johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,924
141,891
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameomba msamaha kwa Kanisa zima la KKKT, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo

Tukio lilikuwa mubashara KKKT Kinyerezi

Chanzo: Upendo TV


=====

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16, 2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”

Kuhusu kusimamishwa kwake, soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
 
Back
Top Bottom