STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,772
- 555
Wana JF.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetangaza rasmi mgogoro na Serikali baada ya kueleza kuwa haitashiriki Sensa ya Watu na Makazi kutokana na muhimili huo wa Dola kukataa kuingiza kipengele cha dini kwenye dodoso la Sensa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda alisema, Jumuiya za Kiislamu ziliwasilisha serikalini mapendekezo matatu kabla ya Waislamu kushiriki zoezi hilo.
Mapendekezo hayo kushauriana na wawakilishi wa dini iunde tume huru ya Sensa na kuitangaza kabla ya Agosti 20 mwaka huu iwe na wawakilishi wa dini za Waislamu, Wakiristo, na madhehebu mengine katika hatua za mchakato wa Sensa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira alikataa mapendekezo hayo, Sheikh Ponda alisema kuanzia sasa wataendelea kuzitaarifu balozi zote zilizopo nchini, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Nchi wafadhili na mamlaka zingine kwamba kitachofanywa Tanzania ni utafiti na wala siyo Sensa kwa kuwa zaidi ya nusu ya raia wake hawajahesabiwa.
Waislamu tumepanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga dhulma dhidi ya Waislamu.
CHANZO: MWANANCHI JUNI 22 2012
Ni jumuia hazishiriki au waislamu?, Mbona tuko nao mtaani na wanasema watashiriki?