Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Mkuu,
Ukisema hivo utamfutia kiki Mzee Kingunge, mzee wa pumzi.
Maana yeye ni mzee kuliko Mwapachu, na wote wamehama ccm kipindi kimoja ili kumpa support boss lowassa.
Tukifuat 'lojik' yako ya umri, Kingunge atakuwa na stress kubwa sana na 'memory' mbaya kuliko Mwapachu.
Kingunge ni level nyingine kabisa
 
Mwapachu yuko exactly kama walivyo wana CCM walio wengi..
ni kuwaza kupiga dili kutwa
si ajabu na leo kuna fungu kapewa la kurudi CCM
Unamaanisha hata na wale ambao hawajarudi?
 
Kuna dubwana moja linaitwa mfumo, ogopa sana hilo lidude la ajabu lisilokuwa na sura nzuri. Lina mkono mrefu sana sio mchezo. EL wakati wa kampeni alikuwa hoi kiafya, leo hii tabasamu la ujana limerudi. Achana kabisa na hilo lidubwana la ajabu.
 
Watu wengi waliamini EL anashinda akiwemo huyu mwapachu. Na ikawa hivyo. Bahati mbaya hakupewa nchi
Sio watu wengi tu walioona hivyo hata Mwapachu mwenyewe kwenye hotuba yake ya kurudi ccm amesema hivyo hivyo kuwa yeye na marafiki zake waliona wazi Lowassa anashinda na asingekosa ubalozi.

Hii ina maana baada ya utawala kumweka benchi kipindi kirefu tamaa ya madaraka na marupu rupu iliwaka moyoni mwake.Unajua anaweza asisumbuliwe na utawala kwenye biashara zake na hata marafiki zake lakini faida za biashara peke yake zisingemtosha kwani alishazoea marupurupu ya serikalini na madili yake na chama kikimkinga kama watoto wa ikulu.

Anasema aliondoka ccm kumuunga mkono Lowassa ila hakujiunga chama chochote cha ukawa alibaki hewani kama popo bila kujulikana msimamo wake. Leo karudi ccm na kuchangia millioni moja kuinua tawi lake.

Ukawa aliwachangia nini au alikuwa shushushu wa kutumwa tu na ndio maana wala ukawa hawakuhangaika nae.Chezea inteljensia ya Mbowe wewe.

Nimesoma mahali fulani ccm wakisema eti ukawa wamemkosa Mwapachu sasa waonyeshe ni wapi walipompokea na kuwa nae hata wajute kumkosa?

Huyu kama alivyosema mwanakijiji alikuwepo kuwepo tu akisumbuliwa na tamaa zake za madaraka.

HALIPO LA KUJIFUNZA TOKA KWAKE.
 
Alivyokuja tulimshangilia.....sasa anarudi tunamzomea....

Haya Masha, Mpendazoe, Mahanga, Msindai, Lembeli na nyie tieni maji
Ha ha ha ha ha ha kwamba wakati wao umefika...Kina Mngeja wamekula sana hela ya braza Eddo
 
Waswahili wanasema "Ukitaka kuruka agana na Nyonga". Mzee alikurupuka sana bila ya kujua Mwenzie Kingunge aliondoka baada ya Mkwere kumnyang'anya Miradi yote kuanzia Ubungo bus terminal na Parking hakuwa na cha kupoteza. sasa yeye kakurupushwa na Maigizo ya kufagia barabara. Aliwaiga kina Rostam na Minywele wenzie wana reserve kama Petrol reserve ya America.

Bora warudi huko huko ccm tena hata Lowassa arudi huko huko ccm maana ndio nyumbani kwao. Huku upinzani watu wanagawana majukumu na sio vyeo. Ila viongozi wacdm walitoka kwenye mstari na lugha za kihuni sijui kubadilisha gia angani nk. Tena viongozi wa cdm wakae sawa huku tunakokwenda ni lazima tuwape ukweli wao, hatuna muda wa kuendekeza siasa za tumbo kwa maelezo ya kihuni, vinginevyo tunawapotezea japo ccm ni mwiko kuisupport kwani hatuna nasaba nayo.
 
Hivi kwani ilikuwa lazima arudi CCM?

Hiki kibabu kinazeeka vibaya sana.
 
Bora warudi huko huko ccm tena hata Lowassa arudi huko huko ccm maana ndio nyumbani kwao. Huku upinzani watu wanagawana majukumu na sio vyeo. Ila viongozi wacdm walitoka kwenye mstari na lugha za kihuni sijui kubadilisha gia angani nk. Tena viongozi wa cdm wakae sawa huku tunakokwenda ni lazima tuwape ukweli wao, hatuna muda wa kuendekeza siasa za tumbo kwa maelezo ya kihuni, vinginevyo tunawapotezea japo ccm ni mwiko kuisupport kwani hatuna nasaba nayo.
Unataka arudi CCM rais Wa mioyo ya watu!!! Mwenye maono,anayeiweza Tanzania acha basi hizoo.
 
Kaambiwa arudi ili apewe kazi maalum, ikiwezekana hata ubalozi nje ya bongoland.
Hizo tetesi ni za kweli japo sioni impact yake UKAWA wala huko CCM yaani huyu mheshimiwa maarufu huko wanabidii zaidi ya hapo ni kama mimi tu hatuna umaarufu
 
Ungevuta muda kidogo mzee mwapachu..mbona umerudi mapema sana. hata mwaka haujatimia..?
 
Magufuli akimpa Huyu mtu cheo nitashangaa sana! Hivi kweli mwapachu alisema aliyoyasema! Mpaka siamini macho yangu!
 
Back
Top Bottom