Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Askofu ambomoa Dk. Slaa, amuonya na dhambi ya uzinzi!

Status
Not open for further replies.
sasa unamuuliza nani?? Wacheni umbea watoto wakiume kuna mambo mengi ya kuzungumzia kuhusu nchi yetu sio huu upuuzi

ndo tunamjadili raisi wetu mtarajiwa.......
kwenye ukweli inabidi kuongea sasa miaka
yooooote hiyo anaishigi na mchumba tu
 
Tata Mwita Maranya, zamani ukienda kanisani unakumbana na uwepo wa Roho Mtakatifu, lakini sasa kuna homa imeingia mjini na haya makanisa ya kina Mwama-Kula, wana Roho Mtakavitu.

Sijui yeye anayo orodha ya watu wote waliotubu mwaka huu au!
 
Last edited by a moderator:
Kila mara posts kama hizi ndizo zinazo nisababishia ban!

For sure nikichangia uzi huu kura ban!

Ila ipo siku yako utaingia kwenye 18 na utajuta kuzaliwa!
 
Asimshangae sana maana kashfa za SLAA ni kubwa sana na siku tukiamua kuzimwaga zote hapa jamvini ATAAIBIKA sana!
 
kwani hawa yani slaa na josehin wanamdanganya mungu au wanamdanganya binadamu?
 
baba mch.utapiga makofi sanaaa kanisani.lakini njaa hazitakuisha..wanaomwaabudu mungu wa kweli hawasemisemi hovyo.
 
ASKOFU mwenyewe huenda ni mtoto aliyepatikana kwa zinaa ni NANI ajuaye? NDOA za washirika wake wote zikoje kanisani kwake? Namshauri Askofu ALITUMIE NENO LA MUNGU KWA HALALI AACHE KUJIPENDEKEZA NA KUTUMIWA NA WANASIASA HASA CCM.
 
Nina uhakika DR W Slaa atalitolea ufafanuzi hili. Labda alishafunga ndoa lakini haikutangazwa!

Kuna baadhi ya mambo ukikosa kuyafanya utotoni, ukiyakutia ukubwani huwa yanaleta taabu saana! Wakubwa mmenielewa!

cc: Mwita Maranya
 
pentecoste church of god emanuel, ndio kanisa gani?.

kwanza huyo askofu mpotoshaji ni nani alimwambia slaa alienda kuhiji? Mtu asitembelee historical event? Au kwa uelewa wake mtu akienda islael ni kuhiji? Jamani hawa kenge tuweni makini nao wanatuamisha arusha kwenye mabomu
 
Askofu wa kanisa la pentecost Church Of God Emmanuel Mwamakula.amelaani kitendo cha katibu mkuu wa CHADEMA bwana W.Slaa kwenda kufanya idaba ya hijja nchini israel na mwanamke hajafunga nae ndoa. Slaa aliondoka nchini feb 24 mwaka huu akiwa na mtu aliyemtambulisha kama mchumba wake na ambaye amekiri kuzaa nae mtoto,Josephene Mushumbusi kwa ndege no QR 545 kwa ajiri ya kwenda kutimiza ibada hiyo ambayo yeye anadai ni ya kuliombea taifa.

Akizungumza na gazeti hili Askofu Mwamakula alisema ameshangazwa na kitendo cha Slaa kuwa ujasiri wa kwenda kufanya idaba hiyo takatifu na mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa(hawara). Hiki alichofanya Slaa kinapaswa kukemewa na kulaaniwa vikali,haiwezekani mtu akamchukua mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa na kuambatana nae kwenda sehemu takatifu ambako ni mbele za mungu na kufanya ibada,huu ni 'uchafu' uliopitiliza,alisema askofu huyo.

Aliendelea kusema kwamba Slaa alipaswa kwanza kutubu kwa kitendo chake cha kupora mke wa mtu na kuzaa naye wakati anajua wazi kufanya ni kutenda zinaa,kwani kwenye maandiko matakatifu imewekwa wazi kwamba mwanamke au mwanaume anayemuacha mume au mke wake na kwenda kwa mwingine anazini.

Slaa amewahi kuwa padre wa kanisa katoliki anajua maandiko kwamba ndoa ya kikristo inapofungwa,kinachotenganisha ni kifo tuu!lakini kinachoshangaza yeye amepora mke wa mtu na kwenda nae sehemu takatifu bila aibu. Ninasema ni kwamba,Slaa alipaswa kwanza kutubu na kutumia nafasi hiyo kuomba mungu amuepushe na adhabu kali ikizingatia umri wake amesonga sana.

Lakini yeye anaona fahari kufanya matendo ambayo hayaendani na umri wake na kibaya zaidi ni matendo yanayokwenda kinyume na dini yetu.Alisema Askofu huyo kutoka Mbeya. Slaa amekwenda Mbeya kutembea tu,hana usafi wa kutosha kuliombea taifa wakati yeye ndiye alipaswa kuombewa kwanza kutokana na dhambi nzito ya uzinifu inayomkabili!

Hata hivyo,uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa,katika kuficha uhusiano wake huo na mchumba wake huyo(Josephine Mshumbusi) kwenye orodha ya wasafiri ambayo mwandishi wa habari hii ameiona,Slaa akiwa namba 70,mchumba wake huyo amejitambulisha kama mke wa Aminiel Mahimbo na sii mchumba wa Slaa.

Chanzo:Africa Leo toleo no 72.

pole sana baba askofu ,Pitia tena canon law, jaribu kusoma vitabu vya agano jipya.
Nahitaji kujua Mungu huyo unaye muongelea kama anahangaika na hicho unachotaka kutuaminishisha .
Sijaelewa kama amani ya taifa huombewa Kwa mtido huo.
madhabahu inakazi ya kusafisha nasio vinginevyo.
usafi na utakatifu ni process .An endless effort .

baba askofu , Nia pamoja na dhamira Safi utapimaje baba askofu ukiwa kwenye kiti cha uaskofu?(UASKOFU ni chombo cha hapa duniani, kinaanzia duniani na kuishia duniani )

Ndoa Safi na Ndoa iliyokataliwa na Farao utaiwekaje kwenye mizani ya Mungu .
Sio ajabu unataka kutakasa wewe na Mungu je atafanya nini? basi wewe baba askofu unakalia utakaso na wewe tukuite mungu na sio Mungu.
soma amri ya kwanza inasemaje .
Nasikitika kwenye hili soma sijakuelewa baba .
 
Mwamakula ndiyeMungu mwenye kuhukumu, hawa watu wanataka waabudiwe wakijibebesha utakatifu ambao hawana. Israel ni nchi tu ndy maana hata maeneo mhim yamechukuliwa na watu wa imani nyingine tunamwabudu Mungu Tukiwa ndani ya Roho wa Mungu na kweli ya neno lake ndiyo maana ROHO NA KWELI Akutane na Dr, Slaa amshauri siyo kupayuka imani za kifalisayo
 
Nani kamwambia Israel wanaenda waliofunga ndoa au watu wasafi tu?!!!!!!!!
 
umri wake umeenda ya nini hadi leo hajaoa!!!!!!
ni kipi kinachomzuia kuoa!!!!!!!
dkt+slaa3.jpg



........ivi ni kwa nini hasa haoi..

nafurahi kuona mambo ya msingi siasa iko pembeni..
 
kama d.slaa hajaowa hapo hapana tatizo koz nimaisha ya mtu binafsi.lakini anachukuwa wake za watu hapo amelaniwa na mashetani ya ngono yamemzidi.ila siwezi kushangazwa kwasababu hawa jamaa wamezoea kuchukua wake za watu.mimi nazani wapewe ruhusa ya kuoa.d.slaa ifikapo mwaka 2015 kama hujaowa kura yangu hutoipata kwasababu nikikupa kura na ukiinga ikulu utaendekeza umlaya zaid kuliko shughuli za maendeleyo
 
Tofauti ya ukristu na dini nyinginezo, Mungu wetu yuko mahali pote. Hizo ziara za Israeli ni za kihistiria zaidi na hazichagui nani aende na nani asiende.
 
Mh hana hata chembe ya Aibu huyu kiumbe

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Toa boliti lililoko machoni kwako kabla ya kunyooshea kidole kibanzi kilichopo jichoni kwa mwenzio

POINT.....Babu aangalie sana mwenendo wake kabla ya kupanda jukwaani na kuita wengine wezi na mafisadi ili hali ruzuku tu inamtoa denda.

Na aache mara moja kujitapa eti anataka kuwakomboa watanzania ili hali yeye mwenyewe anashindwa kujikomboa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom