Sawa, unasema energy inaweza kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine. Mfano chemical energy inaweza kubadilika kuwa heat, electrical energy inaweza kubadilika kuwa light na heat, na kinetic energy inaweza kubadilika kuwa heat. Sasa swali langu ni hili, ni wapi kwenye hiyo principle tunaona energy ikibadilika kuwa nafsi, consciousness au binadamu?
Kama unasema tulikuwepo milele kama energy, tulikuwa energy ya aina gani? Chemical, electrical, thermal, kinetic au energy gani hasa? Na ni process gani iliyofanya hiyo energy iwe consciousness na hatimaye iwe mimi na wewe?
Halafu umejuaje kwamba Mungu ndiye aliyefanya hiyo transformation? Energy kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ni fact tunayojua. Lakini kusema Mungu alibadilisha energy kuwa mwanadamu ni claim nyingine kabisa. Evidence ya hiyo connection iko wapi?
Na kama tulikuwepo milele kabla ya kuwa binadamu, Mungu alituumba kweli au alibadilisha tu kitu ambacho tayari kilikuwepo milele kuwa form nyingine? Hapo ndipo nataka unieleze vizuri.