Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Kwa nini akae pembeni wakati uwanja ni mkubwa tu na msiotaka maridhiano mnaweza kuleta mabadiliko kupitia huko kwingine??
Kuteseka ni sehemu ya struggle. Kama hutaki kuteseka kaa pembeni ili walio tayari hata kufa ili kuleta mabadilikio ya kweli washike usukani. Kuliko kusaliti stuggle na kuanza kujikombakomba kwa CCM bora ukae pembeni ulee wajukuu au ule bata kadri unavyoweza
 
Kwa nini akae pembeni wakati uwanja ni mkubwa tu na msiotaka maridhiano mnaweza kuleta mabadiliko kupitia huko kwingine??
Tumeshawekeza nguvu nyingi sana kupitia CHADEMA kiasi kwamba ikianza kuwa CCM B tunakuwa tumepoteza miaka mingi sana ya nguvu tuliyoitumia kwenye chama hicho ambacho tumekisaidia kufika hapa kilipo kwa machozi, jasho na damu
 
Kuteseka ni sehemu ya struggle. Kama hutaki kuteseka kaa pembeni ili walio tayari hata kufa ili kuleta mabadilikio ya kweli washike usukani. Kuliko kusaliti stuggle na kuanza kujikombakomba kwa CCM bora ukae pembeni ulee wajukuu au ule bata kadri unavyoweza
Hili sio jibu la swali uliloulizwa na buccaneer

Na kama unajibu kijeuri badala ya kuitetea hoja yako, na wewe unaweza kujibiwa kijeuri vivyo hivyo kwa kuambiwa kwamba, ukiona CHADEMA hakukufai nenda na tafuta njia uanzishe chama chako cha siasa kama kina Zito Kabwe uone kama ni rahisi..

By the way, ni kama huelewi vile kwa sababu hakuna aliyesaliti struggle bali hizo ni hisia zako za kutaka kuendelea kuishi maisha ya juzi ukashindwa kuelewa kuwa tunaishi leo kwa kuwa, nyakati na majira hubadilika. Mazingira ya kufanya siasa pia hubadilika na vivyo hivyo mikakati na mbinu hubadilika pia..!!
 
Wapinzani sisi hatuelewi huo msimamo wa viongozi wa CDM kwa muongozo wa Mbowe. Wao viongozi waendelee na siasa za kujikomba, lakini sisi hatuna muda huo. Kama Mbowe aliweza kumpokea Lowassa na watu wakamvumilia, basi safari hii atajua hana ushawishi huo aliodhani anao. Ni muda mrefu Mbowe alishaonyesha kupoteza mwelekeo.
Wewe ni wa kufukuzwa chamani maana umekengeuka
 
Tuacheni kejeli instead tuwapongeze Samia na Mbowe kwa kuweka masilahi ya nchi yetu mbele kuliko kitu kingine chochote.

Hii nchi angeendelea kuwa hai yule HAYAWANI wa Chato ingekuwa nchi ya hovyo kuliko Yemen na Somalia
Muache aendee kuoza huko aliko
Yes. Ni kweli kabisa..

Sijui kina Missile of the Nation ni kwanini tu wanaendelea kulilia siasa za uhasama za kuviziana na kupigana risasi, kutekana, kupotezana na kuuana ziendelee..

Mimi naona mambo yanaendelea vizuri kabisa. Vyama vya upinzani vinaendelea na siasa za majukwaani vyema Kwa kuikosoa na kuisema CCM kwelikweli. Katika situation kama hii mtu anawezaje kudai upinzani umekufa? Umekufaje Kwa mfano? Kwa kuwa CCM na CHADEMA wameweza kukaa pamoja na kukubaliana kuachana na siasa za uhasama wa kuuana?

Aaah, please give me a break ndugu Missile of the Nation !!
 
Kwa hiyo unataka kutwambia kuwa siasa kama za John Cheyo, Shibuda na Lyatonga Mrema ndiyo siasa makini au vipi?
 
Kuteseka ni sehemu ya struggle. Kama hutaki kuteseka kaa pembeni ili walio tayari hata kufa ili kuleta mabadilikio ya kweli washike usukani. Kuliko kusaliti stuggle na kuanza kujikombakomba kwa CCM bora ukae pembeni ulee wajukuu au ule bata kadri unavyoweza
Kwanin wewe unataka watu wataseke kwa niaba yao huku wewe ukiwa nyuma ya keyboard kama unaona wameshindwa kazi ingia mzigoni hujakatazwa
 
Kwa hiyo unataka kutwambia kuwa siasa kama za John Cheyo, Shibuda na Lyatonga Mrema ndiyo siasa makini au vipi?
Mfano south afrika wakati mandela kafungwa watu walikua wanaandamana
Ila Tanzania wakati mbowe na chadema wanashughulikiwa wote tulikua kimya alafu leo hii ndo tunajikuta tunauchungu wa mapambano kwanin ulikuwa huwatetei wakati wanateseka tuacheni unafki

Wewe umekaa nyuma ya keyboard alafu unataka wanaume wakupiganie maisha hayako na wahatarishe maisha yao na familia zao hivyo usipende sana mterereko we ni wa kiume
 
Hili sio jibu la swali uliloulizwa na buccaneer

Na kama unajibu kijeuri badala ya kuitetea hoja yako, na wewe unaweza kujibiwa kijeuri vivyo hivyo kwa kuambiwa kwamba, ukiona CHADEMA hakukufai nenda na tafuta njia uanzishe chama chako cha siasa kama kina Zito Kabwe uone kama ni rahisi..

By the way, ni kama huelewi vile kwa sababu hakuna aliyesaliti struggle bali hizo ni hisia zako za kutaka kuendelea kuishi maisha ya juzi ukashindwa kuelewa kuwa tunaishi leo kwa kuwa, nyakati na majira hubadilika. Mazingira ya kufanya siasa pia hubadilika na vivyo hivyo mikakati na mbinu hubadilika pia..!!
Mi mbowe hata nisikie ameenda ccm siwezi mlaumu na sina deni naye
Wakati wa dhiki sisi wananchi tuliogopa kumsaidia walipambana wao kama wao leo hii unawapangia kipi cha kufanya sio sawa

Hakuna kazi ngumu kama kuwapigania watanzania sababu ni watu ambao ni hopeless
 
Watanzania tuna uelewa mdogo kuhusu masuala ya kisiasa hasahasa issue ya maridhiano. Kama ungekuwa unafahamu maridhiano ya aina yoyote yanavyofanyika usingethubutu mtoa mada kuja na hii story yako hapa. Kwanza nikuulize, Je, umefuatilia Hotuba ya Mbowe ya leo mbele ya Rais? Kama ni mtu muungwana na uliye objective, huwezi kumshuku Mbowe kwa lolote. Kwa ile Hotuba ya Mbowe ya leo mbele ya Rais, ilikuwa Hotuba nzito sana inayoonesha ni namna gani Kiongozi wa Upinzani anatakiwa kuwa. Na kama isingekuwa uvumilivu wa Rais tuliyenaye, sidhani kama Mbowe angeruhusiwa kutoa Hotuba kama ile mbele ya Rais.

Halafu kukugusia kidogo ni kuwa, inapokuja suala la maridhiano, kuna kitu kinaitwa win-win gains, yaani unaachia baadhi ya vitu na mwenzio nae anaachia baadhi. Unapokea baadhi ya vitu na mwenzio anapokea baadhi ya vitu. Hii kitaalamu pia inaitwa kutengeneza consensus kwenye mazungumzo ili kuwa na common understanding kwenye conflicting interests. Ukibakia na misimamo yako tu kwenye dialogues na opponent wako haiitwi tena collaboration/mazungumzo. Itakuwa ni kitu kingine labda tuseme kutafuta suluhu kupitia kutunishiana misuli.

Mtoa mada, unaelewa lakini nachomanisha japo kwa uchache? Masuala ya maridhiano ni mambo ya kitaalamu, yana misingi yake. Sema sisi Wabongo tunapenda kusema chochote hata kama huna ufahamu mzuri wa jambo husika, ila bado unataka tu kuonekana unafahamu sana. Tujenge utamaduni wa kujifunza mambo endapo hatufahamu vizuri jambo.
 
Back
Top Bottom