Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Zipo taarifa za chini kwa chini zinazodai kuwa Balozi Juma Mwapachu ana mpango wa kurejea CCM. Mpaka sasa bado haijafahamika ni sababu zipi hasa zilizompelekea kufikia uamuzi huo.

Itakumbukwa kwamba wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Balozi Mwapachu alirudisha kadi za TANU na CCM na kutangaza kumuunga mkono aliyekuwa mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.

=======

UPDATES:

NOTE: Kulikuwa na tamko la awali likimhusisha Mh. Edward Lowassa; Balozi Mwapachu amekana kuandika tamko hilo ingawa kakiri kuwa kweli ameamua kurejea CCM.

image.jpeg

Hatimaye imekuwa kweli. Balozi Mwapachu ametangaza rasmi kurejea CCM

 
Arudi asirudi haongezi value yoyote CCM.Walitutelekezea CCM vitani yeye na akina kingunge na akina Sumaye tumepigana wenyewe tumeshinda.Sasa ni HAPA KAZI TU.Atajijua yeye na wenzie waliotusaliti na kusaliti CCM kwenye vita ya uchaguzi.
Hata huku UKAWA hatuoni impact yake, hivi baada ya kurudisha zile kadi alisema anaenda wapi?
 
Imekuaje tena huko,wamemuomba hela nini?maana jaama kwa kukaba hawajambo.Kaenda chama cha wanyang'anyi,anategemea nini? Hesabu zimegoma. hahahahha.
 
Sitawashangaa kwa propaganda zenu hizi. kwani mlianza wakati wa kampeni kuwa LOWASA endapo akishindwa kupata uraisi atarudi CCM kwani kule CDM amefuata cheo na siyo uanachama wa CDM.

Mkapatwa na aibu kubwa sana baada ya kuona kuwa mh. Lowasa bado yupo ngangari ndani ya CDM pamoja na UKAWA bado inadunda tu.

Mlipatwa na AIBU KUBWA SANA majuzi mlipomuona Mh. Lowasa akiwa katika mkutano mkuu wa CHADEMA pale jijini MWANZA.

Mlipata aibu kubwa majuzi mliposhuhudia mama Regina Lowasa akiwa na BAWACHA pale hospitali ya Morogoro wakifanya usafi pamoja na kutoa misaada katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.

NI AIBU YENU MILELE.

BADO MTASEMA MENGI.
Hakuna Kulala.jpg
 
Back
Top Bottom