Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,237
- 44,470
Yaani, mnawafundisha hawa vijana vitu gani nyinyi? Mnataka Taifa liwakumbuke kwa yepi hasa? Majina yenu tu? Mnataka tutakapoandika historia tuseme na wao walikuwepo? Binafsi sina tatizo kabisa na wewe kurudi CCM au kuachana na CCM kabisa au kujiunga na chama kingine chochote kwani hilo ni suala la hiari ya mtu. Sikusema lolote ulipoondoka kwani sikuwa shahidi ulipoingia ilikuwaje.
Kujiunga na chama cha siasa ni hiari ya mtu na ni sehemu ya demokrasia ndio maana sijali sana watu kutoka au kujiunga na chama chochote.
Kitu ambacho kimenitibua sana ni maelezo ya kwanini umeamua kurejea! Maelezo yako yanaonesha kitu kimoja cha hatari kabisa; wewe si mtu wa kanuni na mwenye kusimamia unachosimamia.
Maelezo yako yanaonesha pia kuwa wewe si mtu wa tafakari makini na mwenye kupima matokeo ya maamuzi yako mbalimbali. Umejionesha tu ni mtu wa kuongozwa na hisia na kufuata upepo; ni kama kijana mdogo ambaye anahitai kuendelea kufunzwa. Hili naona ni la kuudhi na kutisha zaidi.
Hata sasa swali kubwa linalobakia ni kuwa je tunaweza kukuamini; je tunaweza kuamini kuwa unasema kweli sasa? Je umejionesha kuwa unaweza kuaminika; mtu yeyote anayekuita rafiki anaweza kukuamini sasa na akaingia mapatano nawe?
Binafsi naamini – na inaonekana mwenyewe umegundua hilo – umeonesha mfano mbaya kama kiongozi mkongwa; umeonesha ukosefu mkubwa wa hekima na zaidi umeonesha udhaifu mkubwa wa kusimamia mambo uliyoyaamini.
Sidhani kama hadi hivi sasa kuna lolote ambalo CCM kama chama imelifanya ambalo lingekubadili mawazo; na umesema kweli kuwa sasa umerudi kumfuata mtu kama ulivyoondoka kumfuata mtu; hii ni aina mbaya kabisa ya uongozi tunayotaka kujenga nchini.
Watu wasio na kanuni na maadili ya kuaminika wanaweza vipi kusimama na kujionesha kuwa wanaweza kuaminiwa na kuwa wana kanuni?
Binafsi naamini badala ya kujaribu kuzengea nafasi fulani mahali fulani wakati huu ungeamua kujiendeleza na mambo yako na kuachana na siasa ili angalau uonekane umeaminika. Ni matumaini yangu Magufuli hatowazawadia watu wa aina yako kwani taifa letu linahitaji viongozi bora na siyo bora viongozi; tunahitaji watu ambao watasimama kama mifano kwa vijana na vizazi vijavyo badala ya kuja kutajwa kama viongozi waliowahi kuwepo kuwepo na siyo walikuwepo viongozi viongozi!
Kusamehewa najua wengi tutakusamehe; lakini hatuwezi kukuamini hadi ujioneshe unaweza kuaminika kweli. Kwa hayo uliyoyaseme leo kuwa yaliyopita si ‘ndwele’ tugange yajayo; mmh! Tafadhali Balozi Mwapachu!
MMM
Note: Imehaririwa kuakisi maelezo ya Mwapachu kuwa taarifa iliyokuwa inasambaa siyo yake; mantiki ya ukosoaji wa maamuzi yake bado inasimama na hata maelezo yake ambayo yamepatikana hadi hivi sasa bado yanasimama na ukosoaji huu.