Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Mtoto anazaliwa hana "ushahidi" kwamba mama yake ni mama yake. Lakini "anajua" ndani yake. Anajihusisha naye. Baadaye ndio anapata ushahidi: sauti, harufu, maziwa.

Kama tungesubiri ushahidi kwanza, hatungeamini chochote.

Mambo yako hivi:-

1. Kujua kwa silika/ Uzoefu. Unajua moto unachoma hata kabla hujaona ripoti ya kisayansi.

Unajua 2+2=4 hata kabla mwalimu hajaandika ubaoni. Maarifa ya moja kwa moja.

2. Kutafuta ushahidi. Baada ya kujua, akili yako inasema: ngoja nithibitishe hili ni kweli kweli. Ndipo unatafuta ushahidi. Unapima, unauliza, unaangalia.

3. Kuimarisha kujua. Ushahidi unapokuja, unageuza "ninajua" kuwa "ninajua kwa uhakika."
Dai la kwanza kupokelewa ni ujuzi?
Sasa ukianza kwa kujua
vipi ushahidi unaofata usipothibitisha ulichodhani ni ujuzi rasmi tiyari?
Kama ujuzi ndo unaanza, mtu anajuaje kwamba hajui
 
Mfano wa 0 ni scam tu, 0 haikuumba 1, 2, 3; 0 ni sehemu ya mfumo wa namba, si chanzo kinachozalisha namba. Kwa hiyo 0 kuwa reference point hakuthibitishi kwamba lazima kuwe na ‘chanzo cha kwanza’ cha ulimwengu.
Kwa lugha rahisi haukubaliana na akili yako.
 
Dai la kwanza kupokelewa ni ujuzi?
Sasa ukianza kwa kujua
vipi ushahidi unaofata usipothibitisha ulichodhani ni ujuzi rasmi tiyari?
Kama ujuzi ndo unaanza, mtu anajuaje kwamba hajui
Jibu la swali lako ni "HUKUWAHI KUJUA."
 
Mfano wa mtoto hauonyeshi kwamba mtoto anajua mama yake ni mama yake kabla ya ushahidi. Anaanza na attachment na biological recognition, si knowledge ya kimantiki kwamba ‘huyu ndiye mama yangu.’ Sauti, harufu na maziwa unazotaja ndiyo evidence inayojenga hiyo recognition.
Biological recognitioni ni nini?

Kwa nini attachment itokee? Kwa sababu kuna "kujua", kujua kwa silika. (Subconscious mind)

Kwa hiyo tendo hilo au shughuli hiyo ni tokeo la kujua.
 
Kama mtoto anakuja kumtambua mama yake kupitia harufu, sauti na maziwa, basi kwa mantiki hiyo hiyo, huyo Mungu mnayedai ndiye aliyeumba Dunia, alitupa njia gani ya moja kwa moja ya kumtambua? Kama mtoto amepewa njia ya kumtambua mama yake, kwa nini sisi tusipewe njia ya kumtambua Muumba wetu?
UBONGO WAKO.

Unapokosea ubongo wako unakulaumu. Unapofanya vema ubongo wako unakusifu.
 
Kwa nini attachment itokee? Kwa sababu kuna "kujua", kujua kwa silika.

Kwa hiyo tendo hilo au shughuli hiyo ni tokeo la kujua.

Tatizo lako hapa ni kwamba unachanganya instinct na knowledge. Attachment ya mtoto ni biological response, si ushahidi kwamba mtoto ana maarifa ya kufahamu ‘huyu ndiye mama yangu.’

Ukisema kila instinct ni ‘kujua’, basi umebadilisha maana ya neno kujua kiasi kwamba hata reflex ya mwili inakuwa knowledge. Hapo huwezi tena kutumia ‘kujua’ kama ushahidi wa ukweli.

Kwa hiyo usitumie attachment ya mtoto kuthibitisha kwamba mwanadamu ‘anamjua Mungu kwa silika.’ Umeonyesha kwamba mwanadamu ana instincts; hujaonyesha kwamba instincts hizo zinampa knowledge ya Mungu.

Thibitisha Mungu aliumba Dunia acha mizinguko
 
Nichukuwe huu mfano wako na hapa nanukuu" Unasema Tundu lisu ni Gaidi wewe ndio inabidi utoe evidence."

Kwenye maelezo yangu nimesema nyuma ya ulimwengu angalau vitu vya asili vinavyoooneka kuna "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili" tunaouita Mungu.

Sababu za kufikia hitimisho hilo ni jinsi gani ulimwengu ulivyotokea; ulivyo na mpangilio na muundo, unavyofanya kazi na unavyoendelea.

Aidha, (sababu nyingine) ni maarifa ya binadamu. Maafia ya binadamu yana asili ya huo Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili (Mungu).

Binadamu ameweza kuunda mitambo baada ya kuangalia vitu vya asili jinsi vinavyofanya kazi. Amejifunza sheria za fizikia; akajifunza viumbe hai jinsi vinafanya kazi akaunda mitambo mbalimbali.

Kwa lugha rahisi ameiga vitu vya asili kuunda vifaa mbalimbali.
Nimeona kumbe ulinijibu 📌

Mfano wako wa binadamu kuiga nature hausaidii, Binadamu anapotengeneza ndege kwa kuiga ndege, tunajua kuna designer kwa sababu tunamuona designer huyo na tunaona mchakato wa kutengeneza. Hatujui ndege ameundwa kwa sababu tu ana mabawa; tunajua kwa sababu tuna ushahidi wa mtengenezaji.

Sasa kwenye ulimwengu unafanya reverse: unaona mfumo wenye mpangilio, halafu unasema lazima kuna Designer. Nionyeshe evidence inayothibitisha huyo Designer, si evidence ya kwamba ulimwengu una mpangilio.

Na kusema “binadamu ameiga nature” kunathibitisha kwamba nature ina patterns ambazo binadamu anaweza kujifunza. Hakuthibitishi kwamba pattern hizo ziliwekwa na akili. Tunaweza kujifunza sheria za gravity bila hiyo yenyewe kuthibitisha nani ‘aliandika’ gravity.
 
Mungu yeye ametoka wapi ? Chanzo chake ni kipi?
Nikifika kwenye hili swali huwa na stack

Ni one ☝️of the most honesty question for really

Hili swali dini limelitafutia majibu ya kutuliwaza na hii ndio maana hata dini zinaonekana hazijui na zinadanganya

I agree ni kweli kuna some natural super power above us , some call God !
But what is his/ her source ?

Haiwezekani awe ametokea from no where yaani ilikuaje kuaje hadi akatokea ? Shida na kuzaliwa kwa ma atheist ndio imetokea hapa

Ni very open question kwa mtu mwenye kufikiri kwa utimamu
 
Mfano wako wa binadamu kuiga nature hausaidii, Binadamu anapotengeneza ndege kwa kuiga ndege, tunajua kuna designer kwa sababu tunamuona designer huyo na tunaona mchakato wa kutengeneza. Hatujui ndege ameundwa kwa sababu tu ana mabawa; tunajua kwa sababu tuna ushahidi wa mtengenezaji.

Sasa kwenye ulimwengu unafanya reverse: unaona mfumo wenye mpangilio, halafu unasema lazima kuna Designer. Nionyeshe evidence inayothibitisha huyo Designer, si evidence ya kwamba ulimwengu una mpangilio.

Na kusema “binadamu ameiga nature” kunathibitisha kwamba nature ina patterns ambazo binadamu anaweza kujifunza. Hakuthibitishi kwamba pattern hizo ziliwekwa na akili. Tunaweza kujifunza sheria za gravity bila hiyo yenyewe kuthibitisha nani ‘aliandika’ gravity.
Nataka kuwa wazi hapa. Haya sio mabishano. Ni kuelewa na kujua ukweli ambao ndio lengo la mwisho la kima mtu.

Maelezo niliotoa kwenye comment 498 yanaeleza kwa nini nimefikia hitimisho la Uwepo wa hali ya juu wenye akili (designer) tunaouita Mungu.

Sababu niloyotoa ni pamoja na "maarifa ya binadamu" au kwa mameno mengine "akili ya binadamu."

Nimezungumza suala la uelewa.

Tunaona matokeoa ya akili ya binadamu (maarifa ya binadamu au kazi za ubongo wa binadamu). Binadamu anaunda vifaa. Anatengeneza mitambo . Anaweza kujua mfumo mwingine wa jua nje ya mfumo wetu wa jua.

Hayo tunayoyaona ambayo akili ya binadamu imeunda, inatengeneza: vifaa, mitambo ni matokeo.

Hatusemi mtambo wa MRI ni akili. Tunasema mtambo huo ni matokeo ya kazi ya ubongo, akili ya binadamu.

Sasa, Akili ya binadamu iko wapi?

Kwa lugha nyingine ulivyouliza.

kama ulimwengu kwa sababu ya mpangilio, muundo na unavyofanya kazi, ni tokeo la Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili.

Uwepo huo wa Hali ya Juu Wenye Akili uko wapi? Hili ndilo swali lako.

Kwa mujibu wa sayansi hatuna kitu kinaitwa akili. Tuna kazi au shughuli za ubongo.

Kwa nini kadiri ya sayansi hatuna kitu kinaitwa akili. Kwa sababu sayansi haiwezi kupima akili. Inaweza kupima athari au matokeo ya akili.

Hii ni kwa sababu sayansi ni mtalaamu wa kupima vitu vinavyoweza kuonekana, kupimwa na kurudiwa.

Sayansi inaweza kupima:-

1. Ubongo = Uzito, Ukubwa, shughuli za umeme - MRI, EEG.

2. Kasi = Unatatua maswali kwa dakika ngapi.

3. Kumbukumbu = Unakumbuka maneno mangapi.

4. Matokeo = IQ test, Mitihani, Kazi uliomaliza.

Sayansi haiwezi kupima moja kwa moja:-

1. Ufahamu = Ninahisi nini sasa? Huwezi kuiweka kwenye bomba.

2. Maana = Kwa nini shairi hili linakuuliza?

3.Upendo = Unaupima kwa gramu ngapi?

4.Uchaguzi = Kwa nini uliamua kusaidia mtu badala ya kujibania?

Haya manne yaani Ufahamu, Maana, Upendo, Uchaguzi ndio Akili Yenyewe. "Ni moto unaotoa moshi."

Kwanini sayansi haiti akili badala yake inaita shughuli za ubongo?

Kwa sababu:-

1. Akili siyo ya kimwili, si kitu.

2. Sayansi inashughulika na vitu.

3. Akili inashughulika na maana.

Wazo la Mungu (Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili) linatoka wapi?

Imani.

Imani inasema ulimwengu umeumbwa na Mungu, ambae neno hilo tunaloliita Mungu maana yake ni "uwepo wa hali ya juu wenye akili."

Na kwamba mtu anaweza kumjua huyo Mungu kwa kupitia yeye mwenyewe na kwa kupitia vitu vya asili vilivyopo.

Yeye mwenyewe kwa sababu ya hali yake ya akili.

Vitu vya asili kwa sababu ya mpangilio, muundoa na ufanyaji kazi wao.

Zaidi, huyo Mungu anaongea na mtu kupitia dhamiri - hali inayokulaumu ukifanya vibaya na inayokupongeza ukifanya vizuri.

Tunaweza kuthibitisha hilo kwa kuchunguza ubongo unakuwaje mtu akifanya vibaya na unakuwaje akifanya vizuri.

HITIMISHO
Sayansi haijengi imani. Inaonyesha imani iliyopo tayari kwa kuonyesha "Jinsi gani," ilivyo.

Kwa lugha rahisi Sayansi ni taa na Imani ni jua.

Taa Inakusaidia kutembea usiku. Inakuonyesha miiba na mashimo.

Lakini taa haiwezi kuchomoza jua. Jua linachomoza lenyewe.
 
Walokole bana

Maneno meeeeeengi Kisa tu umeulizwa onesha Mungu Yuko wapi!!!

Sasa Kwa ufupi na sitaki nijibu Kila hoja yako hapo maana unaandika vitu Ambavyo kwangu havina man tiki,

Tunajua MRI ina designer kwa sababu tuna ushahidi wa watu walioitengeneza na mchakato wa kuitengeneza. Kwa ulimwengu, umeonyesha mpangilio, lakini bado hujaonyesha ushahidi wa Designer wake ni yupi!!!

Rudi kwenye hoja kuu onesha designer wa Dunia ni nani ?

Weka evidence mzee acha maneno.

Lete vyombo

Lete ushahidi
 
Mkuu, unaendelea kuzunguka tu kwenye mfano wa mtoto wakati hoja kuu bado hujajibu: nani ni Designer wa Dunia?

Umesema kuna mpangilio, hivyo kuna akili nyuma yake. Sawa. Tueleze huyo Designer ni nani, na una ushahidi gani wa kumtambua?

Mfano wa mtoto na attachment haujibu hilo. Hata tukikubali kujua kwa silika, bado hujaonyesha kwamba silika hiyo inatuelekeza kwa Designer wa ulimwengu.

Kwa kifupi, umeonesha unaamini kuna Designer lakini hujatuonesha huyo Designer. Kila siku mnamuabudu huyo Mungu wenu ( Designer) kwanini mnapata tabu tukututhibitishia Ili na sisi tuanze kwenda kanisani kumuabudu badala yake mnazunguka.

Biological recognitioni ni nini?
Kwa nini attachment itokee? Kwa sababu kuna "kujua", kujua kwa silika. (Subconscious mind)

Kwa hiyo tendo hilo au shughuli hiyo ni tokeo la kujua.
 
Tunajua MRI ina designer kwa sababu tuna ushahidi wa watu walioitengeneza na mchakato wa kuitengeneza. Kwa ulimwengu, umeonyesha mpangilio, lakini bado hujaonyesha ushahidi wa Designer wake ni yupi!!!
Narudia kusema tena.

Tatizo lako ni uelewa.

Mfano wa MRI.

Unachoweza kuonyesha hapo ni watu kwa maana ya umbo la binadamu. Sio akili ya binadamu.

Swali. Unaweza kunionyesha akili ya binadamu iko wapi?

Unaweza kunionyesha hizo shughuli za ubongo ambazo wewe na mimi tunaona matokeo yake, mfano MRI zinafananaje?

Kwa lugha rahisi unaweza kunionyesha ufahamu unafananaje?

Mchakato wa kutengeneza unaouzungumzia ni uunganishaji wa hiyo MRI (assembling).

Lakini kabla ya hiyo MRI haijatokea kama mashine lilikuwa wazo. Sasa unaweza kunionyesha huo mchakato wa wazo ambao matokeo yake ni hiyo mashine ya MRI?
 
Mkuu, unaendelea kuzunguka tu kwenye mfano wa mtoto wakati hoja kuu bado hujajibu: nani ni Designer wa Dunia?

Umesema kuna mpangilio, hivyo kuna akili nyuma yake. Sawa. Tueleze huyo Designer ni nani, na una ushahidi gani wa kumtambua?

Mfano wa mtoto na attachment haujibu hilo. Hata tukikubali kujua kwa silika, bado hujaonyesha kwamba silika hiyo inatuelekeza kwa Designer wa ulimwengu.

Kwa kifupi, umeonesha unaamini kuna Designer lakini hujatuonesha huyo Designer. Kila siku mnamuabudu huyo Mungu wenu ( Designer) kwanini mnapata tabu tukututhibitishia Ili na sisi tuanze kwenda kanisani kumuabudu badala yake mnazunguka.
Mwelekeo wako unazingatia sayansi.

Hatahivyo, ni wazi hiyo sayansi unayoizingatia bado pia hujaijua vizuri zaidi ya ushabiki.

Kwa nini? Unachanganya sayansi na imani. Unashindwa kuelewa kwamba sayansi inashughulikia swali "jinsi gani" na imani anashughulikia swali "Kwa nini."

Sayansi inaongoza kwa kanuni ya kupima. Kama kitu hakipimiki kwa sayansi hicho kitu hakipo.

Tuelewe kwamba sayansi ni maarifa yanaokua na kuendelea. Ndio sababu yanaweza kusahihishwa.

Lakini katikati ya maarifa ya sayansi, katikati ya akili ya binadamu kuna ukweli (imani) ambao wenyewe upo tu. Uwe unapimika au haupimiki, unaonekana au hauonekani, unajua au haujui. Ukweli upo tu.

Kwisha kusema hayo.

Akili ya binadamu iko wapi?
 
hapo unachanganya kutopimwa moja kwa moja na kutokuwepo. Sayansi haisemi “kisichopimika hakipo”; inasema claim kuhusu uhalisia inahitaji evidence.

Akili tunaiona kupitia matokeo yake na uhusiano wake na ubongo. Ubongo ukibadilika, memory, tabia na maamuzi vinaweza kubadilika. Kwa hiyo “akili haipimiki moja kwa moja” si evidence kwamba iko nje ya ubongo.

Wewe leta evidence kuwa Mungu ni Designer wa Dunia acha maneno bwasheeeeeeeee🙂‍↕️
 
Ila Makerubi mda mwingine mnajichosha bure, kwani lazima kila mtu aamini hizo story za uongo za Kitu kisicho onekana, Khaaah.
 
Nataka kuwa wazi hapa. Haya sio mabishano. Ni kuelewa na kujua ukweli ambao ndio lengo la mwisho la kima mtu.

Maelezo niliotoa kwenye comment 498 yanaeleza kwa nini nimefikia hitimisho la Uwepo wa hali ya juu wenye akili (designer) tunaouita Mungu.

Sababu niloyotoa ni pamoja na "maarifa ya binadamu" au kwa mameno mengine "akili ya binadamu."

Nimezungumza suala la uelewa.

Tunaona matokeoa ya akili ya binadamu (maarifa ya binadamu au kazi za ubongo wa binadamu). Binadamu anaunda vifaa. Anatengeneza mitambo . Anaweza kujua mfumo mwingine wa jua nje ya mfumo wetu wa jua.

Hayo tunayoyaona ambayo akili ya binadamu imeunda, inatengeneza: vifaa, mitambo ni matokeo.

Hatusemi mtambo wa MRI ni akili. Tunasema mtambo huo ni matokeo ya kazi ya ubongo, akili ya binadamu.

Sasa, Akili ya binadamu iko wapi?

Kwa lugha nyingine ulivyouliza.

kama ulimwengu kwa sababu ya mpangilio, muundo na unavyofanya kazi, ni tokeo la Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili.

Uwepo huo wa Hali ya Juu Wenye Akili uko wapi? Hili ndilo swali lako.

Kwa mujibu wa sayansi hatuna kitu kinaitwa akili. Tuna kazi au shughuli za ubongo.

Kwa nini kadiri ya sayansi hatuna kitu kinaitwa akili. Kwa sababu sayansi haiwezi kupima akili. Inaweza kupima athari au matokeo ya akili.

Hii ni kwa sababu sayansi ni mtalaamu wa kupima vitu vinavyoweza kuonekana, kupimwa na kurudiwa.

Sayansi inaweza kupima:-

1. Ubongo = Uzito, Ukubwa, shughuli za umeme - MRI, EEG.

2. Kasi = Unatatua maswali kwa dakika ngapi.

3. Kumbukumbu = Unakumbuka maneno mangapi.

4. Matokeo = IQ test, Mitihani, Kazi uliomaliza.

Sayansi haiwezi kupima moja kwa moja:-

1. Ufahamu = Ninahisi nini sasa? Huwezi kuiweka kwenye bomba.

2. Maana = Kwa nini shairi hili linakuuliza?

3.Upendo = Unaupima kwa gramu ngapi?

4.Uchaguzi = Kwa nini uliamua kusaidia mtu badala ya kujibania?

Haya manne yaani Ufahamu, Maana, Upendo, Uchaguzi ndio Akili Yenyewe. "Ni moto unaotoa moshi."

Kwanini sayansi haiti akili badala yake inaita shughuli za ubongo?

Kwa sababu:-

1. Akili siyo ya kimwili, si kitu.

2. Sayansi inashughulika na vitu.

3. Akili inashughulika na maana.

Wazo la Mungu (Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili) linatoka wapi?

Imani.

Imani inasema ulimwengu umeumbwa na Mungu, ambae neno hilo tunaloliita Mungu maana yake ni "uwepo wa hali ya juu wenye akili."

Na kwamba mtu anaweza kumjua huyo Mungu kwa kupitia yeye mwenyewe na kwa kupitia vitu vya asili vilivyopo.

Yeye mwenyewe kwa sababu ya hali yake ya akili.

Vitu vya asili kwa sababu ya mpangilio, muundoa na ufanyaji kazi wao.

Zaidi, huyo Mungu anaongea na mtu kupitia dhamiri - hali inayokulaumu ukifanya vibaya na inayokupongeza ukifanya vizuri.

Tunaweza kuthibitisha hilo kwa kuchunguza ubongo unakuwaje mtu akifanya vibaya na unakuwaje akifanya vizuri.

HITIMISHO
Sayansi haijengi imani. Inaonyesha imani iliyopo tayari kwa kuonyesha "Jinsi gani," ilivyo.

Kwa lugha rahisi Sayansi ni taa na Imani ni jua.

Taa Inakusaidia kutembea usiku. Inakuonyesha miiba na mashimo.

Lakini taa haiwezi kuchomoza jua. Jua linachomoza lenyewe.
Maneno meeeeeeeeeengi

Huyo Mungu wako anashindwa kuwalinda watoto dhidi ya watumishi wake!
 
Attachments

  • Screenshot_20260819-083007.png
    Screenshot_20260819-083007.png
    916.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom