Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Sasa kumebuka watu
Watafuta habari za kuumua

Lakini hunahaja ya kusumbuana nao
Kwakuwa umejitambua
Kutoka ktk kundi la MAROFA NA WAPUMBAVU
Wapotezee
 
View attachment 330218

Ndugu zangu. Wengi wenu mmekwisha pata taarifa kuhusu kurejea kwangu lCCM..Tamko langu la kurejea CCM nililitoa katika ofisi ya CCM ya Kata Mikocheni saa 10.40 jioni. Ni nililitoa kwa kuongea bila kuisoma na kusambaza printed speech yenyewe. La kushangaza ni kwamba kuna wahuni waliamua na kunitia Jamii Forum wakachapisha eti tamko langu. Tamko lenyewe limeandikwa hovyo. Kiswahili kibovu na hata uandishi wenyewe hauna ufanisi wowote . Ni kukosa heshima kwa mtu mwandishi mzuri kama mimi ambaye hata Chuo Kikuu cha DSM kimetunukia degree ya udaktari wa fasihi. Juu ya hivyo hadithi ndefu iliyotolewa ni kejeri na matusi kuhusu utu na uadilifu wangu. Ningesema hawa wahusika ni watu washenzi wakudharauliwa na kupuuzwa. Lakini lazima tugeuze matumizi ya mitandao ya jamii kama tutajenga jamii ya kiutu na kiungwana. Hatua za kisheria hazina budi kuchukuliwa dhidi ya wahalifu hawa.
Ndugu zangu,
Tamko langu rasmili llitatoka kesho kwenye magazeti. Na pia nitalichapisha katika ukurasa huu. Tuendelee kuwa pamoja.

Source:Balozi Mwapachu FB Account
Mbona Kiswahili hiki ni dhaifu kuliko cha kwenye tamko feki?
 
TAFADHALI MWAPACHU!

Yaani, mnawafundisha hawa vijana vitu gani nyinyi? Mnataka Taifa liwakumbuke kwa yepi hasa? Majina yenu tu? Mnataka tutakapoandika historia tuseme na wao walikuwepo? Binafsi sina tatizo kabisa na wewe kurudi CCM au kuachana na CCM kabisa au kujiunga na chama kingine chochote kwani hilo ni suala la hiari ya mtu. Sikusema lolote ulipoondoka kwani sikuwa shahidi ulipoingia ilikuwaje. Kujiunga na chama cha siasa ni hiari ya mtu na ni sehemu ya demokrasia ndio maana sijali sana watu kutoka au kujiunga na chama chochote.

Kitu ambacho kimenitibua sana ni maelezo ya kwanini umeamua kurejea! Maelezo yako yanaonesha kitu kimoja cha hatari kabisa; wewe si mtu wa kanuni na mwenye kusimamia unachosimamia. Maelezo yako yanaonesha pia kuwa wewe si mtu wa tafakari makini na mwenye kupima matokeo ya maamuzi yako mbalimbali. Umejionesha tu ni mtu wa kuongozwa na hisia na kufuata upepo; ni kama kijana mdogo ambaye anahitai kuendelea kufunzwa. Hili naona ni la kuudhi na kutisha zaidi.

Sababu ulizotoa za kwanini unataka kurudi zinachanganya na zinakesha kama vile sababu zako z akuondoka zilivyokuwa. Ama uliamini kuwa ni kweli uliyoyasema wakati uleau unaamini ni kweli unayoyasema sasa. Uliondoka kumfuata Lowassa – siyo CHADEMA wala misiamo ambayo alikuwa anaenda kuisimamia na leo umemkimbia kama hukuwa unamjua. Yaani, kama ni matafiki umejionesha kuwa si rafiki wa kuaminiwa.

Kwa mtu mwenye umri na uzoefu kama wa kwako, neno lako linatakiwa kuaminiwa. Linataka kuonekana limefikiriwa vizuri na linatakiwa lioneshe aina ya mtu aliyelitoa. Binafsi, sipendi kuzungumzia mtu kabisa na leo umenifanya nimjadili mtu kwa sababu mfano ulioutengeneza ni wa hatari, unapotosha na unakwaza vijana labda n ahata watu wazima wengine ambao waliamini ulichosema wakati ule! Leo umegeuka tena umegeuka kama hujawahi kugeuka!

Unasema baada ya muda huu wa wewe kuwa nje ya CCM baadaye umeamua kurudi kwa sababu kadhaa: Kwamba miongoni mwa sababu hizo ni:

1. Kulewa mahaba ya Lowassa – hii ni kejeli; ni kejeli kwa watu wote wenye akili timamu hasa kwa mtu wa haiba na uwezo wako.

2. Kulewa ahadi ya Uwaziri – kwamba, ulikimbilia kwa Lowassa kwa sababu uliamini angeshina na wewe ungekuwa miongoni mwa wanaoapishwa! Yawezekana hii ni sababu kubwa zaidi yaw ewe kwenda kule kuliko ya mahaba ya uzeeni.

3. Kuamini mafuriko ya Lowassa – hili nalo la ajabu; yaani ulikuwa unafuata picha na video kwa kuangalia umati na kuamini tu kuwa umati peke yake ni kushinda. Kwani picha na video zinapiga kura?

4. Kukubaliana na wenzako kuondoka lakini wengine wakakausha dakika za mwisho na hivi sasa “wana vyeo”. Inaonekana hili la kukosa vyeo au kutaka vyeo linakugusa sana; hukupata cheo kwa vile Lowassa hakushinda na unaona wenzako waliobaki wamepata vyeo na wewe umekosa yote. Wanasema “mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote”.

Lakini katika maelezo yako yale rasmi ambayo yanasambaa mitandaoni inaonekana siri kubwa yaw ewe kurudi na inawezekana ikawa ni sababu yaw engine kurudi vile vile CCM ni hii:

“Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.”

Kauli hii inatukumbusha pia kauli ambayo ilitolewa na Lowassa miezi michache nyuma kuwa maswahiba wake au watu waliokuwa wanamuunga mkono wananyanyaswa na kubanwa na serikali hasa kwenye masuala ya kodi. Alilisema hili baada ya serikali ya Magufuli kuanza kuwabana wakwepa kodi. Sasa tukijumlisha alilolisema na unalolisema inaonekana ushirika wenu ulikuwa na sababu nyingine kabisa ya kutaka kuwa watawala wetu; na tunashukuru sisi wengine kwamba Watanzania waliwakataa na hawana majuto kwani leo umewapa sababu ya kuamini kuwa mabadiliko feki yale yalikataliwa kwa uhalali kabisa na sasa umekumbatia mabadiliko ya kweli.

Hata sasa swali kubwa linalobakia ni kuwa je tunaweza kukuamini; je tunaweza kuamini kuwa unasema kweli sasa? Je umejionesha kuwa unaweza kuaminika; mtu yeyote anayekuita rafiki anaweza kukuamini sasa na akaingia mapatano nawe?

Binafsi naamini – na inaonekana mwenyewe umegundua hilo – umeonesha mfano mbaya kama kiongozi mkongwa; umeonesha ukosefu mkubwa wa hekima na zaidi umeonesha udhaifu mkubwa wa kusimamia mambo uliyoyaamini. Sidhani kama hadi hivi sasa kuna lolote ambalo CCM kama chama imelifanya ambalo lingekubadili mawazo; na umesema kweli kuwa sasa umerudi kumfuata mtu kama ulivyoondoka kumfuata mtu; hii ni aina mbaya kabisa ya uongozi tunayotaka kujenga nchini.

Watu wasio na kanuni na maadili ya kuaminika wanaweza vipi kusimama na kujionesha kuwa wanaweza kuaminiwa na kuwa wana kanuni? Binafsi naamini badala ya kujaribu kuzengea nafasi fulani mahali fulani wakati huu ungeamua kujiendeleza na mambo yako na kuachana na siasa ili angalau uonekane umeaminika. Ni matumaini yangu Magufuli hatowazawadia watu wa aina yako kwani taifa letu linahitaji viongozi bora na siyo bora viongozi; tunahitaji watu ambao watasimama kama mifano kwa vijana na vizazi vijavyo badala ya kuja kutajwa kama viongozi waliowahi kuwepo kuwepo na siyo walikuwepo viongozi viongozi!

Kusamehewa najua wengi tutakusamehe; lakini hatuwezi kukuamini hadi ujioneshe unaweza kuaminika kweli. Kwa hayo uliyoyaseme leo kuwa yaliyopita si ‘ndwele’ tugange yajayo; mmh! Tafadhali Balozi Mwapachu!

MMM
Kwa ufupi huyo mtu ni.....OPPORTUNIST.
 
Hiikaandika Mwapachu kweli?

Atunukiwe degree ya fasihi halafu aandike "kejeri" badala ya "kejeli"?

Au na hii ni fake ya fake?
 
Hapana mkuu nnapingana na wewe, ameidhalilisha sana CCM kwa kuonesha aina ya wanachama iliyo nayo nikimaanisha wanachama MASLAHI mbele..

Wapo radhi hata kuuza nchi hii kwa sababu ya matumbo yao, imagine mtu kama huyu akiahidiwa pesa nyingi ili kutoa siri za kiusalama ci mapema tu anachukua chake!!?
Hata nanyi mnajidhalilisha watu wanapokuja kwenu ndo kwanza wanapewa Na nafasi muhimu ndani ya chama hadi kugombea urais hivi mnakua hakuna kabisa mnaowaamini walizaliwa Na kulelewa uko imagine lowasa anaamua kurudi nae.
 
Swali la Dr Slaa linakaribia kupata jibu.
Je, Lowasa ni asset au liability? CDM/UKAWA laana ya Dr Slaa itazidi kuwatafuna,mkaombe msamaha kiutu uzima. CDM ni kiwiliwili tu kinaruka ruka,kichwa kiko Canada
 
Waswahili wanasema "Ukitaka kuruka agana na Nyonga". Mzee alikurupuka sana bila ya kujua Mwenzie Kingunge aliondoka baada ya Mkwere kumnyang'anya Miradi yote kuanzia Ubungo bus terminal na Parking hakuwa na cha kupoteza. sasa yeye kakurupushwa na Maigizo ya kufagia barabara. Aliwaiga kina Rostam na Minywele wenzie wana reserve kama Petrol reserve ya America.
 
Mzee kashikwa pabaya. Sijui wamembana wapi wazee wa visasi?
 
kuondoka kwake ccm kulituathiri sana mpaka tukapoteza Ubunge, bado tunam-mind sana.
salama yake amshauri JPM amtunuku u-DC Mgombea wetu wa Ubunge aliyegalagazwa. au ndio kusema, "kazi mliyonituma nimeimaliza!?".
 
Amejing'aata hadi sijamuelewa! lakini hatosumbuliwa tena karudi kwenye kundi la walanguzi
 
TAFADHALI MWAPACHU!

Yaani, mnawafundisha hawa vijana vitu gani nyinyi? Mnataka Taifa liwakumbuke kwa yepi hasa? Majina yenu tu? Mnataka tutakapoandika historia tuseme na wao walikuwepo? Binafsi sina tatizo kabisa na wewe kurudi CCM au kuachana na CCM kabisa au kujiunga na chama kingine chochote kwani hilo ni suala la hiari ya mtu. Sikusema lolote ulipoondoka kwani sikuwa shahidi ulipoingia ilikuwaje. Kujiunga na chama cha siasa ni hiari ya mtu na ni sehemu ya demokrasia ndio maana sijali sana watu kutoka au kujiunga na chama chochote.

Kitu ambacho kimenitibua sana ni maelezo ya kwanini umeamua kurejea! Maelezo yako yanaonesha kitu kimoja cha hatari kabisa; wewe si mtu wa kanuni na mwenye kusimamia unachosimamia. Maelezo yako yanaonesha pia kuwa wewe si mtu wa tafakari makini na mwenye kupima matokeo ya maamuzi yako mbalimbali. Umejionesha tu ni mtu wa kuongozwa na hisia na kufuata upepo; ni kama kijana mdogo ambaye anahitai kuendelea kufunzwa. Hili naona ni la kuudhi na kutisha zaidi.

Sababu ulizotoa za kwanini unataka kurudi zinachanganya na zinakesha kama vile sababu zako z akuondoka zilivyokuwa. Ama uliamini kuwa ni kweli uliyoyasema wakati uleau unaamini ni kweli unayoyasema sasa. Uliondoka kumfuata Lowassa – siyo CHADEMA wala misiamo ambayo alikuwa anaenda kuisimamia na leo umemkimbia kama hukuwa unamjua. Yaani, kama ni matafiki umejionesha kuwa si rafiki wa kuaminiwa.

Kwa mtu mwenye umri na uzoefu kama wa kwako, neno lako linatakiwa kuaminiwa. Linataka kuonekana limefikiriwa vizuri na linatakiwa lioneshe aina ya mtu aliyelitoa. Binafsi, sipendi kuzungumzia mtu kabisa na leo umenifanya nimjadili mtu kwa sababu mfano ulioutengeneza ni wa hatari, unapotosha na unakwaza vijana labda n ahata watu wazima wengine ambao waliamini ulichosema wakati ule! Leo umegeuka tena umegeuka kama hujawahi kugeuka!

Unasema baada ya muda huu wa wewe kuwa nje ya CCM baadaye umeamua kurudi kwa sababu kadhaa: Kwamba miongoni mwa sababu hizo ni:

1. Kulewa mahaba ya Lowassa – hii ni kejeli; ni kejeli kwa watu wote wenye akili timamu hasa kwa mtu wa haiba na uwezo wako.

2. Kulewa ahadi ya Uwaziri – kwamba, ulikimbilia kwa Lowassa kwa sababu uliamini angeshina na wewe ungekuwa miongoni mwa wanaoapishwa! Yawezekana hii ni sababu kubwa zaidi yaw ewe kwenda kule kuliko ya mahaba ya uzeeni.

3. Kuamini mafuriko ya Lowassa – hili nalo la ajabu; yaani ulikuwa unafuata picha na video kwa kuangalia umati na kuamini tu kuwa umati peke yake ni kushinda. Kwani picha na video zinapiga kura?

4. Kukubaliana na wenzako kuondoka lakini wengine wakakausha dakika za mwisho na hivi sasa “wana vyeo”. Inaonekana hili la kukosa vyeo au kutaka vyeo linakugusa sana; hukupata cheo kwa vile Lowassa hakushinda na unaona wenzako waliobaki wamepata vyeo na wewe umekosa yote. Wanasema “mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote”.

Lakini katika maelezo yako yale rasmi ambayo yanasambaa mitandaoni inaonekana siri kubwa yaw ewe kurudi na inawezekana ikawa ni sababu yaw engine kurudi vile vile CCM ni hii:

“Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.”

Kauli hii inatukumbusha pia kauli ambayo ilitolewa na Lowassa miezi michache nyuma kuwa maswahiba wake au watu waliokuwa wanamuunga mkono wananyanyaswa na kubanwa na serikali hasa kwenye masuala ya kodi. Alilisema hili baada ya serikali ya Magufuli kuanza kuwabana wakwepa kodi. Sasa tukijumlisha alilolisema na unalolisema inaonekana ushirika wenu ulikuwa na sababu nyingine kabisa ya kutaka kuwa watawala wetu; na tunashukuru sisi wengine kwamba Watanzania waliwakataa na hawana majuto kwani leo umewapa sababu ya kuamini kuwa mabadiliko feki yale yalikataliwa kwa uhalali kabisa na sasa umekumbatia mabadiliko ya kweli.

Hata sasa swali kubwa linalobakia ni kuwa je tunaweza kukuamini; je tunaweza kuamini kuwa unasema kweli sasa? Je umejionesha kuwa unaweza kuaminika; mtu yeyote anayekuita rafiki anaweza kukuamini sasa na akaingia mapatano nawe?

Binafsi naamini – na inaonekana mwenyewe umegundua hilo – umeonesha mfano mbaya kama kiongozi mkongwa; umeonesha ukosefu mkubwa wa hekima na zaidi umeonesha udhaifu mkubwa wa kusimamia mambo uliyoyaamini. Sidhani kama hadi hivi sasa kuna lolote ambalo CCM kama chama imelifanya ambalo lingekubadili mawazo; na umesema kweli kuwa sasa umerudi kumfuata mtu kama ulivyoondoka kumfuata mtu; hii ni aina mbaya kabisa ya uongozi tunayotaka kujenga nchini.

Watu wasio na kanuni na maadili ya kuaminika wanaweza vipi kusimama na kujionesha kuwa wanaweza kuaminiwa na kuwa wana kanuni? Binafsi naamini badala ya kujaribu kuzengea nafasi fulani mahali fulani wakati huu ungeamua kujiendeleza na mambo yako na kuachana na siasa ili angalau uonekane umeaminika. Ni matumaini yangu Magufuli hatowazawadia watu wa aina yako kwani taifa letu linahitaji viongozi bora na siyo bora viongozi; tunahitaji watu ambao watasimama kama mifano kwa vijana na vizazi vijavyo badala ya kuja kutajwa kama viongozi waliowahi kuwepo kuwepo na siyo walikuwepo viongozi viongozi!

Kusamehewa najua wengi tutakusamehe; lakini hatuwezi kukuamini hadi ujioneshe unaweza kuaminika kweli. Kwa hayo uliyoyaseme leo kuwa yaliyopita si ‘ndwele’ tugange yajayo; mmh! Tafadhali Balozi Mwapachu!

MMM
Mbona nimeisikiliza speech ya mwapachu ila hajaongea haya uliyoyaandika hapa?
Umeyatoa wapi MM?
Mushumbusi hajambo na dr S?wasalimie
 
Wewe [emoji86] Ungefunika tu hilo kalio lako na ucongee lolote kuhusu cdm. Hujui siasa inaendeshwaje maana kama cdm icingefanya iliyofanya sahivi isingekuwa hapo ilipo. Fanya tathmini kama ubongo wako uko sawa uchguzi uliopita kilikuwa na wabunge wangapi halmashauri ngapi na sasa inatarajia kukamata jiji la dar baada miji mikubwa kusombwa pia na cdm. Haya ni mafanikio makubwa ndani ya chama cdm. So! usiwe kama ngucheerro [emoji86]

Kwa taarifa yako cdm hata lisingekuja hilo kundi la wahuni bado ingepata zaidi. Hiki unachokisema wewe labda kwa watu wasiojua siasa wala kuijua cdm. Huyo EL alikatwa na ccm kwa hofu ya kuogopa nguvu ya cdm, idadi ya watu kujiandikisha kwa hasira uchaguzi huu ilijitokeza kwa sababu ya kutaka kuing'oa ccm, na walio wengi walijua EL ndio atachaguliwa na ccm. Sisi cdm ndio tukaona tumepata hilo kapi toka ccm kumbe tumepatikana. Nani kakudaganya cdm imependwa baada ya kuja EL? Mimi binafsi nimempa EL kura yangu sio kwa kumkubali bali ni ile tofauti yangu ya kudumu dhidi ya ccm lakini nilikuwa najua hafai. Na kwakuwa najua elimu ya uraia wangalau niliona ni bora nimpe EL ili kupunguza wingi wa wabunge wa ccm bungeni. Wewe baki kudanganya watu hapa na kutoa matusi ya kishamba ili uonekane mjanja kumbe ni boya tu. Na ukitaka matusi hebu niPM nikuchomekee disk mbovu ndio utajuta kujichanganya na mimi K...ma mama..ko. Watu tumepigwa mpaka mabomu huyo EL akiona sawa tu tulichokuwa tunafanyiwa wapinzani, leo unataka kutuambia usengerema gani we kenge. Chama ni watu sio mtu kama unavyotaka tumuamini huyo EL.
 
Mzee Mwanakijiji fell for the bluff , went ahead and submitted a scathing commentary on Balozi. Mwanakijiji owes Mwapachu an apology .
 
Nimesoma bandiko lako kwa makini nimegundua kuna maneno kama unajitukana na wewe hivi ......anyway Watanzania wengi misimamo ni zero kabisa..
 
...“Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.”
Maana yake mzee ameona kwamba wenzake waliobaki huko CCM shughuli zao hazikwamishwi
 
Back
Top Bottom