Lowassa alikipenda kiti moto kipindi!. Aliokoa maisha yangu Rome Italy!. He was "Of the People, By The People, & For The People!" ADIOS... AMIGOS...!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,
IMG-20240216-WA0113.jpg

1708893441136.png



Huu ni mwendelezo wa Tribute to Edward Lowassa ilianza wiki iliyopita TRIBUTE: Pumzika Lowassa. Kazi umekamilisha, umeacha alama, mwendo umeumaliza. Watanzania wazalendo tutakukumbuka daima-1

Kwa wasomaji wapya , huu ni mwendelezo wa jinsi nilivyokutana na Edward Lowassa nikihusisha visa na mikasa ya hapa na pale.

Wiki iliyopita tuliishia nikiwa TBC, umekuja mwaliko wa Wiki ya Maji, nika lobby trip, ofisi haina mtu wa camera, nikabeba camera yangu, kufika eneo la tukio, ili niweze kulipwa double na kurudishiwa nauli ya ndege ya watu wawili, nikam set kijana mmoja hawa wapiga picha kwenye mikutano na kuzipanga chini, nikamtengenezea kitambulisho cha mtu wa TBC, nikampa, dili ya kupiga pesa ikapita, jamaa alipovuta tuu ule mshiko, alitokomea kusiko julikana na kile kitambulisho.

Kumbe yule jamaa kile kitambulisho amekifanya dili, akatinga jijini Dar es Salaam na kuhudhuria matukio mbalimbali akijifanya ni mtu wa TBC!.
Sasa endelea
.
Kumbe yule jamaa kile kitambulisho amekifanya dili, akatinga jijini Dar es Salaam na kuhudhuria matukio mbalimbali akijifanya ni mtu wa TBC!.

Za mwizi 40, siku ya siku jamaa katinga tukio na kitambulisho chake fake, kajisajili, kumbe siku hiyo aliyepangwa tukio hilo ndio yule Cameraman mwenyewe ambae kanjanja anatumia jina lake. Mtu halisi wa TBC alipojisajili akaambiwa huyu jamaa ameisha jisajili hatuwezi kukusajili mara mbili, hivyo akakataliwa kuingia.

Ilikuwa ni tukio la muhimu likinuhusisha kiongozi mmoja kati ya wale viongozi wetu wakuu, hivyo TBC hawawezi kuikosa hiyo story, tukio likaripotiwa ofisini, ofisi ikaripoti polisi, kanjanja akasakwa, akasakwa akawekwa chini ya ulinzi, mtu halisi wa TBC akaruhusiwa kuingia ku cover story.

TBC Moto Ukaniwakia!
Yule jamaa katika mahojiano akanitaja, hivyo na mimi nikafuatwa ofisini niunganishwe kesi ifunguliwe.

Kumbe kuna mlolongo wa tarajiwa za kijinai za kumshitaki mtumishi wa umma permanent and personable, wakati taratibu za kujinai zinaendelea, yule jamaa akajiongeza, akawapanga polisi, wakapangika akaachiwa!, hapa naamini utakuwa ni unajua ni nini kilifanyika!.

Wakati taratibu za kuniunganisha zimekamilika, kule polisi kukakutikana hakuna ushahidi wowote, faili halionelani, na yule jamaa ameyeyuka kwenye mahabusu ya polisi, no any records, atakuwa ameshauriwa salama yake ni apotee!, ahame mji asionekane popote, kweli jamaa akapotea issue ikafa.

Japo issues ilipotezewa kule polisi, huku kazini kwangu TBC moto uliendelea kuniwakia, kwenye taarifa yangu ya utendaji wa kazi, zile fomu zangu za OPRAS zikachafuliwa vibaya sana!, mimi nikagoma kusaini, najua sheria inanilinda na inamruhusu mtumishi kutosaini fomu zile ukijiona hujaridhika na ile assessment yako.

Nikaitwa kwa Mkurugenzi na meneja na mkuu wa Idara na kuelezwa the consequences za kukataa amri halali ya kulazinmishwa kusaini opras, nikajibu I'm ready!. Kilichofuatia baada ya hapo ni barua ya Summary Dismissals kwa kosa la insubordination!. That was my sad ending with TBC!.
Somo hapa ni mtu unaweza kutenda kitendo kidogo tuu cha deal mbuzi ili kuvuta pesa mbuzi kikaja kukugharimu big time kwenye career yako au maisha yako!.

Lowassa Aokoa Maisha Yangu Rome Italy.
Baada ya kisa hicho, mimi na familia yangu niliamua kuhama nchi, nikaanzia UK, then US family ilasettle, mimi sasa nikawa na hanja hanja kutafuta wapi haswa kuna greener pastures. Nikajaribu Sweden, Germany, Holland, Swiss, nikatua Rome Italy.
Kote ninamopita najichanganya na Watanzania na bado na maintains Press Card yangu always to gain the easy access ya tukio lolote.

Nikiwa Rome, kukafanyika mkutano wa Kimataifa wa World Food Day 10-years After, Tanzania ikatuma a very strong delegation. Mimi nika register kama Journalist from Tanzania.

Siku ya mwisho ya mkutano, I don't know what really happened to me mpaka kesho, nikiwa press gallery ni with my mac computer, camera, na begi, I just passed out!.

Kuzinduka ni nazinduka niko Hospital kubwa ya Rome, nimezungukwa na kundi kubwa la watu, Waziri Lowassa, Waziri Anna Tibaijuka, Balozi wa Tanzania nchi Italy wakati huo, Balozi Prof. Costa Rick Mahalu.

Ndio naelezwa nikiwa chumba cha waandishi nilizimika ghafla nikaanguka, nikakimbizwa hospital . Press pass yangu ikaonyesha ni Mtanzania, ubalozi wakaarifiwa ndio kisa cha kuzungukwa vile.

Hapo Hospital nimepatiwa tuu huduma ya kwanza, sikuwa na travel insurance, and not part of Government Delegation. Nikaulizwa hali yangu, najisikia Fresh tuu, natakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina sina bima.

Lowassa akamuuliza Balozi Mahalu ubalozi unaweza kusaidiaje?. Balozi akamjibu kwa kawaida ubalozi unasaidia watumishi wa umma on official visit, huyu sio mtumishi wa umma na hapa Rome yuko kivyake tuu!.
Ndipo Lowassa akasema huyu Mayalla japo sio mtumishi wa serikali lakini ni Mtanzania mwenzetu, tunamfahamu, tena kile kipindi chake cha Kiti Moto, nilikuwa nakipenda sana, sijui kwanini kilikufa?!. Balozi tafuta namna ya kumsaidia na mkikwama kabisa nijulisheni tutafanya jambo!.

Watanzania ni watu wenye upendo sana wawapo ughaibuni, Lowassa alianzisha harambee ya papo kwa papo, na ubalozi wetu Rome, ukatia mkono, ukaingilia kati kuanzia vipimo, bili yote ya hospitali, nikapimwa nikatibiwa nikookolewa maisha yangu!.

Balozi Mahalu akamua assign afisa ubalozi wetu pale Rome, Adolf Nchemwa, akashughulikia bili zote za Hospital na nilitoka akanichukua kukaa kwake na familia yake yenye mke na watoto wawili mabinti.

From there mimi nikageuka ni Mgeni wa ubalozi nikagharimiwa kila kitu mpaka niliporejea nyumbani Tanzania. Yote haya yalifanyika kwasababu ya Lowassa!, Balozi Mahalu na Adolf Mchemwa!.

Somo hapa Watanzania tuwapo ughaibuni, tujenge utamaduni wa kujitambulisha ubalozini just incase of anything, ubalozi una taarifa zako. Mimi kilichoniokoa kule Italy ni press pass na nilipata msaada kwa hisani tuu ya Lowassa, lakini endapo ningejitambulisha ubalozini ukikutwa na jambo lolote ni rahisi kusaidiwa.

Harusi ya Binti Lowassa
Wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu alioza binti, Binti Lowassa na mimi nilitafutwa kuwa MC wa main event ya harusi ya binti Lowassa. Serikali nzima ilihudhuria na ikatokea tukawa marafiki na Bwana harusi.

From there mimi nikawa kama ni mtu wa Lowassa, hata kashfa ya Richmond ilipoibuka bado tulisimama na Lowassa.

Kufuatia kuwepo kwa dhana ya uchawa kwenye kuwaunga mkono wanasiasa tunaokubali na kuna watu ni wafuasi wa Lowassa wanajiita "Friends of Lowasa" mimi kwa bahati mbaya sikuwa mfuasi wa Lowassa wala siko kwenye kundi la friends of Lowasa kwasababu mimi ni independent, Lowassa akikosea ninamkosoa.

Harakati mbalimbali za Kisiasa za Lowassa Ikiwemo Safari ya Matumaini
.
Kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru, mimi nilisimama na Sioi Sumari, nikamshauri Lowassa Ushauri: Edward Lowassa asikanyage Arumeru, atamponza Sioi ushauri huu haukusikilizwa.

Safari ya Matumaini
Lowassa alipoianza ile safari ya matumaini, tulisimama nae na tukaeleza wazi wazi kumuunga mkono Elections 2015 - Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Japo chaguo la wengi kwa mgombea wa uchaguzi Mkuu wa 2015 alikuwa ni Edward Lowassa, nilipopenyezewa hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli tuliishusha.

Tukawaandaa wafuasi kisaikolojia Elections 2015 - Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais wetu wa 2015 ni...

Tukawaeleza Elections 2015 - Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Na kweli muda ulipowadia ni kweli jina la Lowassa lilikatwa na kwanza tukashauri Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Kisha licha ya kukatwa CCM, bado tulisimama nae Elections 2015 - Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Tumewashauri Chadema wampokee Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!

Tukawasisitizia Chadema kuwa Lowassa ni mtaji Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Wakati wote wa kampeni tulisimama nae Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Na tukamtabiria Lowassa ushindi Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu

Kusema ukweli kabisa siasa ni mchezo mchafu, Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda! na bado kwenye matokeo ya mwisho akishindwa!.

Baada ya matokeo kutangazwa Lowassa akalalamika kuwa ni yeye aliyeshinda, tukasimama nae Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Ila pia tukamshauri ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.

Hivyo alipoitwa Ikulu tulishangaa Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!

Ila pia tukamshauri Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!
Kuugua
Kuna msemo usemao rafiki wa kweli ni wakati wa dhiki, wakati Lowassa anaugua, yale makundi ya watu hayakuonekana tena, hata friends of Lowasa nimekuja kuwaona msibani!, waliokuwa wanahangaika nae ni mkewe, watoto na familia, na marafiki wachache na serikali kumhudumia kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni.

Somo la Kifo cha Lowassa
Somo Kuu la kwanza la kifo cha Mwamba huu ni kijifunza kuweka akiba ya maneno, nikisikiliza baadhi ya clips za wanasiasa jinsi walivyokuwa wanamsema vibaya Lowassa akiwa hai, na sasa wamekuja msibani na kugeuza maneno bila aibu!, tujifunze kuweka akiba ya maneno na sometimes ni bora kunyamaza kimya.

Somo la pili ni kuwa determined, ukidhamiria jambo lako lishikilie, usikubali kukatishwa tamaa. Lowassa was a very determined person.

Somo la tatu ni Lowassa ni mwalimu mkubwa wa siasa za kuwa na kiasi, alikuwa CCM, akafanyiwa figisu akalatwa kwa figusu, akahamia Chadema. Akiwa Chadema hakuisema vibaya CCM, na aliposhindwana na Chadema na kurejea CCM, Lowassa hakuisema vibaya Chadema!. Ni wanasiasa wachache sana wana haiba ya namna hii. Leo kwenye msiba wa Lowassa CCM na Chadema wanashindana kumuenzi kwa kumzungumza kwa wema.

Pumzika Lowassa Pumzika, ulikuwa ni mtu miongoni mwa watu (of the people) na ukawatumikia watu kwa uwezo wako wote kwa kushirikiana na watu (by the people) na ukautoa uhai wako kwa ajili ya watu wako, kwa kifupi ni Lowassa ni ametufia (for the people)

Mwendo umeumaliza, imani umeilinda
Bwana Alileta, Bwana Ametwaa
Jina lake Lihimidiwe...

Adios....
Amigos...!

Paskali
 
Huwa pia nawashauri sana CHADEMA na vijana wake pamoja na viongozi wake kuwa wawe na kiasi katika maneno yao .wasipende kutukana matusi na kumdhalilisha kila mtu kisa tu hayupo upande wao au kwa kuwa wanatofautiana mitizamo. Ndio maana aibu ziliwashika sana mwaka 2015 alipokuja kuwa mgombea wao na kutakiwa kuanza kumsafisha kwa yale yote waliomchafua na kumdhalilisha.

Wanasiasa wote bila kujali vyama vyetu tuwe na siasa za kistaarabu zenye kujikita katika hoja na siyo kudhalilishana kwa matusi na maneno machafu ambayo hayapaswi kutolewa na watu walio staarabika. Tushindane kwa hoja na kushindanisha hoja badala ya matusi.

Hasa vijana ndio tunapaswa kuwa makini sana katika kuchunga ndimi zetu tuwapo majukwaani na mahali popote pale tupatapo nafasi ya kuzungumza au kutoa neno.tusiwe watu wa mihemuko au jazba au hasira katika kuongea.tutoe maneno yaliyo jaa hekima, busara na staha.tuwe na chujio la maneno yetu kabla ya kuyatoa hadharani. Maneno hudumu katika vifua vya watu ,ambapo baadaye yanaweza kuja kukugharimu na kufanya ujute kwanini ulitoa maneno fulani siku fulani.maneno ni kama risasi yakitoka hatarudi kwa hiyo kabla ya kuyatoa tufanye mchujo kutumia akili na siyo hisia.

Hata niliyeandika hapa nami sijakamilika bali naendelea kujifunza na kuomba msamaha pale napokosea au kufanya makosa.
 
Pascal mayala mm ndugu yako, rafiki yako othman Dan fodio nakutafuta ninashida na wewe naomba tuwasiliane kama hutajali ni dm namba yako nikupigie.

Asante.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Mkuu othuman dan fodio, pole sana kunitafuta kwa njia hii!, ili kunitafuta huku pia kumenisaidia kujijua kumbe visibility yangu bado ni very poor!.
Kila Jumatano na Jumapili, nina kipindi cha TV, on Channel Ten, na kuna number zangu,
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=5kk-lx6eg5t7k1oi, hivyo taarifa hii ya wewe kunitafuta, ndio inanijulisha kuwa kumbe kipindi changu on Channel Ten hakiangaliwi!, hivyo ama kipindi kihamie TBC, ITV au Azam TV.

Pia kila Jumatano nina makala gazeti la Mwananchi, ninaweka number yangu, na kila Jumapili, nina makala Gazeti la Nipashe, na ninaweka number yangu!, kunitafuta huku kuna maanisha pia makaza zangu hazisomwi!. Kama Mwananchi ambalo ndilo gazeti number 1 la Kiswahili. No. 2 ni Nipashe!, kama magazeti haya hayasomwi, ni taarifa, muhimu kuwa mainstream media imepungua sana relevance, sasa inabidi nijielekeze Twitter, You tube, instergram na Tick Tock
Number yangu ni 0754/0784- 270403. (anza na sms/ WhatsApp mimi ndio nitakupigia)
pascomayalla@gmail.com
Karibu
Pasco
 
Ni kweli sababu ya kipindi chako ndo sababu ya mbuzi wa kikristo kuitwa kitimoto? Kama ni hivyo basi BAKITA wakutambue
Mkuu MSAGA SUMU , ni kweli mbuzi Katoliki inaitwa Kiti Moto, kwasababu ya kipindi changu cha Kiti Moto, ila jina la Kiti Moto halikuwa patented.

Kwenye Kiti Moto mimi nilikuwa ni preseter tuu, kipindi sio changu ni cha Masai Studio, jina la Kiti Moto sijui ni nani alilibuni ila mmoja wa wamiliki wa Masai Studio, Allyoki yupo humu.

P
 
Mtindo mpya wa kujikot mwenyewe,hausumbuki hii kitaaluma imekaaje?
Kuna aina mbili za uandishi,
1. Plain writings ni kuandika tuu maandishi kama kupiga story
2. Kuandika literally work, unaandika maandishi yenye footnotes na references.

Hivyo baadhi ya nyuzi zangu ni literacy works, uzuri wangu hayana copyright, hivyo hata mtu akitumia hakuna kosa.

Hii ya kuandika na kuji quote ni ili kukujulisha jambo hilo niliisha liandikia.

P
 
Back
Top Bottom