahitaji mawaziri ambao hawamuonei noma hata Rais pale wanapohisi amechemsha. Rais angekuwa na ujasiri wa kutosha cabinet yake ingemu include Mama Anne Kilango na Dr Mwakyembe, watu ambao nimelazimika kuwapenda recently kwa jinsi walivyoweka utaifa mbele na kusahau itikadi za chama chao za kulindana. Pia mtu tough kama J.P Magufuli alitakiwa apewe Wizara nzito na nyeti, kumpeleka kwenye Uvuvi na Mifugo ni sawa na kumhamisha polisi wa cheo cha juu toka kwenye kazi yake na kumpeleka awe mshauri wa mgambo Lindi au Kibondo.
 
JK kwa hakika hayuko seious hata kidogo

Sitta alikuwa anaenda vizuri na Elimu sasa ???????

Magufuri alikuwa anaenda vizuri na Aridhi sasa ?????

Bad cabinet

I_see_dumb_people_o_O_by_cool_slaye.jpg
 
Naweza kusema nimechoka na baraza hili. So far naona kizunguzungu tu, i wonder kama mabadiliko hayo lengo lake ni ku-apease wana mtandao na CCM asili, au yalilenga kuangalia weakness zilizopita na kuhakikisha utendaji unakuwa mzuri zaidi, au ni kuwaweka tu ili 2010 ifike halafu tuangalie mapya.
Nimeshangazwa sana na Magufuli kuhamishwa wizara ya Ardhi, i wonder kama kutakuwa na consistency ya utekelezaji na ufuatiliaji wa mambo yanayokuwa initiated na mawaziri, kama kwa miaka minne mtu anakuwa kwenye wizara tatu tofauti. Labda tuwe na muda zaidi tuweze kudigest haya, may be we will see a sense of it. Kwa sasa i can not see any!
 
Mbona hili si baraza jipya la mawaziri,Ni viraka vimebandikwa kwenye lile vazi la zamani!! Adam MALIMA???Mbunge wa Mukuranga???Tunasubiri maajabu na miujiza ya maisha bora!!
This might b the weakest cabnet ever,Is this what we are waiting so long??woe to Tanzania,The way of uprightness is like the light of early morning, getting brighter and brighter till the full day.
This has shown how ruling party decides in critical situation itching the nations.
DR.Mwinyi na DR Nchimbi wizara ya ulinzi??hawa vijana wataweza kusimamia maswala ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama??
Sitaki kuamini sasa hivi kwamba kuna jipya,Time will tell

No_Country_for_Old_Men_poster.jpg
 
Sasa Mkuu hapa si tutakufa njaa mwaka huu?
Kama kavuruga namna ile elimu ya juu, itakuwaje kwa kilimo ambacho mpaka sasa kinachechemea?


Msolla ni Prof wa Kilimo..asipoweza kutumia akili yake hapo sasa basi sijui watanzania tumfanye nini..!!
 
Sijui kama tutafika kwa mtindo huu ambao JK anaenda nao. Mimi nadhani ipo haja ya Katiba kuangaliwa upya ili tuweke mambo sawa sawa kwa kila rais anayeingia madarakani aifuate.

ipo haja ya kuwa na notice board ndani ya ikulu inayoelezea mambo ambayo seikali ifanye (guidelines) to any president.

mambo hayo ni pamoja na
1) Idadi ya wizara
2) Idadi ya manaibu waziri ktk kila wizara
3) Majina ya wizara
4) Sifa za mawaziri wanaotakiwa ktk kila wizara (respectively)
6) Shughuri za kila wizara
n.k
Hii kazi ifanywe na professionals waliobobea ktk masuala ya Uchumi, siasa, technology, business, kilimo, nishati, habari n.k
Hii itapunguza kuwa kila rais anakuja na version yake ya majina ya wizara, idadi na sifa. Ipo siku atakuja rais mwendawazimu ataweka wahuni wote ndani ya baraza na hatutalalamika kwa sababu kila kitu ameachiwa yeye.
 
Baraza hili "la zamani"la mawaziri hatuna imani nalo. Rais Kikwete hapa hakufanya kazi yake vizuri. Baraza hili halitaweza kurudisha hadhi ya serikali. Ni kama kwamba rais J.kikwete amedharau MATAKWA YA WANANCHI. Tanzania ina wananchi 30 million si lazima kila siku mawaziri wawe ni hao hao.
BARAZA HILI LA MAWAZIRI HALIFAI KABISA NA UFISADI UTAENDELEA ZAIDI.Sasa wamekwisha fahamu ni njia gani watumie bila ya kushikwa.
MHESHIMIWA KIKKWETE NI KAMA MFA MAJI SASA HIVI. ANA TAPA TAPA NA HAJUWI AFANYEJE. AKIPIGA MBWIZA ANAKUFA MAJI NA MAWIMBI MAKALI YANAENDELEA KUJA.
 
JK kweki hayuko serious- bado ni usanii tuu??

A: Out so far ni hawa!

1. Kingunge
2. Mungai
3. Msolwa
4. Mapachu
5. Mramba
6. Meghji
7. Karamaji
8. Msabaha
9. Lowasa

B: Wapya (In)
1. Mama Nkya- (Naibu)
2. HAMISI KAGASHEKI (naibu)
3. Malima (Naibu)

C: Manaibu walifanywa Mawaziri kamili
1. Mustafa Mkulo
2. Kamala
3. Ngeleja
4. Chikawe

D: Wengine wamebadilishwa tu wizara

However- are these major changes?

Hapo kwenye OUT umewasasahau;
1.Anthony Diallo
2.Ngasongwa
3.Ritta Mlaki
 
Watanzania bwana !!!!!!!!!!!!.

Wakati wa kipindi cha Mkapa, Magufuli alikuwa wizara ya Ujenzi. JK alipomchagua kuwa wizara ya Ardhi watu walilalamika kuwa angebaki ujenzi. Alipofika wizara ya ardhi na kuonyesha uwezo wake, watu hamtaki aondoke na kwenda wizara nyingine.

Kinachotakiwa ni kila mtu katika nafasi yake afanye juhudi za kufanya kazi kama Magufuli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom