Avatar ya kwanza naipenda zaidi kwani huwa kila napoiangalia inanikumbusha survey moja ya socio-economic niliyowahi kufanya ambapo nilikuwa nahoji maswali ikiwa ni pamoja na kazi wazifanyazo wanakijiji. Nilikutana na mzee mmoja kwenye kibanda chake kwanza ndio anarejea kutoka shambani (mri wake kama miaka 67-70), baada ya kumaliza utangulizi katika hojaji yangu nilimuliza:
Mimi: Sasa mzee wewe kazi yako nini?
Mzee: Sina Kazi
Mimi: Sasa wewe unajikimu vipi kimaisha kama huna kazi?
Mzee: Nahangaika na kuumia hivyo hivyo kama unavyoniona sasa ninavyorejea
Mimi: Naona una jembe, kwa maana hiyo unarejea kutoka shambani
Mzee: Ndio
Mimi: Kwa maana hiyo kazi yako ni mkulima
Mzee: Samahani kijana, kwani ukulima ni kazi?
Mimi: Ndio, kwani wewe unadhani sio kazi?
Mzee: Kwani ukifanya kosa na ukahukumiwa kwenda gerezani, shughuli utakayoikuta kule sio kilimo? Unaweza kwenda kuwa mhasibu au mwalimu
Mimi: Ndio sana sana utafanya kazi ya kulima kule. Sidhani kama unaweza kupata nafasi ya kufanya hizo kazi nyingine
Mzee: Je baada ya kutoka gerezani utapata kiinua mgongo, kama wewe unvyotegemea utakavyostaafu.
Mimi: Hapana huwezi kupata kiinua mgongo, kwani ile ni adhabu
Mzee: Je, hapa Tanzania, sisi wakulima tunapozeeka kwani tunapata kiinua mgongo au mafao ya uzeeni?
Mimi: Hapana
Mzee: Kwa maana hiyo, ukulima sio kazi ila ni ADHABU. Tofauti ni mazingira tu, lakini serikali inafurahia sana wananchi wanapokuwa wazalishaji yenyewe inauza mazao nje wala huwezi kujua thamani halisi ya mazao, na unapojichokea unaachwa kujifia mwenyewe kijijini. Lakini nyie wenzetu.
Hii sio habari ya kutunga.
Avatar ya pili:
Naiona kama ya mzee wa kifugaji kule loliondo na Hanany, ambao kwa asili wao kazi yao ni kukaa vijiweni na kunywa pombe, kwani sehemu kubwa ya uchungaji hufanywa na morani na kina mama (Wenetu hawa wanafanya kazi zao kwa rika). Kwa sasa inaonekana huyu mzee hana uhakika wa kupata maziwa na pombe yake ya kila siku kwani maeneo yao ya kuchungia mifugo yameuzwa (mfano Loliondo n.k). Hapo kama anatafakari, nini kitafuata baada ya hapa baada ya sisi kuonekana kutokuwa na thamani katika ardhi ya nchi yetu! (Hii ya pili nimeijengea mzingira wafugaji wetu wanayokabiliana nayo ambayo nayo ni halisi).
Hivyo kwangu mimi zote ni nzuri na zinamwakilisha Mtanzania nyonge asiyekuwa na haki ndani ya nchi yake. Kura yangu inaanguka kwa MZEE MWANAKIJIJI