MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,690
- 6,500
Mtasema kila kitu ila muda utahanua. Nyie ndio wale wahafidhina alokuwa anasema mamaKwa hali inavyoendelea nchini ni dhahiri hakuna tena upinzani. Bali kuna uungwaji mkono juhudi wa Wapinzani kwa CCM kila mmoja kwa staili yake. ACT Wazalendo wanakula pamoja na CCM kule Zanzibar na CHADEMA nao wanatafuta robo mkate wao huku Tanganyika.
Kabla CHadema hawajaanza kupetiwapetiwa, Kutomaswatomaswa na kulambishwa asali na CCM hii ya leo ya Kinana na Samia, walikuwa wakitokwa povu sana kuhusu ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar. ACT walikuwa wakijitetea kuwa eti ni takwa la kikatiba kuingia humo huku CHADEMA wakiwaita ACT Wasaliti kwa hoja ya kuwa wamewasaliti Wazanzibar kwa kushiriki kula matunda ya uchaguzi haramu.
Leo tunaona CHADEMA nao wamekinga mkono kula ruzuku ambayo hapo mwanzo walisema ni haramu kwa kuwa imetokana na uchaguzi haramu. Kiufupi wamelamba matapishi yao!.
Ukiachilia mbali hilo, CHADEMA walikuwa wakijulikana sana kuwatukana akina hayati Lyatonga Mrema , John Cheyo na Shibuda kuwa eti ni makada wa CCM kutokana na kuwa na siasa za mrengo wa kukubaliana na CCM katika mambo mengi. Leo tunamuona Mwenyekiti Mbowe naye akigeuka kuwa Cheyo na Shibuda aliyechangamka zaidi.
Mbowe leo kaibeba rasmi mikoba ya John Cheyo na ameanza kutumia arguments zilezile za John Cheyo kuwa anataka siasa za "maridhiano", ambazo kimsingi siasa za hivyo ni za kutomasanatomasana, kubembelezanabembelezana ilimradi tu kila mtu aachiwe sphere yake ya influence ili aweze kula kwa urefu wa kamba yake.
Tujiulize, Hizi sifa ambazo Mbowe anazitoa kwa Samia zina tofauti gani kwa mfano na Sifa za Cheyo au Shibuda walizokuwa wakizimwaga kwa Magufuli?
Hii inaonyesha kuwa pengine ukiwa mpinzani na ukaanza kuzeeka, unaanza kuwa na tabia za OLD MAN CCM SYNDROME. Yaani unaanza kuwa na tabia zile za kiCCM CCM. Unaanza kujisogeza kwa CCM, unaanza kuongea kama wanaCCM, na unaanza kubehave kama wanaCCM
Huu ni muda muafaka kwa wanaCHADEMA kumtafakari Mwenyekiti Mbowe kuona kuwa , Je ni kweli siasa hizi za kulala kitanda kimoja na CCM anazoanza kuzifanya zinatokana na utafiti wa kina na upeo wa kisiasa au zinatokana na
1. Mosi, Je ana makubaliano ya siri na CCM ikiwa kama sababu ya kuachiwa kwake Jela na kwa hivyo anafuata script aliyotengenezewa AU
2. Je ana masilahi bianfsi ikiwemo ya kibiashara au kurudishiwa mali zake alizoporwa na serikali ya CCM kipindi cha Mwendazake?
3. Au je ni uzee na uchovu(wa Kisiasa) kwa hiyo ndo ameamua kwenda na falsafa maarufu ya "Kama huwezi kuwashinda, basi ungana nao?".
Katika nchi yoyote ukiona UPINZANI unafanya ROMANCE na Chama Tawala, Jua kuwa hakuna upinzani hapo bali kuna genge la wapiga dili wa kisiasa