Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Status
Not open for further replies.

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
7,113
Reaction score
950
Askofu wa kanisa la pentecost Church Of God Emmanuel Mwamakula.amelaani kitendo cha katibu mkuu wa CHADEMA bwana W.Slaa kwenda kufanya idaba ya hijja nchini israel na mwanamke hajafunga nae ndoa. Slaa aliondoka nchini feb 24 mwaka huu akiwa na mtu aliyemtambulisha kama mchumba wake na ambaye amekiri kuzaa nae mtoto,Josephene Mushumbusi kwa ndege no QR 545 kwa ajiri ya kwenda kutimiza ibada hiyo ambayo yeye anadai ni ya kuliombea taifa.

Akizungumza na gazeti hili Askofu Mwamakula alisema ameshangazwa na kitendo cha Slaa kuwa ujasiri wa kwenda kufanya idaba hiyo takatifu na mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa(hawara). Hiki alichofanya Slaa kinapaswa kukemewa na kulaaniwa vikali,haiwezekani mtu akamchukua mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa na kuambatana nae kwenda sehemu takatifu ambako ni mbele za mungu na kufanya ibada,huu ni 'uchafu' uliopitiliza,alisema askofu huyo.

Aliendelea kusema kwamba Slaa alipaswa kwanza kutubu kwa kitendo chake cha kupora mke wa mtu na kuzaa naye wakati anajua wazi kufanya ni kutenda zinaa,kwani kwenye maandiko matakatifu imewekwa wazi kwamba mwanamke au mwanaume anayemuacha mume au mke wake na kwenda kwa mwingine anazini.

Slaa amewahi kuwa padre wa kanisa katoliki anajua maandiko kwamba ndoa ya kikristo inapofungwa,kinachotenganisha ni kifo tuu!lakini kinachoshangaza yeye amepora mke wa mtu na kwenda nae sehemu takatifu bila aibu. Ninasema ni kwamba,Slaa alipaswa kwanza kutubu na kutumia nafasi hiyo kuomba mungu amuepushe na adhabu kali ikizingatia umri wake amesonga sana.

Lakini yeye anaona fahari kufanya matendo ambayo hayaendani na umri wake na kibaya zaidi ni matendo yanayokwenda kinyume na dini yetu.Alisema Askofu huyo kutoka Mbeya. Slaa amekwenda Mbeya kutembea tu,hana usafi wa kutosha kuliombea taifa wakati yeye ndiye alipaswa kuombewa kwanza kutokana na dhambi nzito ya uzinifu inayomkabili!

Hata hivyo,uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa,katika kuficha uhusiano wake huo na mchumba wake huyo(Josephine Mshumbusi) kwenye orodha ya wasafiri ambayo mwandishi wa habari hii ameiona,Slaa akiwa namba 70,mchumba wake huyo amejitambulisha kama mke wa Aminiel Mahimbo na sii mchumba wa Slaa.

Chanzo: Africa Leo toleo no 72.
 
Kwa kweli hii Tz watu wanakosa weledi na maono nyie wananchi wamezalilishwa hadi wanajifungulia sakafuni kwa sababu tuu ya mafisadi wachache wanaficha hela zetu. Elimu imekufa hospitals mbovu. Watu wanafanya biashara za madawa ya kulevya hadi wengine wanakamatwa China na kupelekea nchi yetu kuwekwa rehani bado hamlioni hilo mnahangaika na maisha ya mtu mmoja. UMEPOTEA
 
AFRICA LEO ndio gazeti gani hili..linapatikanata nchi gani?
 

[TD="bgcolor: #ffffff"] MAHAKAMA ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na mume wa zamani wa Josephine Mushumbusi, Eminiel Mahimbo, baada ya kubaini kuwa haikuwa na msingi wowote kisheria.
Josephine Mushumbuzi kwa sasa ni mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.


Mahimbo alikata rufaa kupinga hukumu ya mahakama ya mwanzo Sinza ambayo ilivunja ndoa hiyo.


Rufaa hiyo ilifutwa jana na Hakimu Aniseth Wambura ambaye alisema kuwa mahakama hiyo inakubaliana na hukumu iliyotolewa na mahakama ya mwanzo.
Alisema mahakama inakubaliana na hukumu hiyo iliyotolewa Aprili mwaka jana katika kesi ya madai ya talaka iliyofunguliwa na Josephine anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Philemon Mutakyamilwa.


Katika uamuzi wake huo, mahakama hiyo ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwa sababu Mahimbo hakuwa mwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.


"Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa, mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Josephine kwamba kwa tabia ya kutokuwa mwaminifu hapakuwepo na ndoa baina yao, hivyo hukumu ya mahakama ya mwanzo Sinza ilikuwa sahihi," alisema Hakimu Wambura.
Akizungumza na Tanzania Daima jana baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki kwa sababu kesi hiyo ilikuwa na msukumo wa kisiasa uliokuwa na lengo la kumchafulia jina mteja wake, Josephine.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
.... tanzania daima...ijumaa, 24 mei 2013...


Josephine Mshumbuzi amshinda mtalaka wake



na Happiness Katabazi



[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff, align: center"]
[/TD]
[/TD]
 
Mh haya mambo naona kama hayatuhusu sana........ila sishangai kwa Tanzania ya leo ya kila mtu anayetaka kutokea kwa mgongo wa mwenzake........
 
Huyo askofu ndiye mtoa hukumu kwa wanadamu, ashindwe ktk jina la yesu hukumu itatolewa siku ya mwisho atakaporudi yesu.
Yeye matendo yake amejichunguza ?
 
Ushamba unamsumbua huyo askofu , nani kamwambia Israel kila mtu anaenda kwenye Ibada, kinachoitwa kuHijj ni wazimu mtupu, wapi Biblia imeandika kuna kuhiji Israel, huo ni upagani.
Dr Slaa(PHD) amekwenda kutalii, na kutazama nchi hiyo byenye Historia pana kwa ustawi wa kidunia
 
Maaskofu wa mitaani! Hawasiti kuhukumu!! hayo ni mashetani ya duniani and their role is to curse every human being and the world. Huwezi kumsikia Askofu kama huyo anaona mazuri kwa binadamu mwenzake kwa sababu kazi yake kama ilivyo ya mpinga kristo ni kuhukumu na kuhakikisha analaani Dunia ili apate wafuasi huko nyumbani kwao Jehanam! Poor bishop! poor followers of Antichrist unknowingly!! We are surrendering you under the cross of Jesus and we are covering you with the precious blood that healed the world!
 
Maaskofu wa mitaani! Hawasiti kuhukumu!! hayo ni mashetani ya duniani and their role is to curse every human being and the world. Huwezi kumsikia Askofu kama huyo anaona mazuri kwa binadamu mwenzake kwa sababu kazi yake kama ilivyo ya mpinga kristo ni kuhukumu na kuhakikisha analaani Dunia ili apate wafuasi huko nyumbani kwao Jehanam! Poor bishop! poor followers of Antichrist unknowingly!! We are surrendering you under the cross of Jesus and we are covering you with the precious blood that healed the world!

jamani tuache ubishi. hivi dr slaa hazini kweli? au hatujui maana ya uzinifu
 
kwa Yeyote aliye msafi na asimame ampige mwanamke huyu jiwe!!
 
Huyo askofu ndiye mtoa hukumu kwa wanadamu, ashindwe ktk jina la yesu hukumu itatolewa siku ya mwisho atakaporudi yesu.
Yeye matendo yake amejichunguza ?

kumbuka yeye ameongea kama kiongozi wa kiroho na anapaswa kuongea kweli tupu na ndivyo alivyofanya
 
Vyanzo vingine vya habari kaaaazi kweli kweli! Eti makanisa mengine nayo yana Askofu! Huyu Emmanuel Mwamakula mwenyewe kila uchao anashinda na wanawake za watu huku akijifanya anawaombea. Sijui uaskofu mwingine unatoka wapi!

Eti kwa kuficha wasijulikane wanasafiri pamoja mchumba wake Dr Slaa amejitambulisha kama mke wa Aminiel Mahimbo. Unajuaje kama hati yake ya kusafiria hajaibadilisha jina?

Hivi mtu apeleke shauri mahakamani na kushinda kesi na bado aendelee kujificha, inaingia akilini kweli? Mwambieni huyo askofu njaa kwamba akawahubirie wanao muamini yeye lakini sio sisis waTanganyika tunao ipigania haki na usawa katika taifa hili.

NA ALAANIWE YEYE NA HAO WANAO MUAMINI. Laana Kumu kabisa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom