Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Pole sana kwa matatizo, iHiyo hali ya kujisikia vibaya, kuona umeonewa, na kuona kudhulumiwa ni makosa, mnaipata wapi nyinyi ma-atheist?

Kwenye ulimwengu wa evolution na u-atheist, hakuna kitu kinaitwa dhuluma au wizi. Kuna mwenye nguvu kumyang'anya mnyonge.

Kujisikia kwako vibaya baada ya kufanyiwa hivyo kunathibitisha kuna sheria ya Mungu ya kimaadili iliyopo ndani ya moyo wako, hivyo yani.
Nenda Serengeti kajaribu kumnyang'anya watoto wake Simba jike ambaye hajui story za Mungu uone reaction yake.

Pia Tembo huwa wanaomboleza na kupatwa majonzi mwenzao akifa na hata hawana habari za mungu.
 
Umekiri mwenyewe, hawajui, sasa kama wanasayansi wenyewe wanajibu we don’t know kuhusu kilichokuwepo kabla ya Big Bang, nyinyi atheists mnaoibuka na kusema hakuna Mungu" mmetoa wapi hiyo absolute confidence?
Kwanza kabisa tuchambue neno "mungu".

Mungu ni roho yenye mamlaka ya kuumba na kutawala ulimwengu. Uungu ni cheo. Hata wewe unaweza kuupata uungu ukiweza kushawishi watu kuwa uliwaumba na unawatawala.

Miungu ipo mingi sana na ina majina yake, mfano "Yahweh" wa wakristo nk nk. Miungu ina sifa za uwepo, upendo, ujuzi na uweza.

Kwa kulinganisha sifa hizi zinazoelezwa kwenye maandiko ya kidini na maisha halisi, tunaona kwamba miungu hii haipo. Mfano, mungu mwenye upendo hawezi kuruhusu watoto wachanga wapigwe mabomu Gaza nk nk.

Ulimwengu unaweza ukawa na muumbaji hatukatai(elewa neno "muumbaji"), lakini je, huyo muumbaji ana sifa za uungu? Hapana! Yupo kweli? Hatujui. Rahisi hivyo.😊
 
We feel God...
Sawa, nami pia naamini kuwa kuna MUNGU.

Ila ukiambiwa sasa thibitisha kuwa hicho unachofeel ni MUNGU aliyeumba ulimwengu, au uthibitishe kwamba unayeamini ni MUNGU ndiye huyo huyo ninayemuamini au anayemuamini mhindu na ndiye chanzo cha yote hapo ndo mazoezi yataanza. Hayo mazoezi ni kwasababu whatever you feel inatokana na Imani Siyo fact.
 
Ukimuuliza Atheist " Hicho kitanda ulicho lalia kimetengenezwa au kimetokea tu chenyewe? " . Atakujibu kimetengenezwa na mtu.". Haya sasa muulize " Huyo mtu alie tengeneza hicho kitanda unamjua au umewahi kumuona au ulimuona wakati anakitengeneza? .. Atakwambia " Sijawahi kumuona".

Muulize tena " Kama hujawahi kumuona alie tengeneza kitanda unatumia vigezo kusema kimetengenezwa na mtu? Atakujibu " Kwa kutumia tu common sense haiwezekani kitanda kama hiki ambacho ni mashine ( simple machine) kiwe kimetokea ti chenyewe bila kutengenezwa.. "

At the same time anasema " Mwanadamu ametokea tu mwenyewe bila chanzo".

How comes kitanda ambacho ni " Simple machine" kiwe kimetengenezwa, halafu huyu mwanadamu ambae ni " Complex machine" awe ametokea tu kwa bahati?

Wazo la namna hii haliwezi kukaa kwenye kichwa cha mtu mwenye akili timamu. Something must be missing in his head.

Anazidiwa akili hata na mtoto wa miaka mitatu. Watoto karibu wote duniani at that age huwa wanawauliza wazazi at that age huwa wanawauliza wazazi wao " Mama hivi mimi mlinitoaga wapi? ".

Tayari akili yake imesha pata ukomavu wa kujua kwamba lazima atakuwa ametolewa sehemu..

Hata kwa kutumia common sense au a " Probability Test" ni ngumu sana kwa akili ya mwanadamu ambayo inawaza sawa sawa ku conclude kwamba ametokea tu..

" The probability of human being to have been created by a higher power is 99% percent "..

Atheists ni wagonjwa wa akili 🔴
Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Una elewa wewe?

Kama ulimwengu lazima uwe na chanzo, Hata hicho chanzo cha ulimwengu hakiwezi kutokea tu from nowhere. Na chenyewe lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo chake, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho.

Wagonjwa wa akili ni nyie THEISTS mnaokubali kwamba huyo Mungu wenu ali exist tu, from nowhere. Halafu mnafosi ulimwengu uliumbwa.

Kama haiwezekani ulimwengu kuwapo bila chanzo, Hata huyo Mungu haiwezekani awepo bila chanzo.

Msifosi ulimwengu uwe na chanzo, Halafu kwa huyo Mungu hamfosi chanzo chake, mnakubali tu mkichwamkichwa kwamba ali-exist bila chanzo.

It doesn't make sense.

Na pia ni logical fallacy inaitwa special pleading fallacy.

The special pleading fallacy happens when someone applies a general rule to everyone else, but claims an unjustified exception for themselves or their topic. It relies on a double standard and changes the criteria mid-argument without a valid reason.

Kama kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo, Hapapaswi kuwa na chochote kile kilicho exist chenyewe tu, pasipo chanzo. Including huyo Mungu wenu!
 
Sio sipendezwi na ufanyaji kazi wake, ni kwamba haimake sense uwepo wa huyo kiumbe wa kufanya hayo mambo
Kwanza hakuna ushahidi kama yupo, na pili kwenda motoni sio chaguo la mtu. Nani anataka kwenda motoni?
Hata mhalifu hawezi kutaka kwenda jela, lakini anaenda kwa sababu alichagua kuvunja sheria. Kwenda motoni ni suala la wewe kuchagua njia inayokupeleka huko.

Ukichagua kukataa sheria za Mungu, kuishi kwa ukaidi, na kufanya uovu, maana yake umechagua matokeo yake. Huwezi kunywa sumu kwa hiari yako halafu ukalalamika mbona inakuua!
 
Hivi kweli kuna kosa duniani linastahili kuchomwa moto wa milele? Huyo Mungu ambaye hajui hata kubalance uzito wa adhabu uendane na kosa hayupo
Yani wizi, uongo, kutoamini nk adhabu yake ni moto? Mbona ana roho mbaya hivi
 
Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Una elewa wewe?

Kama ulimwengu lazima uwe na chanzo, Hata hicho chanzo cha ulimwengu hakiwezi kutokea tu from nowhere. Na chenyewe lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo chake, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho.

Wagonjwa wa akili ni nyie THEISTS mnaokubali kwamba huyo Mungu wenu ali exist tu, from nowhere. Halafu mnafosi ulimwengu uliumbwa.

Kama haiwezekani ulimwengu kuwapo bila chanzo, Hata huyo Mungu haiwezekani awepo bila chanzo.

Msifosi ulimwengu uwe na chanzo, Halafu kwa huyo Mungu hamfosi chanzo chake, mnakubali tu mkichwamkichwa kwamba ali-exist bila chanzo.

It doesn't make sense.

Na pia ni logical fallacy inaitwa special pleading fallacy.

The special pleading fallacy happens when someone applies a general rule to everyone else, but claims an unjustified exception for themselves or their topic. It relies on a double standard and changes the criteria mid-argument without a valid reason.

Kama kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo, Hapapaswi kuwa na chochote kile kilicho exist chenyewe tu, pasipo chanzo. Including huyo Mungu wenu!
Wewe ni Atheists?
 
Hao jamaa wana matatizo kichwani.
Wenye matatizo kichwani ni nyie THEISTS mnaokubali na kuamini mkichwamkichwa kwamba huyo Mungu wenu hana chanzo, alizuka tu from nothing!

Halafu mnafosi ulimwengu uliumbwa.
Kitanda kidogo tu wanajua kina fundi, lakini mfumo tata wa binadamu eti umetokea kwa bahati mbaya, huwa wananishangaza sana.
Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

Kama haiwezekani ulimwengu kutokea tu wenyewe, Hata huyo Mungu hawezi kutokea tu mwenyewe.

Kama kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake hata huyo Mungu atahitaji kuwa na chanzo chake.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu pasipo chanzo.

Na kama si kila kitu kilichopo kinahitaji kuwa na chanzo chake, Hata Ulimwengu na vyote vilivyomo except man-made things, havina na havihitaji kuwa na chanzo.
 
Mfumo wa binadamu sio wa kipekee kwa wanyama wengine.
Hivyo hakuna upekee
Hoja rahisi sana hii, kama ukienda barabarani ukakuta gari la Toyota na gari la Suzuki zote zina matairi manne, usukani, na injini inayotumia piston, utasema hayo magari yamejitengeneza yenyewe kwa sababu yanafanana?
 
Kwenye falsafa hiyo hiyo unayotaka kuigusia, kuna kanuni inaitwa occam’s razor inasema kwamba jibu rahisi na lenye mantiki zaidi ndilo la kweli. Kuliko kubuni nadharia ya kamati ya miungu elfu moja waliokaa kikao kuunda ulimwengu, ni rahisi na ina mantiki zaidi kukubali uwepo wa Muumba Mmoja Mwenye Nguvu Zote.
Sasa Mungu sio jibu rahisi.

Na ndio maana hakuna uthibitisho wa uwepo wake.

Dhana ya Mungu haina mantiki na ndio maana utaona miongozo yake ipo katika msingi wa imani.

Imani sio mantiki.

Kwa hiyo kwa kanuni yako mwenyewe ambayo umeitaja, inapingana kabisa na swala la Mungu.
 
Ukimuuliza Atheist " Hicho kitanda ulicho lalia kimetengenezwa au kimetokea tu chenyewe? " . Atakujibu kimetengenezwa na mtu.". Haya sasa muulize " Huyo mtu alie tengeneza hicho kitanda unamjua au umewahi kumuona au ulimuona wakati anakitengeneza? .. Atakwambia " Sijawahi kumuona".

Muulize tena " Kama hujawahi kumuona alie tengeneza kitanda unatumia vigezo kusema kimetengenezwa na mtu? Atakujibu " Kwa kutumia tu common sense haiwezekani kitanda kama hiki ambacho ni mashine ( simple machine) kiwe kimetokea ti chenyewe bila kutengenezwa.. "

At the same time anasema " Mwanadamu ametokea tu mwenyewe bila chanzo".

How comes kitanda ambacho ni " Simple machine" kiwe kimetengenezwa, halafu huyu mwanadamu ambae ni " Complex machine" awe ametokea tu kwa bahati?

Wazo la namna hii haliwezi kukaa kwenye kichwa cha mtu mwenye akili timamu. Something must be missing in his head.

Anazidiwa akili hata na mtoto wa miaka mitatu. Watoto karibu wote duniani at that age huwa wanawauliza wazazi at that age huwa wanawauliza wazazi wao " Mama hivi mimi mlinitoaga wapi? ".

Tayari akili yake imesha pata ukomavu wa kujua kwamba lazima atakuwa ametolewa sehemu..

Hata kwa kutumia common sense au a " Probability Test" ni ngumu sana kwa akili ya mwanadamu ambayo inawaza sawa sawa ku conclude kwamba ametokea tu..

" The probability of human being to have been created by a higher power is 99% percent "..

Atheists ni wagonjwa wa akili 🔴
Ndiyo, atheist anaweza kuwa na ugonjwa wa akili, kama ilivyo kwa mtu wa dini yoyote.

Lakini kutokuwa na imani katika Mungu si ugonjwa wa akili. Atheism ni msimamo wa kutokuamini uwepo wa Mungu; ugonjwa wa akili ni hali ya kiafya inayoweza kutambuliwa kwa dalili na tathmini ya kitaalamu.

Kwa hiyo, kusema “atheist ni mgonjwa wa akili kwa sababu haamini Mungu” si sahihi.
 
Sawa, nami pia naamini kuwa kuna MUNGU.

Ila ukiambiwa sasa thibitisha kuwa hicho unachofeel ni MUNGU aliyeumba ulimwengu, au uthibitishe kwamba unayeamini ni MUNGU ndiye huyo huyo ninayemuamini au anayemuamini mhindu na ndiye chanzo cha yote hapo ndo mazoezi yataanza. Hayo mazoezi ni kwasababu whatever you feel inatokana na Imani Siyo fact.
Usiogope
 
Hii mada ngumu.
Nikuulize kama mwanadamu lazima ameumbwa na fulani (Mungu). Kila kitu lazima kiwe kimeumbwa.
Huyo fulani naye lazima ameumbwa, tukifuata mtiririko wako wa kujenga hoja.
Je, huyo aliye muumba mwanadamu ameumbwa na nani?
Huoni kunakuwa na an endless cycle ya kutafuta muumbaji?

Angalizo: NAAMINI Mungu yupo.
 
🤣🤣🤣 Mbona unajiwahi mkuu? Anyways, sometimes uoga/ hofu, ndio akili. Nimekukubali sana mkuu
 
Alie muumba anamuhusu yeye. Mimi anae ni husu ni huyu alieniumba
Hili siyo jibu.
Ukisema lazima Kila kitu kiwe na mtengenezaji wake, basi hata Mungu lazima awe na aliyemuumba.
Huwezi kuishia juu juu tu kwamba aliyemuumba huyo aliyekuumba yeye hakuhusu.

Kwa ufupi binadamu ndiyo wamemtengeneza au wamemuumba Mungu.
 
Mtu wa kwanza aliumbwa..
Mtu wa kwanza nani?

Una uthibitisho kulikuwa na mtu wa kwanza?

Nani alimuona huyo mtu wa kwanza akiumbwa? 
We are the descendants.. It doesnt need Rocket science to understand that
Kama sisi ni descendants, iweje tuna tofautiana rangi na vinasaba?

Kama sisi ni descendants, iweje kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea, wajapani?

Inakuwaje descendants tuna tofautiana?

Kwa nini hatufanani kwenye kila kitu kama origin yetu ni mtu mmoja wa mwanzo?
 
Back
Top Bottom