Watu wa aina ya Balozi Mwapachu wanawavuruga sana vijana Watanzania!
Fikiria kuna watu walikuwa wanapiga kelele za kumpongeza sana siku ambalo aliachana na CCM. Leo pia wanapiga kelele ya kumdharau katika maamuzi yake huku wengine wakiachwa na mshangao.
Mbaya zaidi anawaambia yaliyopita si ndwele, tugange yajayo!
Misemo ya Kiswahili inakuwa na maana inapotumiwa inavyotakiwa.
Mtu anayehama CCM na kurudi back CCM, kama ana akili timamu, anatakiwa kutosema habari hiyo. Wanaompokea CCM ndio wanaotakiwa kusema kama yaliyopita ni ndwele au si ndwele.
Alichosema Mwapachu ni kama mtu kakuzaba kibao wakati anafikiri wewe mtoto, halafu anapoona kumbe wewe ndiye baba mwenye nyumba akwambie yaliyopita si ndwele.
Kama kuna mtu wa kusema yaliyopita si ndwele hapa, ni yule anayesamehe.
Anayesamehewa hawezi kuchagua tu kwamba nini ni ndwele na nini si ndwele.
Ataambiwa "Mla ndizi husahau, lakini mtupa maganda hasahau".
Tunajua asiyekubali kushindwa si mpinzani lakini kujirudi huku kwa baniani mbaya, kiatu chake dawa na kumtukana mamba kabla ya kuvuka mto ni ishara ya bendera kufuata upepo iliyo katika chombo kinachozama kisicho usukani.
Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua na kanga hazai ugenini kama jogoo la shamba haliwiki mjini.
Maneno mema humtoa nyoka pangoni, lakini la kuvunda halina ubani na maji yakimwagika hayazoleki.