Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Kwa hali inavyoendelea nchini ni dhahiri hakuna tena upinzani. Bali kuna uungwaji mkono juhudi wa Wapinzani kwa CCM kila mmoja kwa staili yake. ACT Wazalendo wanakula pamoja na CCM kule Zanzibar na CHADEMA nao wanatafuta robo mkate wao huku Tanganyika.

Kabla CHadema hawajaanza kupetiwapetiwa, Kutomaswatomaswa na kulambishwa asali na CCM hii ya leo ya Kinana na Samia, walikuwa wakitokwa povu sana kuhusu ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar. ACT walikuwa wakijitetea kuwa eti ni takwa la kikatiba kuingia humo huku CHADEMA wakiwaita ACT Wasaliti kwa hoja ya kuwa wamewasaliti Wazanzibar kwa kushiriki kula matunda ya uchaguzi haramu.

Leo tunaona CHADEMA nao wamekinga mkono kula ruzuku ambayo hapo mwanzo walisema ni haramu kwa kuwa imetokana na uchaguzi haramu. Kiufupi wamelamba matapishi yao!.

Ukiachilia mbali hilo, CHADEMA walikuwa wakijulikana sana kuwatukana akina hayati Lyatonga Mrema , John Cheyo na Shibuda kuwa eti ni makada wa CCM kutokana na kuwa na siasa za mrengo wa kukubaliana na CCM katika mambo mengi. Leo tunamuona Mwenyekiti Mbowe naye akigeuka kuwa Cheyo na Shibuda aliyechangamka zaidi.

Mbowe leo kaibeba rasmi mikoba ya John Cheyo na ameanza kutumia arguments zilezile za John Cheyo kuwa anataka siasa za "maridhiano", ambazo kimsingi siasa za hivyo ni za kutomasanatomasana, kubembelezanabembelezana ilimradi tu kila mtu aachiwe sphere yake ya influence ili aweze kula kwa urefu wa kamba yake.

Tujiulize, Hizi sifa ambazo Mbowe anazitoa kwa Samia zina tofauti gani kwa mfano na Sifa za Cheyo au Shibuda walizokuwa wakizimwaga kwa Magufuli?

Hii inaonyesha kuwa pengine ukiwa mpinzani na ukaanza kuzeeka, unaanza kuwa na tabia za OLD MAN CCM SYNDROME. Yaani unaanza kuwa na tabia zile za kiCCM CCM. Unaanza kujisogeza kwa CCM, unaanza kuongea kama wanaCCM, na unaanza kubehave kama wanaCCM

Huu ni muda muafaka kwa wanaCHADEMA kumtafakari Mwenyekiti Mbowe kuona kuwa , Je ni kweli siasa hizi za kulala kitanda kimoja na CCM anazoanza kuzifanya zinatokana na utafiti wa kina na upeo wa kisiasa au zinatokana na

1. Mosi, Je ana makubaliano ya siri na CCM ikiwa kama sababu ya kuachiwa kwake Jela na kwa hivyo anafuata script aliyotengenezewa AU

2. Je ana masilahi bianfsi ikiwemo ya kibiashara au kurudishiwa mali zake alizoporwa na serikali ya CCM kipindi cha Mwendazake?

3. Au je ni uzee na uchovu(wa Kisiasa) kwa hiyo ndo ameamua kwenda na falsafa maarufu ya "Kama huwezi kuwashinda, basi ungana nao?".

Katika nchi yoyote ukiona UPINZANI unafanya ROMANCE na Chama Tawala, Jua kuwa hakuna upinzani hapo bali kuna genge la wapiga dili wa kisiasa
Mtasema kila kitu ila muda utahanua. Nyie ndio wale wahafidhina alokuwa anasema mama
 
Acheni kupopoma.
WaTanzania hatuna shukurani wala mchango wa kusaidia kusonga mbele kazi kurudishana Nyuma tu.
Ulitaka Yale Yale ya aliyeenda yaendelee kujirudia sio.
Huu ni ujinga!
 
Asilimia kubwa ya wanaopinga siasa za kistaarabu ni wafuasi wa jiwe, wafuasi wa zito wanaoona wameachwa nyuma kwa kinachoendelea ss hv, wafuasi wa covid 19 na wahafidhina ambao wao bila siasa za ghiliba hawawezi kupata mile age.
 
Hili sio jibu la swali uliloulizwa na buccaneer

Na kama unajibu kijeuri badala ya kuitetea hoja yako, na wewe unaweza kujibiwa kijeuri vivyo hivyo kwa kuambiwa kwamba, ukiona CHADEMA hakukufai nenda na tafuta njia uanzishe chama chako cha siasa kama kina Zito Kabwe uone kama ni rahisi..

By the way, ni kama huelewi vile kwa sababu hakuna aliyesaliti struggle bali hizo ni hisia zako za kutaka kuendelea kuishi maisha ya juzi ukashindwa kuelewa kuwa tunaishi leo kwa kuwa, nyakati na majira hubadilika. Mazingira ya kufanya siasa pia hubadilika na vivyo hivyo mikakati na mbinu hubadilika pia..!!
Huyo mnafiki muache kama alivyo, ameamua kujitoa akili makusudi anapiga kelele zisizokuwa na maana.

Wakati wapinzani wakionewa, ni wao waliokuwa wakiandika humu upinzani sio uadui, leo Samia ametamka hayo maneno, wanageuka Mbowe kalambishwa asali, ni ujinga ujinga mwepesi sana.
 
Kwani imekuwaje!
20230309_044256.jpg
 
Hujajibu swali, umerukia tu kuandika insha ndefu.
Narudia swali, CHADEMA na CCM wamekubaliana nini?
Swali zuri sana hili.
Kwa CHADEMA kushiriki katika hujuma za kuyafanya siri wanayokubaliana, hicho kinakuwa kichocheo muhimu sana kwa watu wanaofikiri kuwa tayari CHADEMA hawana tofauti na akina Shibuda na Cheyo.

Hili ni takwa (sharti) muhimu aliloweka CCM, ili ukifika wakati mambo kusamabaratika, iwe tayari CHADEMA hana wigo wa kujiondoa lawamani.

Hili ni kosa namba moja alilofanya Mbowe.
 
Mi mbowe hata nisikie ameenda ccm siwezi mlaumu na sina deni naye
Wakati wa dhiki sisi wananchi tuliogopa kumsaidia walipambana wao kama wao leo hii unawapangia kipi cha kufanya sio sawa

Hakuna kazi ngumu kama kuwapigania watanzania sababu ni watu ambao ni hopeless
Watz hawastahili kupambaniwa kwa namna yoyote, ukipata nafasi ya kuwatandika basi watandike kweli kweli.
 
Nimejaribu kukusoma hadi mwisho, honestly sijaelewa kinachokufanya ulalamike nini hasa...

Na kwani kwako wewe ndugu Missile of the Nation maana yako ya "chama cha upinzani" ni nini labda kwa sbb inawezekana sisi wegine tunaelewa kwa maana tofauti na unayoielewa wewe mwenzetu?
Swali la msingi sana.Aeleze alivyotaka CDM ingefanya siasa za aina ipi?Je,wapigane ngumi?Waue watu?Wafanye ugaidi?Wapindue serikali?Watukane asubuhi ya leo hadi keshoye kwa mtiririko?Au ana chama chake mbadala akilete kifanye atakacho?
 
Sasa ndo wavae viatu vya Cheyo na Shibuda kwa kasi namna hii?.

Maana hata kina Cheyo argument yao ya kujikomba kwa CCM ni hiyohiyo mnayoita siasa za "kisataarbu"
 
Wao lazima waendelee kukosoa tu,wakusifia wapo hao MACHAWA!! Na sasa wabunge watakuwa na wakati mgumu sana kwani toka wamebaki wenyewe bungeni hakuna wanalowasemea wananchi!!wanaowasemea wananchi wapo nje ya bunge!!!
Chadema sasa hivi wanasifia na kukosoa tofauti na huko nyuma walikuwa wanakosoa tu mwanzo mwisho, hivyo sasa hivi kuna mabadiliko.
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom