Naombeni msaada kwenye jambo langu na Bima ya afya

Naombeni msaada kwenye jambo langu na Bima ya afya

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
659
Reaction score
1,093
Salaam wakuu.
Nilifunga ndoa ya kanisani mwaka 2022,baadae nikawa na migogoro na mke wangu jambo liliopelekea kutengana. Bila kuvunja ndoa nikapata mwanamke mwingne nikazaa nae mtoto mwaka2023 na nikafunga nae ndoa ya serikali mwaka 2024. Wakati wa kusajili ndoa kwa mkuu wa wilaya niliulizwa nina mke mwingine nikajibu NDIO ninaye hivyo tangazo la ndoa na cheti cha ndoa vikaonesha ni ndoa ya wake wengi. Kupitia kile cheti cha ndoa ya serikali nikamkatia mke wangu bima ya afya ili imsaidie kwenye matibabu. Mwaka jana 2025,tukatafutana nayule mwanamke wa ndoa ya kanisani tukamaliza tofauti zetu na hatimae akaja kuishi namimi hadi leo tupo nae na anajua kuwa kuna ndoa nyingine nimefunga ila hana shida kwenye hilo. Ikumbukwe huyu mke wa pili kwasababu za kikazi siishi nae sehemu moja ila tunatembeleana tu inapopatikana nafasi.
Sasa msaada ninaomba kwenu ,huyu mwanamke niliyemkatia bima anapokea matibabu flani ya kiafya kwasasa.Juzi nimepigiwa simu na watu wabima wakauliza kuwa nina wake wangapi nikawajibu wawili na vyeti ninavyo.Mwisho wakasema niende na hivyo vyeti ofisini kwao ili waweke mambo sawa. Huyu mke wa kanisani sijamkatia bima na wala cheti cha ndoa sijakitumia popote pale.
Je, niko salama au kuna namna naweza kuonekana nimedanganya kwa kufunga ndoa mbili ?
Natanguliza shukrani
 
Samahani ungeitaja ni kampuni gani ya bima hiyo mana NHIF waliniambia hawana mfumo wa kutambua cheti cha ndoa, nikasajiri kila mtu kivyake
 
Kivyake kivp yaan??? Fafanua tupate ufahamu wengi
Samahani ungeitaja ni kampuni gani ya bima hiyo mana NHIF waliniambia hawana mfumo wa kutambua cheti cha ndoa, nikasajiri kila mtu kivyake
 
Samahani ungeitaja ni kampuni gani ya bima hiyo mana NHIF waliniambia hawana mfumo wa kutambua cheti cha ndoa, nikasajiri kila mtu kivyake
NHIF mkuu.Nyaraka muhimu waliyohitaji ni cheti ch ndoa
 
Back
Top Bottom