Baba Mtakatifu Fransisko amteua Padre Jovitus Francis Mwijage kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Bukoba

Zile ni "Amri" yaani Order

Pale hakuna Uongozi, wote mnapaswa Mtii sawa?

Lakini katika kumpata Papa kuna Demokrasia which is Good

Kwanini kuumpata Kadinali na Mapadri kusiwe na Demokrasia yaani wapigiwe kura na Wajumbe?
Kwanini kuwapata Malaika Mungu hakuweka option kwamba kura zipigwe malaika mkuu ni nani, Rafaeli aende wapi n.k si kila mahali demokrasia ni muhimu, kama haujui moja ya nguzo muhimu sana kwa wakatoliki ni "Utii". Lengo kuu la kanisa ni kuhakikisha imani za waumini zinaimarika na hatimaye wafike mbinguni, Jinsi ya kutekeleza hilo ni mipango ya Kanisa lenyewe, Wewe kama muumini unapaswa kuwa mtii na kufuata mafundisho, Period! Hauwezi kwenda shule then Headmaster anatoa options wanafunzi mpige kura kuchagua waalimu! Sio kazi yenu!. Leo tunashuhudia madhehebu ya kiprotestant kama Morovian,KKKT, n.k waumini wakitoka nje ya masuala ya kiimani na kuanza kugombania nafasi za uongozi na siasa zikitawala badala ya kujikita katika imani zao! Jambo ambalo halifai kabisa.
 
Usimfananishe Mama wa Mungu na Nyerere au fimbo ya Bungeni
Bikira Maria ndani ya kanisa katoliki anapewa heshima zote! (Si kusujudiwa au kuabudiwa) sanamu kama jinsi zilivyo Rozari, Picha za watakatifu, Sehemu na vitu mbalimbali vya watakatifu, pete, n.k (Visakramenti) vikishabarikiwa vinakuwa vitakatifu, Hivyo vinapewa heshima! Chochote kilichobarikiwa kinapewa heshima! Kama jinsi msalaba uliobarikiwa unavyopewa heshima makanisani.
 
Bora hao KKKT wana Demokrasia, na wanachaguana miongoni mwa Watanzania

Huyu Muargentina ndiye anayewateua Mapadri na Kadinali?
View attachment 2786418
Usichojua ni kuwa nyuma ya uteuzi kuna VETTING OF HIGHEST degree inafanywa na pia kuna Consultation ya hali ya juu pia ikihusisha wanakanisa wa huko kwenye jimbo na TEC. Yaani Pope anaenda kutangaza tu baada ya mchujo mkali. Ni nadra sana kupita pumba ktk mchujo huo, unapimwa kila kitu na lazima utoshe, vinginevyo jimbo linawekwa chini ya Uangalizi ama analetwa mtu toka mbali kuongoza jimbo. Wanaosema Kilaini anafanyiwa FIGISU ni kwamba alistaafu tangu Machi mwaka huu, alikuwa anashikilia tu, wakati mchujo ukiendelea. Waweza kukuta walikuwa 20 hivi ama zaidi
 
Kama hujui basi halikuhusu, jali na kuzingatia ya kwako tu, mind your own business, period!
Badala ya kujibu hoja unaanza mipasho na kusutana au ndio Mama Maria mnae mwomba awaongoze ndio anahitaji hayo!!
 
Kuna nini na haya majina ya Wahaya
Florius
Antelius
Angelius
Desiserius
Blutus
Priscus
......
Ni tamaduni tu...za kihaya zinazochanganywa na matumizi ya kilatini..
Kuna kamusi ya majina hayo imeandikwa kwa kihaya...wahaya wengi hutoa majina na maana zake humo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kama Demokrasia ni Upuuzi kwanini yeye Papa anapigiwa kura kidemokrasia

Mbona unajikanyaga?
Mchakato wa uteuzi wa askofu ni mchakato mrefu kidogo ambapo ndani yake kuna hiyo demokrasia unayosema


Sio kwamba papa anaamka tu anateua hapana kuna mchakato unafuatwa ndio maana Toka Askofu Rwoma alipostaafu ni mwaka sasa ndio ameteuliwa askofu mwingine. Hii inamaana kuna mchakato unakua unaendelea hadi kumpata Askofu mpya.


Katika mchakato huo kuna kuteua majina ya wanaofaa kushika nafasi hiyo ,then wanakuwa wanachunguzwa mienendo yao na mwisho anapatikana mteule. Kwa ivo uteuzi wa Askofu Sio uamzi wa papa tu
 
  • Baccalaureate in the theology 1997, University of Urbaniana
  • Baccalaureate in Church History 2006
  • Licentiate in Church History and Patrimony of the Church, 2006-2008, Gregorian University in Rome
  • Doctorate in Church History and Patrimony of the Church, Gregorian University in Rome 2008-2011
Hizi ni degree, diploma au certificate au za hapa na pale?
Samahani lakini.

Hongera kwa Padre Prof Jovitus Mwijage
 
Kwan majina ya kilugha hayatumiki? Sidhani kuna jamii inatumia majina yao ya asili kama wahay...mfano huyu ni Askofu Jovitus Mwijage...mwijage ni jina lake la kwanza na jovitus la pili

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mkuu ulichokieleza sio sahihi Mwijage ni jina lake la tatu/mwisho. Kwanini ni nadra kumkuta mhaya anaitwa Koku Tumgonze Rushakuzi.
 
Back
Top Bottom