Baba Mtakatifu Fransisko amteua Padre Jovitus Francis Mwijage kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Bukoba

Mrao keryo

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,611
2,169
Askofu Bukoba.jpg

Baba mtakatifu Francisco leo tarehe 19.10.2023 amemteua padre Jovitus Fransis Mwijage wa jimbo Katoliki Bukoba kuwa Askofu mpya wa jimbo hilo. Ikumbukwe Askofu wa Bukoba aliyekuwepo, Desiderius Rwoma alistaafu kwa mujibu wa sheria za Kanisa kutokana na umri.

Pia kwa sasa Jimbo Katoliki Bukoba litakuwa na maaskofu watatu, yaani Askofu mstaafu Rwoma, Askofu msaidizi na msimamizi wa kitume Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini na Askofu mteule Jovitus Mwijage. Viva Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume! Hongera Askofu mpya mteule Jovitus Mwijage!

----
Mwijage.jpeg
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Jovitus Francis Mwijage kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Mapadre Wazalendo Tanzania, UMAWATA, Mjumbe wa Baraza la Seminari kuu Tanzania na pia Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Uchumi ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS.

Askofu mteule Jovitus Francis Mwijage alizaliwa tarehe 2 Desemba 1966 Jimboni Bukoba baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 20 Julai 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza dhamana na utume wake kama Paroko-usu Parokia ya Mwemage na Mwalimu na Mlezi Seminari Ndogo ya Rubya, Jimbo Katoliki la Bukoba.

Askofu mteule Jovitus Francis Mwijage alizaliwa tarehe 2 Desemba 1966 Jimboni Bukoba baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 20 Julai 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza dhamana na utume wake kama Paroko-usu Parokia ya Mwemage, Mlezi Seminari Ndogo ya Rubya, Jimbo Katoliki la Bukoba. Mwaka 2012 alijipatia shahada ya uzamivu kwenye historia ya Kanisa toka Chuo Kikuu cha Gregorian, Roma.

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2011 alitumwa na Jimbo Katoliki la Bukoba kwa ajili ya kujiendeleza kwa masomo ya juu na hivyo kujipatia shahada ya uzamivu kwenye historia ya Kanisa kunako mwaka 2012. Kati ya mwaka 2011-2012 alikuwa ni Jaalimu wa historia ya Kanisa, Seminari kuu ya Segerea. Tangu mwaka 2012 hadi mwaka 2023 aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS, Tanzania. Na tangu mwaka 2012 hadi uteuzi wake, alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Mapadre Wazalendo Tanzania, UMAWATA na pia Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Uchumi ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS.

Chanzo: Askofu Jovitus Francis Mwijage wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Tanzania - | Vatican News

--
CV OF FR. JOVITUS MWIJAGE
  • BIODATA
  • Born: 02-12-1966, Father, Francis Ndibalema and Mother, Francisca Kokwongeza
  • Sacraments of Initiation: Baptized, 11.1.1967, 1st Communion, 2.11.1975, Confirmation 27.12.1981
  • Nationality : Tanzania
  • Occupation: Priest
  • Marital Status: Celibate (Catholic Priest)
  • Place and date of Ordination: Bukoba-Ishozi Parish, 20.07.1997

  • EDUCATION
  • Preparatory year/ Kindergarten: Nteko Substation 1975
  • Primary School: Kyelima Primary school 1976-1981, Rutabo Preparatory Seminary 1981-1982
  • Secondary School/ High School: St. Mary Rubya Junior Seminary 1983- June 1989. ( ‘A’ Level 1st Division)
  • Philosophy: Ntungamo Philosophicum Seminary 1989-1992
  • Theology: Segerea Senior Seminary 1992-1997
  • Languages, Italian- Perugia University 2005
  • Germany language Course at Geineukirchen, in Linz Diocese, obtained a Certificate June – July 2005
  • Latin language Course in 2005-2006, at Gregorian University
  • French language Course, One Year course of French at Saint Louis de Francese in Rome, One Month Course at Paris at Alliance Francese, 2008.
  • Baccalaureate in the theology 1997, University of Urbaniana
  • Baccalaureate in Church History 2006
  • Licentiate in Church History and Patrimony of the Church, 2006-2008, Gregorian University in Rome
  • Doctorate in Church History and Patrimony of the Church, Gregorian University in Rome 2008-2011
  • PASTORAL EXPERIENCE
  • Teaching for one year (Year of formation) at Rutabo Preparatory Seminary: June 1989- June 1990
  • Pastoral Year: Rubya Seminary June 1995- June 1996
  • After Ordination, appointment, Assistant Parish Priest and financial administrator of Mwemage Parish , 1997-1998.
  • Rubya Seminary: 1999-2005; Teacher of History, Kiswahili, Latin, Geography and General study.
  • Appointed as Chaplain of Rubya Training Centre for 5 Months in 1999
  • Germany: Arch-dioceses of Freiburg at the parish of Constance -St. Gehbard, one month July 2008 and one month May 2011.
  • Austria: In Millistat Parish, assistant Parish Priest in all summers from 2006 to 2011.
  • February to November 2012 - 2023, Professor of Church History at Segerea Senior Seminary.
  • From November 2012 to 2023, Director of Pontifical Mission Societies in Tanzania
  • National Executive Secretary of UMAWATA (Association of diocesan Priests) 2012 - 2023
  • National Executive Secretary of Regional Board of Seminaries, Kipalapala, Kibosho, Ntungamo and Segerea 2012 - 2023
  • member of the Finance Committee of PMS (International Secretariat) representing African Continent National Directors from 2020 - 2023
 
Msahihisho hapo juu: Askofu wa Jimbo la Bukoba mstaafu ni Desiderius Rwoma na sio Severini Niwemugizi!
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisco amewateua mapadri wawili kuwa maaskofu katika majimbo Katoliki ya Njombe na Bukoba.

Maaskofu hao wateule ni pamoja na; Padri Jovitus Mwijage kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba na Padri Eusebio Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe.

Katika taarifa iliyochapishwa na tovuti ya Vatcan inasema Papa Francis amemtua Padri Kyando kuwa Askofu wa Jimbo la Njombe ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa msimamizi wa kiroho wa jimbo hilo.

Aidha, Baraza la Maaskofo Tanzania (TEC) pia limetoa taarifa hiyo ikiwamo ya uteuzi wa padri Mwijage ambaye atahudumu katika Jimbo Katoliki la Bukoba.
 
Sasa sijui huyo Mama Maria nae anaongozwa na nani ,,,kama na yeye anaombwa amuongoze mtu mzima Jovitus!!
Hapa ndipo hata mimi huwa sielewi, Mama Maria ana nafasi gani zaidi kwenye Mamlaka tuliambiwa Mungu ndiye Mkuu, Yesu alitumwa kuja kutuokoa na alipoondoka aliacha Roho mtakatifu ndiye atusimamie, Je Maria anachukua nafasi ya nani?
 
Back
Top Bottom