Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Status
Not open for further replies.
huyo bwana ni askofu kweli? siku hizi ni ruksa mtu yeyote kujitanganza kuwa askofu. ana maslahi gani na dk slaa mpaka alaani kiasi hicho?
nijuavyo suala la ibada ni la mtu binafsi na mungu wake na dk slaa kama nafsi amefanya hivyo na familia yake; iwapendeze watu ama la.
 
Kila mtu askofu siku hizi. hivi ni
kanisa gani tena....?
 
Mh kwahiyo slaa ndo kakosea sana kuzidi mnaemualika kutoa misaada makanisani huku mkojua hela anazotoa ni za uwizi ? Kama ccm wameshindwa siasa wameamua kukutumieni wambie mshindwe na mlegee
 
Kwa kweli hata mimi nimemshangaa sana Dr Slaa.

CC; Josephine,

Mungu wa Israel anajipigania wala hahitaji watu kutoa povu humu, ni nani kati yenu ambaye hana dhambi awezaye kumnyooshea kidole Dr. Slaa. Au ninyi kwa vile dhambi zenu zimekuwa nyekundu kama bendela mnaogopa hata kwenda Israel ili muukwepe mkono wa Bwana! Mungu hana mipaka na wala huna sababu ya kushangaa, popote ulipo kama ukitenda dhambi bila kujali hadhi yako, dhambi hiyo lazima itakutafuna tu. Mwacheni Dr wa ukweli afanye vile Mungu atakavyo mwongoza.
 
Ajabu ya mtu alokuwa mtumishi wa Mungu , mchunga kondoo, anakwenda kuhiji na mtu aliezini nae mpaka wamepatikana watoto wa kitendo cha haramu ambacho hata kwenye kitabu kitukufu cha biblia kimekata "UZINI" "USIIBE" yeye aliewahi kuwa mchunga Kondoo Slaa akazini akazaa watoto, akaiba , na bado anakwenda kuhiji katika mji mtukufu, mji mtakatifu alozaliwa Yesu na mtu anaeendelea kuzini nae , KWELI NASTAAJABU
 
Ushamba unamsumbua huyo askofu , nani kamwambia Israel kila mtu anaenda kwenye Ibada, kinachoitwa kuHijj ni wazimu mtupu, wapi Biblia imeandika kuna kuhiji Israel, huo ni upagani.
Dr Slaa(PHD) amekwenda kutalii, na kutazama nchi hiyo byenye Historia pana kwa ustawi wa kidunia

ivi nyie watumikia matumbo kwanini hamuonagi aibu??? kwann unatetea uovu?? kwann mna ngozi ngumu hivi??? mnatia aibu, slaa sio mungu ana mapungufu huo wa uzinzi ndio moja ya mapungufu yake..
 
Mikakati ya kuua agenda ya mabomu ya Arusha.Issue nzito ile huwezi kuiua kirahisi hivyo
 
babu kashindwa kutokea madem na walivyo wengi hivi mpaka abebe mke wa mwenzie
 
Anayepokea ama kukataa maombi ni Mwenyezi Mungu pekee!
Huyo ndiye ajuaye yaliyo mioyoni mwa kila mmoja wetu! Whether tumeonekana machoni pa watu ama tukiwa sirini.
 
Kwani mtu anapotubu anatubu kwa Mungu au anatubu kwa wanadamu? Kwamba Slaa ametubu au hajatubu mtu mwingine anaweza juaje? Halafu kwani Slaa ni muumini wa hilo kanisa la Pentecost Church of God Emmanuel? Kama sio muumini wa kanisa hilo inamuhusu nini huyo askofu? Halafu jina la kanisa na lenyewe linatia dosari
 
Wakristo hatuna hija, hija ya Mkristo haiko kwenye jengo wala mlimani bali katika Roho na Kweli. Huyo askofu ni kipofu kama anadhani wakristo huenda Israel kwa ajili ya kutafuta utakatifu (kuhiji) naye pia amepotoka.
 
Dk Slaa najua upo hapa na unafatilia huu uzi kwa ukaribu.
Ebu toa kauli bhana,we si ndiye prezidar to be au???
 
Hata mi namshangaa sana slaa

Mi kila siku namchukia Babu kwasababu ya tabia yake ya uzinzi na na kulisaliti kanisa. Huyu Mzee ni mzinzi mkubwa tena anapaswa kulaaniwa hapa duniani na akhera. Amebilisi ndoa ya mtu na kumpora mke akitumia nafasi yake na fedha zake. Hivi wewe ukiporwa mkeo utajisikiaje?
 
Huyu bila shaka ni askofu wa Lowassa huyu.

Lowassa naye si alienda huko Israel na mke akaandika kitabu wakati ni fisadi mkuu,alisharudisha pesa za watanzania kabla hajaenda huko?
 
Askofuuuuuuuu! Kuna uhusiano gani wa moja kwa moja kati ya dini the so called askofu na hija Dr Slaa? Labda Slaa anamtazama nyoka wa shaba! Ondoa boriti lako kwanza...
 
Mi kila siku namchukia Babu kwasababu ya tabia yake ya uzinzi na na kulisaliti kanisa. Huyu Mzee ni mzinzi mkubwa tena anapaswa kulaaniwa hapa duniani na akhera. Amebilisi ndoa ya mtu na kumpora mke akitumia nafasi yake na fedha zake. Hivi wewe ukiporwa mkeo utajisikiaje?

We umezini na wangapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom