Kama cheo cha Naibu Waziri kina tija kwa taifa kwanini hakiingizwi kwenye katiba?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,035
Ni safari ya pili sasa Cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinatumika ktk Baraza la Mawaziri.

Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Utawala wa Awamu ya PILI Rais Ally Hassani Mwinyi alimteua Hayati Augustino Mrema, lakinu hata Majukumu ya Cheo hicho hatukuwahi kuyafahamu.

Mrema Ali hudumu na mwisho wa siku akataka ALIPWE Mafao ya Cheo hicho lakini aliambiwa aonyeshe kwenye KATIBA kifungu kinachoainisha Mafao ya Naibu Waziri Mkuu.

Serikali ya Awamu ya 6 imemteua tena Naibu waziri mkuu kama vile vile ilivyokuwa kwa Mrema kujua Majukumu yake ni shida kwani nae Cheo hicho hakimo kwenye Katiba.

Najiuliza kama kuna Umuhimu wa kuwa na Cheo hiki kwanini Hakiingizwi kwenye KATIBA ili Majukumu yake yaainishwe na Mafao ya Cheo hiki yajulikane?

Kwanini tunataka yajirudi ya Mrema kudai Mafao ya Cheo hiki wakati KATIBA haikutambui?

Tunashauri kama ni Lazima kuwe na NAIBU Waziri Mkuu basi Cheo hiki kiingizwe kwenye KATIBA.
 
Inawezekana cheo cha Naibu Waziri Mkuu kikawa na matatizo.

Lakini, hoja yako haina mashiko.

Kwa sababu, si vyeo vyote vimetajwa kwenye katiba.

Na katiba hiyo hiyo imempa nguvu rais kuunda na kuvunja vyeo anavyotaka.
 
Cheo kina matatizo makubwa mawili
1.Majukumu ya cheo
2.Mafao ya Cheo
 
Cheo kina matatizo makubwa mawili
1.Majukumu ya cheo
2.Mafao ya Cheo
1.Majukumu ya cheo yanaweza kuwa ni kumsaidia Waziri Mkuu katika kazi zake zote.

2. Biteko tayari ana mafao ya Uwaziri, hawezi kuwa na mafao mara mbili serikalini. Hata mshahara halipwi mara mbili.

3. Vyeo vingine ni vya kisiasa zaidi hivi, inawezekana mteuaji na mteuliwa washakubaliana.

Hutakiwi kusema cheo kina matatizo wakati katiba imempa rais nguvu za kuunda na kuvunja vyeo kwa jinsi anavyotaka.

Yani rais ana uwezo wa kuunda cheo na kusema majukumu yake mengine yako classified, anajua aliyeteuliwa, na mafao anayajua aliyeteukiwa.

Na wewe usiwe na cha kuhoji.

Kwa katiba yako ya sasa.

Sasa, hapo hoji katiba ilivyompa rais nguvu, ukihoji majukumu na mafao hayo mambo wala si lazima uyajue.
 
Ninaposema kina matatizo ni kama pale Mrema alivyohangaika kudai mafao ya cheo hicho kingekuwa kipo kwenye katiba asingehangaika vile mpaka akafa bila kulipwa
 
Kwa hiyo mtu akilalamikia mafao tu cheo kina matatizo?

Unajuaje kama Mrema mwenyewe sio mwenye matatizo hakuelewa cheo cha kisiasa tu hakina mafao?

Unajua Dr. Slaa alikuwa balozi wa kisiasa, hakuwa na mafao, na hakulalamika, kwa sababu alielewa kuwa cheo kile kikikuwa ni cha kisiasa tu?
 
Kwani yeye anajua kazi za Waziri wa nchi Kazi Maalumu Mzee George Mkuchika!
 
Ninaposema kina matatizo ni kama pale Mrema alivyohangaika kudai mafao ya cheo hicho kingekuwa kipo kwenye katiba asingehangaika vile mpaka akafa bila kulipwa
Kwani Mzee Mkuchika Waziri wa nchi Kazi Maalumu na yeye ana majukumu gani na mafao yake yakoje!
 
Kwa hiyo mtu akilalamikia mafao tu cheo kina matatizo?

Unajuaje kama Mrema mwenyewe sio mwenye matatizo hakuelewa cheo cha kisiasa tu hakina mafao?

Unajua Dr. Slaa alikuwa balozi wa kisiasa, hakuwa na mafao, na hakulalamika, kwa sababu alielewa kuwa cheo kile kikikuwa ni cha kisiasa tu?
Waziri wa nchi Kazi Maalumu Mzee George Mkuchika na yeye kazi zae ni zipi!
 
Ni safari ya pili sasa Cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinatumika ktk Baraza la Mawaziri.

Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Utawala wa Awamu ya PILI Rais Ally Hassani Mwinyi alimteua Hayati Augustino Mrema, lakinu hata Majukumu ya Cheo hicho hatukuwahi kuyafahamu.

Mrema Ali hudumu na mwisho wa siku akataka ALIPWE Mafao ya Cheo hicho lakini aliambiwa aonyeshe kwenye KATIBA kifungu kinachoainisha Mafao ya Naibu Waziri Mkuu.

Serikali ya Awamu ya 6 imemteua tena Naibu waziri mkuu kama vile vile ilivyokuwa kwa Mrema kujua Majukumu yake ni shida kwani nae Cheo hicho hakimo kwenye Katiba.

Najiuliza kama kuna Umuhimu wa kuwa na Cheo hiki kwanini Hakiingizwi kwenye KATIBA ili Majukumu yake yaainishwe na Mafao ya Cheo hiki yajulikane?

Kwanini tunataka yajirudi ya Mrema kudai Mafao ya Cheo hiki wakati KATIBA haikutambui?

Tunashauri kama ni Lazima kuwe na NAIBU Waziri Mkuu basi Cheo hiki kiingizwe kwenye KATIBA.
Usiamini kinachosemwa na CCM, CCM wamebaki kuwa kikundi cha kupe, ambao wanaiitaji nchi ili waiishi, usalama wao na uchumi unategemea kuendelea kuwa madarakani, nje ya hapo, ni kifo au jera!
 
Inawezekana cheo cha Naibu Waziri Mkuu kikawa na matatizo.

Lakini, hoja yako haina mashiko.

Kwa sababu, si vyeo vyote vimetajwa kwenye katiba.

Na katiba hiyo hiyo imempa nguvu rais kuunda na kuvunja vyeo anavyotaka.
Hiyo sentensi yako ya mwisho ndio tatizo la nchi yetu lilipo... Tunatakiwa tuwe na katiba itakayomzuiya Rais kufanya anavyotaka na wakati wa kutengeneza katiba husika ni jana
 
Ni safari ya pili sasa Cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinatumika ktk Baraza la Mawaziri.

Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Utawala wa Awamu ya PILI Rais Ally Hassani Mwinyi alimteua Hayati Augustino Mrema, lakinu hata Majukumu ya Cheo hicho hatukuwahi kuyafahamu.

Mrema Ali hudumu na mwisho wa siku akataka ALIPWE Mafao ya Cheo hicho lakini aliambiwa aonyeshe kwenye KATIBA kifungu kinachoainisha Mafao ya Naibu Waziri Mkuu.

Serikali ya Awamu ya 6 imemteua tena Naibu waziri mkuu kama vile vile ilivyokuwa kwa Mrema kujua Majukumu yake ni shida kwani nae Cheo hicho hakimo kwenye Katiba.

Najiuliza kama kuna Umuhimu wa kuwa na Cheo hiki kwanini Hakiingizwi kwenye KATIBA ili Majukumu yake yaainishwe na Mafao ya Cheo hiki yajulikane?

Kwanini tunataka yajirudi ya Mrema kudai Mafao ya Cheo hiki wakati KATIBA haikutambui?

Tunashauri kama ni Lazima kuwe na NAIBU Waziri Mkuu basi Cheo hiki kiingizwe kwenye KATIBA.

CCM imeifanya nchi kuwa pagale ambalo watawala huweza kuweka kila aina ya takataka wanayoitaka.

Hiki cheo cja naibu Waziri Mkuu ni miongoni mwa takataka ambazo marais toka Zanzibar wanazitumia kuwapumbaza Watanganyika.
 
Back
Top Bottom