Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Tufanye ni chuki na dini yeah
Ila mimi siamini vitu ambavyo akilini mwangu havimake sense. Eti ni muweza wa yote ila anaamua tu kuacha watu duniani waendelee kuteseka na kufanyiana ukatili. Au tukifa ipo siku tutapaa kwenda kuonana nae. Ana huruma ila atatuchoma moto tusiomwamini, tena moto wa milele. Kwenye Biblia kaua watu wengi, anaonekana ni short tempered na mwenye hasira za karibu. Ana madhaifu mengi sana
Safi sana kwa kuwa mkweli, kumbe hoja hapa sio sayansi wala mantiki, ni emotional resentment dhidi ya dini. Unamuhukumu Mungu kwa vigezo vyako vya kibinadamu. Ni kichekesho kukataa uwepo wa kitu kwa sababu tu hupendi jinsi kinavyofanya kazi au sheria zake.

Malalamiko yako yote yanatokana na mtazamo wako finyu wa kuona maisha ni haya ya duniani tu, moto wa milele ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe.
 
Angalia wewe usije kua ndiyo mgonjwa wa akili
Kama Mungu ni huyo wa kwenye bible & Qur’an basi kasheshe !
Twin umeshawahi kujiuliza what if vitabu vya dini viko sawa? Kama sisi waumini tukifa tukakuta hakuna kitu, hatujapoteza kitu. Lakini wewe ukifa ukakuta yule Mungu wa Biblia na Qur'an yupo na moto wake upo vilevile, nani atakuwa kwenye kasheshe kubwa zaidi?
 
Hii ni kweli ?..

Sijawahi kuwa na hiyo perspective, ila kwa niliowaona au kuwasikia. Wengi huwa ni diaspora
Diaspora wengi wana maisha magumu..

Mkuu kama maisha yako yanakuendea vizuri huwezi kupata wazo la kusema Mungu hayupo...
 
Safi sana kwa kuwa mkweli, kumbe hoja hapa sio sayansi wala mantiki, ni emotional resentment dhidi ya dini. Unamuhukumu Mungu kwa vigezo vyako vya kibinadamu. Ni kichekesho kukataa uwepo wa kitu kwa sababu tu hupendi jinsi kinavyofanya kazi au sheria zake.

Malalamiko yako yote yanatokana na mtazamo wako finyu wa kuona maisha ni haya ya duniani tu, moto wa milele ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe.
Sio sipendezwi na ufanyaji kazi wake, ni kwamba haimake sense uwepo wa huyo kiumbe wa kufanya hayo mambo
Kwanza hakuna ushahidi kama yupo, na pili kwenda motoni sio chaguo la mtu. Nani anataka kwenda motoni?
 
Twin umeshawahi kujiuliza what if vitabu vya dini viko sawa? Kama sisi waumini tukifa tukakuta hakuna kitu, hatujapoteza kitu. Lakini wewe ukifa ukakuta yule Mungu wa Biblia na Qur'an yupo na moto wake upo vilevile, nani atakuwa kwenye kasheshe kubwa zaidi?
Kasheshe kwangu twin
 
Ukisema kuna uovu na mateso maana yake unaamini kuna wema na haki, sasa swali ni hili, bila Mungu, unapata wapi kipimo cha ulimwengu mzima cha kusema hiki ni kibaya na hiki ni kizuri?

Kwenye u-atheist na nadharia ya evolution, hakuna uovu, kuna viumbe wenye nguvu kuwadhuru wanyonge tu ili wasurvive, huoni unapotaja uovu, unathibitisha kuwepo kwa sheria ya Mungu moyoni mwako bila wewe kujua?
Nimeshawai kuibiwa, kudhulimwa, kuumwa magonjwa, kushinda njaa, kufiwa n.k. Hata bila uwepo wa story za mungu bado ningepata maumivu au ningejisikia vibaya tu kwa hayo yote na binadamu wengine ndivyo hivyo hivyo tu.
 
Mambo mengi tu tunaweza kujua ni makosa, sio sahihi na haya make sense bila hata kujua usahihi au ukweli ni upi. Watanzania karibia wote wanajua Samia hakupata 98% ya kura na watu milioni 31 hawakupiga kura katika uchaguzi wa 2025 hata kama hawajui namba sahihi za huo uchaguzi ni zipi.
Kwenye mfano wako huo huo, watanzania wanajua hizo namba si sahihi kwa sababu wanajua hakuna uchaguzi halisi uliotokea, yaani, wanajua kuna chanzo halisi cha wao kusema hivyo. Sasa wewe unayetumia huo mfano kumkataa Mungu, maana yake unakiri kuwa ulimwengu una mfumo halisi na muundo, ila unabisha tu kuwa takwimu zilizopo si sahihi. Kifupi umekuwa agnostic tena.
 
Twin umeshawahi kujiuliza what if vitabu vya dini viko sawa? Kama sisi waumini tukifa tukakuta hakuna kitu, hatujapoteza kitu. Lakini wewe ukifa ukakuta yule Mungu wa Biblia na Qur'an yupo na moto wake upo vilevile, nani atakuwa kwenye kasheshe kubwa zaidi?
Hata mungu wa Biblia na Quran kuwa mmoja ni jambo haliwezekani, hiyo ni contradiction tayari.
 
Ukimuuliza Atheist " Hicho kitanda ulicho lalia kimetengenezwa au kimetokea tu chenyewe? " . Atakujibu kimetengenezwa na mtu.". Haya sasa muulize " Huyo mtu alie tengeneza hicho kitanda unamjua au umewahi kumuona au ulimuona wakati anakitengeneza? .. Atakwambia " Sijawahi kumuona".

Muulize tena " Kama hujawahi kumuona alie tengeneza kitanda unatumia vigezo kusema kimetengenezwa na mtu? Atakujibu " Kwa kutumia tu common sense haiwezekani kitanda kama hiki ambacho ni mashine ( simple machine) kiwe kimetokea ti chenyewe bila kutengenezwa.. "

At the same time anasema " Mwanadamu ametokea tu mwenyewe bila chanzo".

How comes kitanda ambacho ni " Simple machine" kiwe kimetengenezwa, halafu huyu mwanadamu ambae ni " Complex machine" awe ametokea tu kwa bahati?

Wazo la namna hii haliwezi kukaa kwenye kichwa cha mtu mwenye akili timamu. Something must be missing in his head.

Anazidiwa akili hata na mtoto wa miaka mitatu. Watoto karibu wote duniani at that age huwa wanawauliza wazazi at that age huwa wanawauliza wazazi wao " Mama hivi mimi mlinitoaga wapi? ".

Tayari akili yake imesha pata ukomavu wa kujua kwamba lazima atakuwa ametolewa sehemu..

Hata kwa kutumia common sense au a " Probability Test" ni ngumu sana kwa akili ya mwanadamu ambayo inawaza sawa sawa ku conclude kwamba ametokea tu..

" The probability of human being to have been created by a higher power is 99% percent "..

Atheists ni wagonjwa wa akili 🔴
Wanaoamini kwamba hakuna MUNGU wamebase kwenye udhaifu wa tunaoamini kuwa MUNGU yupo.

Mfano

Udhaifu wa 1:

Wewe mwamini mwenzangu ukiulizwa, kama kila kitu lazima kiwe na chanzo, chanzo cha MUNGU ni nini? Na je kama kipo hicho Chanzo si ndo kinastahili kuwa MUNGU? Na hicho kinachostahili kuwa chanzo chanzo chake? So utajikuta ukisema kila kitu kina chanzo basi concept ya MUNGU haitaisha, itaendelea tu weee.

Udhaifu wa 2:
Ukisema MUNGU hana chanzo it means unasema sio kila kitu kina chanzo. Sasa je, kwanini ishindikane binadamu kutokuwa na chanzo? Au dunia kutokuwa na chanzo? Kama MUNGU aliweza kutokea tu kwanini sio binadamu au ulimwengu?

Haya madhaifu yote yapo kwa mujibu wa fact.

Lakini je sisi waamini MUNGU tunaamini kwa fact?

Jibu ni hapana, tunaamini kwa Imani na hapa ndipo matatizo ya kisaikolojia yanapoonekana kwa wasio amini sababu watataka fact sizizo za kiimani kuthibitishiwa suala la kiimani.
 
Kwenye mfano wako huo huo, watanzania wanajua hizo namba si sahihi kwa sababu wanajua hakuna uchaguzi halisi uliotokea, yaani, wanajua kuna chanzo halisi cha wao kusema hivyo. Sasa wewe unayetumia huo mfano kumkataa Mungu, maana yake unakiri kuwa ulimwengu una mfumo halisi na muundo, ila unabisha tu kuwa takwimu zilizopo si sahihi. Kifupi umekuwa agnostic tena.
Hata Watanzania wanaoamini uchaguzi ulifanyika hizo namba wanajua ni za kuchonga tu.
 
Wanaoamini kwamba hakuna MUNGU wamebase kwenye udhaifu wa tunaoamini kuwa MUNGU yupo.

Mfano

Udhaifu wa 1:

Wewe mwamini mwenzangu ukiulizwa, kama kila kitu lazima kiwe na chanzo, chanzo cha MUNGU ni nini? Na je kama kipo hicho Chanzo si ndo kinastahili kuwa MUNGU? Na hicho kinachostahili kuwa chanzo chanzo chake? So utajikuta ukisema kila kitu kina chanzo basi concept ya MUNGU haitaisha, itaendelea tu weee.

Udhaifu wa 2:
Ukisema MUNGU hana chanzo it means unasema sio kila kitu kina chanzo. Sasa je, kwanini ishindikane binadamu kutokuwa na chanzo? Au dunia kutokuwa na chanzo? Kama MUNGU aliweza kutokea tu kwanini sio binadamu au ulimwengu?

Haya madhaifu yote yapo kwa mujibu wa fact.

Lakini je sisi waamini MUNGU tunaamini kwa fact?

Jibu ni hapana, tunaamini kwa Imani na hapa ndipo matatizo ya kisaikolojia yanapoonekana kwa wasio amini sababu watataka fact sizizo za kiimani kuthibitishiwa suala la kiimani.
We feel God...
 
Nimeshawai kuibiwa, kudhulimwa, kuumwa magonjwa, kushinda njaa, kufiwa n.k. Hata bila uwepo wa story za mungu bado ningepata maumivu au ningejisikia vibaya tu kwa hayo yote na binadamu wengine ndivyo hivyo hivyo tu.
Pole sana kwa matatizo, iHiyo hali ya kujisikia vibaya, kuona umeonewa, na kuona kudhulumiwa ni makosa, mnaipata wapi nyinyi ma-atheist?

Kwenye ulimwengu wa evolution na u-atheist, hakuna kitu kinaitwa dhuluma au wizi. Kuna mwenye nguvu kumyang'anya mnyonge.

Kujisikia kwako vibaya baada ya kufanyiwa hivyo kunathibitisha kuna sheria ya Mungu ya kimaadili iliyopo ndani ya moyo wako, hivyo yani.
 
Back
Top Bottom