MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Hii dhana ya kuhama hama kwa mtu mwenye umri wake na heshima zake ni kujidhalilisha.Misemo ya Kiswahili inakuwa na maana inapotumiwa inavyotakiwa.
Mtu anayehama CCM na kurudi back CCM, kama ana akili timamu, anatakiwa kutosema habari hiyo. Wanaompokea CCM ndio wanaotakiwa kusema kama yaliyopita ni ndwele au si ndwele.
Alichosema Mwapachu ni kama mtu kakuzaba kibao wakati anafikiri wewe mtoto, halafu anapoona kumbe wewe ndiye baba mwenye nyumba akwambie yaliyopita si ndwele.
Kama kuna mtu wa kusema yaliyopita si ndwele hapa, ni yule anayesamehe.
Anayesamehewa hawezi kuchagua tu kwamba nini ni ndwele na nini si ndwele.
Ataambiwa "Mla ndizi husahau, lakini mtupa maganda hasahau".
Tunajua asiyekubali kushindwa si mpinzani lakini kujirudi huku kwa baniani mbaya, kiatu chake dawa na kumtukana mamba kabla ya kuvuka mto ni ishara ya bendera kufuata upepo iliyo katika chombo kinachozama kisicho usukani.
Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua na kanga hazai ugenini kama jogoo la shamba haliwiki mjini.
Maneno mema humtoa nyoka pangoni, lakini la kuvunda halina ubani na maji yakimwagika hayazoleki.
Wazee kama Jaji Warioba au Butiku wako CCM sio kwa sababu CCM inafanya mambo mazuri sana, La hasha. Wameendelea kuwa wanaCCM kwa sababu heshima yao wameipata ndani ya CCM.
Halafu huyu Mzee ametoa rushwa ya shilingi milioni moja kwenye tawi ili zitumike kukarabati jengo la ofisi ya tawi.
Mwangalie kwenye hii video wakati akitoa rushwa baada ya kukaribishwa tena ndani ya CCM.
Labda hii rushwa ya shilingi milioni moja ndiyo imepelekea kusema maneno kama Yaliyopita si ndwele...