Bakhresa group punguzeni udini

Bakhresa group punguzeni udini

Status
Not open for further replies.
Jambo baya halihalalishwi na jambo baya jingine
Ni kweli kabisa mkuu,lakini mbona kumekuwa na dharau sana ?,watu wamepiga na wanapiga kelele sana lakini kama ni kumpigia mbuzi gitaa,au labda mpaka yatokee machafuko ndo watu wakumbuke kwamba kuna kelele zilikuwa zinapigwa ?
 
Ni kweli kabisa mkuu,lakini mbona kumekuwa na dharau sana ?,watu wamepiga na wanapiga kelele sana lakini kama ni kumpigia mbuzi gitaa,au labda mpaka yatokee machafuko ndo watu wakumbuke kwamba kuna kelele zilikuwa zinapigwa ?
Mimi mkuu sipendagi kabisa mtu kupewa kazi kwa sababu ya kabila, dini, kanda ama kwa vigezo vya itikadi yoyote ile, mtu apewe kazi kwa vigezo na sifa zinazokubalika na siyo upendeleo ambao mwisho wa siku ni kuleta utengano ktk jamii, jambo ambalo halina afya hata kidogo kwenye umoja wa kitaifa
 
Wakati mwingine muwe mnakaa kimya kama mnaona kabisa mawazo yenu si ya kujenga, kwanini mkubali kuwa mbolea ya kukuza utengano? kwanini ukubali kuwa mfia dini, kwanini ukubali kuwa mfia chama na kwanini ukubali kutoambilika juu ya mtu fulani? kuna ubaya gani au ugumu gani ukachagua kuruhusu akili yako ikafanya kazi na kusimamia ukweli na haki, madikteta huwa wanaingizwa madarakani na watu kama nyie wafia dini, chama na kutoambilika juu ya mtu fulani..Ndugu yangu duniani umekuja peke yako na utaondoka peke yako, kama huwezi kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi ni bora pia usiiharibu, usishiriki kufifisha tabasamu katika nyuso za watu kwa ajili ya kutetea ujinga
Safi sana mkuu umemjibu vizuri na kiuungwana sana
 
Ni sawa wameachwa nyuma lakini kwanini asilimia kubwa wenye mpunga ni Waislamu?
Wenye mpunga wengi ni watu wenye asili ya Asia au Waarabu, kwa upande wa wabantu hakuna mpunga ni kama hao akina john n.k, hata ukiangalia matajiri 10 wanaoongoza Tanzania ni mmoja tu mzawa ambaye ni Reginald Mengi
 
Kama haya malalamiko ni ya kweli hatari sana lakini ukiachilia Mbali Bakhresa Sekta binafsi kuna shida ya ukabila na Udini. Uwezi ukakuta kampuni ya mchaga wamejaa wazaramo hata siku moja. Msumeno ukate Huku na Huku


Mzaramo yako ngoma ofisni anaenda kufanya nini?
 
Mimi mkuu sipendagi kabisa mtu kupewa kazi kwa sababu ya kabila, dini, kanda ama kwa vigezo vya itikadi yoyote ile, mtu apewe kazi kwa vigezo na sifa zinazokubalika na siyo upendeleo ambao mwisho wa siku ni kuleta utengano ktk jamii, jambo ambalo halina afya hata kidogo kwenye umoja wa kitaifa
Sawa mtu apewe kazi kwa sifa zinazostahili,lakini unataka kusema kwamba hawa akina juma huwa hawana sifa zinazokidhi kiasi kwamba ratio imekuwa 90:10 ? Na kwa nini pale ambapo kwenye shirika pakionekana angalau ratio 60:40 (wakristo:waislamu) basi kunakuwa na kelele kwamba pana udini ?
Sote tunapenda amani kwani kikinuka hakuna atakayekuwa salama,si muslam si mkristo,
Sote tushirikiane kuleta amani,utulivu na upendo kwenye jamii zetu yasije kutokea kama ya central africa
 
Bakhresa group au Azam kama wengi wanavyoifahamu kampuni hii, ina udini sana.

Sehemu zao zote walikowekeza ili upate kazi kipaumbele ni lazima uwe unaabudu Islamic; kwanini?

Anzia kwa madereva wa maroli na gari ndogo ili upate kazi lazima uitwe Juma, Hamia, Hamis, Abdul, Aisha na majina fanani na hayo.

Viwanda vyote vya juice, biscuits na chocolate lazima uwe na sifa hiyo.

Hii si sawa kabisa, hivi hawa akina John, Eliakim, Annastazia na wengine wengi wakiamua kususia bidhaa zako itakuwaje?

Hata Rwanda sasa wameanza kulalamikia jambo hilo. Mfagizi tu wa ofisi eti lazima awe Islamic! Na hata sasa nasikia una boti inayotoa huduma kiislamu pekee.

Tambua bidhaa zako hazinunuliwi na waislamu pekee na acheni ubaguzi.
Kweli kabisa hasa tido na Charles ndio wanasimamia huu udini
 
Nashauri na bidhaa zao wauze kwa style hiyohiyo ili wapime soko lao likoje.
 
Kuna mgahawa nimeingia leo asubuhi eti hawauzi soseji kisa wateja wao wa kiislam wanalalamika.....PSHHHHH
Na sisi je? Siendi tena kununua kitu pale.
Tatizo ukiishi na muislam atataka ubadilishe lifestyle yako iendane na mahitaji yake. BULL!
Wewe si ufate wanakouza hayo madude mradi wanafanya biashara halali usiwapangie mtaji ujawatafutia wewe pambana na hali yako.
 
Mada imezungumzia udini; wewe unazungumzia ukabila.

Ingekuwa vizuri zaidi kama ungejikita kwenye mada.
Udini na ukabila ni sawa kesi ya nyani umpelekee ngedere, ni pipa na mfuniko Tanzania uwezi ukaongelea Udini ukaacha ukabila. Au ukaongelea ukabila ukaacha Udini. Maradhi yote hayo yanalitafuna Taifa letu.
 
Umesema Azam media pale wameshindwa kuwajaza akina Bakari kutokana na wachache kuwa wajuzi wa mambo ya utangazaji au uandishi wa habari,tasnia hiyo inahitaji usomi na kujua lugha lakini kwenye udereva au kutengeneza biskuti au kukata tiketi na kuwa konda wa meli hakuhitaji sifa kama za kwenye uandishi wa habari.Kwa kifupi kuna udini sana kwenye makampuni ya mzee huyu,utadhani utajiri wake kaupata kutoka kwa Waislamu pekee-juisi tunywe wote ajira wapewe kundi fulani ,hii wapi na wapi
mna wivu tu hakuna lolote
 
Sawa mtu apewe kazi kwa sifa zinazostahili,lakini unataka kusema kwamba hawa akina juma huwa hawana sifa zinazokidhi kiasi kwamba ratio imekuwa 90:10 ? Na kwa nini pale ambapo kwenye shirika pakionekana angalau ratio 60:40 (wakristo:waislamu) basi kunakuwa na kelele kwamba pana udini ?
Sote tunapenda amani kwani kikinuka hakuna atakayekuwa salama,si muslam si mkristo,
Sote tushirikiane kuleta amani,utulivu na upendo kwenye jamii zetu yasije kutokea kama ya central africa
Mkuu popote pale panapofanyika usaili wa kazi kwa kuangalia zaidi upendeleo wa aina yoyote ni lazima tupige kelele kupinga, ila kuwa ratio sijui asilimia ngapi kwa ngapi hiyo haihalalishi moja kwa moja kuwa kuna upendeleo kwenye usaili, kikubwa hapa pawe na hoja ya kuhalalisha hayo malalamiko yenyewe na siyo hisia badala ya fact, hata huyu aliyeleta hoja hii haijawa na ukweli kwa asilimia zote kwa sababu hajaja na uthibitisho wa kile anachokisema, ila hoja yangu imekuja kama kweli hiki kitu kipo maana ni kitu kinachoigawa jamii, na jambo jingine mkuu ni kwamba unapopinga ubaguzi wakati huo huo wewe unaufanya unakosa uhalali wa kupinga kile unachodai ni ubaguzi, tupingeni ubaguzi wowote mkuu iwe serikalini ama kwenye sekta binafsi, watu wapate kazi kwa sifa na vigezo vinavyokubalika na si vinginevyo
 
Yapo mashirika kibao ya waislam ila hayana ubaguzi wa kiimani. Mimi binafsi ni mpinga ubaguzi wa aina yoyote ile. Yeye si wa kwanza kuleta ndege na hivyo si lazima kupanda zake bro. Ukiona shirika linalalamikiwa mpaka na nchi ujue kunashida hapo.
nchi gani imelalamika? majungu na wivu tu mi naona
 
Bila shaka, Kampuni/Biashara zake hivyo basi anasheria na matakwa yake binafsi ya kuongoza hizo biashara zake. sidhani kama anavunja sheria za nchi.

kuna watu hawajavunjiwa nyumba japo wamejenga ktk hifadhi za barabara kwa sababu wamempa kura kiaongozi, huu nao labda tuuite ubaguzi wa kisiasa?

nenda kwenye kampuni ndogo na za kati za watu binanfsi, wengi wanaoajiriwa ni dini moja ama kabila moja sababu tu za kibinafsi.

nenda kwenya appartments hapo mjini kati zinazomilikiwa na wahindi, mpangaji anaepewa nafasi ya kwanza ni muhindi mwenzao nyinyi wengine baadae sana tena kwa tabu sana.

TRA na CRDB zinalalamikiwa sana kwa tuhuma za uchaga sambamba na NSSF kwa uislamu kipindi cha Dau.

Nadhani hii mwenye maamuzi ktk hizo biashara ama taasisi anajisikia vyema kuweka watu wa namna yake aidha kidini ama kikabila kwa sababu binafsi tu as long as anaamini hazitoshusha utendaji ama profitability.

katika ngazi za kawaida majumbani, angalia vigezo tunavyotumia kuchagua ma housegirl, ni dini na kabila mara nyingi. Binafsi siwekin housegirl nyumbani kwangu asiekua wa dini yangu nikihofia malezi ya watoto ilhali yeye ndio muda mwingi anakua nao.
 
Ni sawa wameachwa nyuma lakini kwanini asilimia kubwa wenye mpunga ni Waislamu?
waislamu wengi wenye pesa/wafanya biashara wakubwa ni wenye asili ya Asia. hii kutokana na historia kwani wazazi wao walikuja kwetu kama wafanya biashara na biashara ikasambaa kaatika generations zilizofuata.

pia kutokana na kunyimwa haki ya kusoma elimu ya secular hasa kipindi cha ukoloni, wengi wa waislamu hawakuingia katika mfumo rasmi wa serikali wa white color jobs hivyo wakawa wafanya biashara kujikimu, na hapo kuwarithisha watoto wao biashara.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom