BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Wanasema tu hivyo sasa ila sense ikija wata shirk tu. Ila mm Nina swali mmoja. Nini mantiki ya kuingiza kipengele cha dini kwenye sensa? Inawezekana kasema ila kwenye maelezo hapo juu sijaona ikisemwa nini sababu la pendekezo hilo.
 
Nchi (Serikali) ya Tanzania haiendeshwi kwa misingi ya kidini, lakini inatoa uhuru kwa kila raia wake kuabudu kupitia misingi ya dini anayoitaka. Hii sensa inafanya na serikali (ambayo haina dini) sasa hizo dodoso za kidini zinaumuhimu gani kwa serikali isiyoendeshwa kwa misingi ya kidini? Kama tumeshapewa uhuru wa kuabudu
kupitia dini zetu, kwa nini tusitumie uhuru huu katika kujua idadi zetu kupitia madhehebu tunayo abudia? Ugumu unakujaje hapo? Kwa nini tusijifunze kufanya maamuzi kwa njia za kistaarabu? Tukiambiwa asilimia kubwa ya sisi waislamu tuna tatizo la kutotumia shule katika kufanya maamuzi tutakataa kwa kutumia hoja gani hapa..?

Mkuu, ngoja nikupe ushauri wa bure. Usipoteze nguvu zako kubishana na huyo, akili zake zina mismis. Shauri yako!
 
Sheikh Ponda anaudhalilisha uislam na kuwadhililisha waislam wenyewe. Na cha ajabu wasomi wa kiislam wanamwacha huyu semi-illiterate 'ahodhi' dini yao!
 
Serikali dhaifu kila eneo watu wanalalamika 2, kwani kikiingizwa hicho kipengele cha dini kunatatizo gani
 
An empty head is devil's workshop.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wana JF.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetangaza rasmi mgogoro na Serikali baada ya kueleza kuwa haitashiriki Sensa ya Watu na Makazi kutokana na muhimili huo wa Dola kukataa kuingiza kipengele cha dini kwenye dodoso la Sensa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda alisema, Jumuiya za Kiislamu ziliwasilisha serikalini mapendekezo matatu kabla ya Waislamu kushiriki zoezi hilo.

Mapendekezo hayo kushauriana na wawakilishi wa dini iunde tume huru ya Sensa na kuitangaza kabla ya Agosti 20 mwaka huu iwe na wawakilishi wa dini za Waislamu, Wakiristo, na madhehebu mengine katika hatua za mchakato wa Sensa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira alikataa mapendekezo hayo, Sheikh Ponda alisema kuanzia sasa wataendelea kuzitaarifu balozi zote zilizopo nchini, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Nchi wafadhili na mamlaka zingine kwamba kitachofanywa Tanzania ni utafiti na wala siyo Sensa kwa kuwa zaidi ya nusu ya raia wake hawajahesabiwa.

Waislamu tumepanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga dhulma dhidi ya Waislamu.

CHANZO: MWANANCHI JUNI 22 2012

Huyo kwenye Red: Mara nyingi sina imani na huyo Uamsho.
Anachojua yeye ni kuhamasisha vurugu tu.
 
Hivi waislamu ni muhimu sana kila kitu wanachopendekeza kiwe hivyo?amesema walipeleka mapendekezo, sasa ni lazima iwe hivyo ulivyopendekeza. Huu ni upuuzi na waache kushiriki, na wataendelea kulalamika tunazurumiwa mpaka mwisho wa hii dunia, waislamu wa nchi hii watakuwa nyuma kwa sababu ya ujuha wa viongozi wao.
ipo siku mambo yatabadilika na si mbali sana
 
Pamoja na kwamba mimi ni Muislamu,elimu dunia imenisaidia kujua uhalisia wa mambo..Nawashauri viongozi wangu waandaa Sensa ya taifa kama nia yao ni kujua idadi yetu..Waandae dodoso linalolenga kujua taarifa zetu kidini..Tutachangia gharama ktk hilo,LAKINI SENSA YA TAIFA LAZIMA NISHIRIKI..,NINALIPENDA TAIFA NA NATAKA LIENDE MBELE...ALLAH HAJATUAMURU TUPINGE MAENDELEO JAMANI..
 
Swali hili lijibiwe na wanaoifahamu Qurani si maamuma,Kwani tunahitaji surat na aya za Kurani tukufu.Maana Mufti amewataadhalisha wafuasi wa dini kukiona cha moto kwa Allah kwa wale watakaokubali kuhesabiwa bila kuulizwa Kama ni wafuasi wa dini ya Islam. Inawezekana wameamriwa na mola wao kugomea sensa za makafiri na mapagani.Tupe aya
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

“Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

“Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

CHANZO: HabariLeo
Mi nadhani misikiti ipo na waumini wao wapo so wanaweza kupiga sensa humo ndani wakajijua ni wangapi
 
Mimi siyo muislam lakini kwa kifupi wenyewe huwa wanasema Uislam ni Mfumo Kamili wa Maisha...kwa hiyo kila kitu kuanzia siasa,sensa nk vimo ndani yake...subiri wenyewe waje wakufafanulie vizuri...
 
"mungu" wa waislam hataki mchezo kabisa lazima kila kitu kiende kwa mfumo wa allah subhana wataala.Tutagomea sensa ,hesabuni hao wagalati.takbirr.
 
Pamoja na kwamba mimi ni Muislamu,elimu dunia imenisaidia kujua uhalisia wa mambo..Nawashauri viongozi wangu waandaa Sensa ya taifa kama nia yao ni kujua idadi yetu..Waandae dodoso linalolenga kujua taarifa zetu kidini..Tutachangia gharama ktk hilo,LAKINI SENSA YA TAIFA LAZIMA NISHIRIKI..,NINALIPENDA TAIFA NA NATAKA LIENDE MBELE...ALLAH HAJATUAMURU TUPINGE MAENDELEO JAMANI..
Uwe unasoma posts kabla ya kuchangia, hili lilishajibiwa hapa na M-joka:

"Mimi nilisema Wakristo wanaruhusiwa kuendesha na kuweka takwimu za idadi ya waumini wao, hata waislamu vile vile wanaruhusiwa, ikiwemo kanisalakini nani wa kumuamini?,

Nani asiyejipendelea? Ndio maana inakuja kwamba ni serikali, utawala ndio uwe na mamlaka katika jambo hili KITAIFA, KITAIFA ndugu yangu, na sio taasisi za kibinafsi
...SASA KWANINI (SERIKALI) WAKWEPE WAJIBU WAO NA KUKIKWEPA KIPENGELE HICHO CHA DINI???? Sijui Mkuu unafahamu sijui.
 
Maswala ya udini hayana maana yeyote kwenye sensa ni ubinafsi wetu tu serkal inataka kujua idadi ya watu pekee kama tunaitaji kujua idadi yetu mufti mkuu awasiliane na masheh nchi nzima ili mtuhesabu ila sijui kama ina maana yoyte zaidi ya ubaguz tusaidiane kiuchumi sio kufanya mambo yasiyo na msingi kwa kwel waislam wenzangu hilo siliungi mkono hata kidogo na mimi siwezi kugomea sensa sababu najua maana yake.mtafanya mpaka dini nyingine watucheke na kutuona wajinga tunajishusha hadhi wenyewe
 
Tafsiri ya neno ibada, hutafsiriwa kuwa ni kila kinachomridhisha Mwenyezi Mungu..........ukiielewa hii tafsiri basi aya utakazopewa zitakuwa ni nyingi tu Mkuu.
Je, unakubaliana na mimi kuhusu hiyo tafsiri ili niendelee, au tusimame hapa kwenye tafsiri kwanza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom