Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Watangazaji wakawa wanafananisha red ya yule dogo wa liva jones baada ya kumchezea rafu Bissouma na Kovacic alichofanya jana baada ya yellow ya kwanza.

Binafsi niliamini Kovacic hastahili kubaki baada ya ule mchezo alioufanya.

Wakati Tomi anampelekea mpira Kai nilisimama nikijua Kai anaunga ule mpira, mpaka unafika kwa Kai Ake akawa kashafika akili ya haraka ikaniambia Kai atajaribu kubody feint na kuscore.

Instead akachagua the simple solution he could see. Akamrudishia sub mwenzake Martinelli. Wakati Martinelli anausogelea mpira, Tomiyasu akawa anapisha njiani, mtangazaji akaita "Martinelliiiiii" mimi muda huo nishasema "Kai vipi tena hapo".

Martinelli anakuja na sasa hivi naamini anaitafuta angle kwa kupiga ndizi. Ake, beki tuliyeambiwa amekuja kumfunika Saka, yeye hakutoka njiani. Ile ndizi ikatua kwake na mpira ukawa wavuni.

Jinsi tumecheza kutotaka kujibizana nao kumesababisha Haaland aonekane wa kawaida, jana au juzi kuna member tukiwa tunaongelea finishing ya Nketiah nikamuambia in terms of finishing and consistency ya conversion Nketiah ndiye top kwa Arsenal.

Na asiposcore utamuona miyeyusho coz huko kwingine ni mbovu. Haaland hajascore na mashabiki wa City wanamuona miyeyusho, lakini ni lini Haaland ameoffer kitu zaidi ya kuscore consistently?

Wiki nzima tunaambiwa Ben atakiona cha moto akikutana na Doku. Doku akaingia na Ben akampiga tobo jamaa na jamaa hajafurukuta hata kidogo.

Tulivyocheza na liva msimu uliopita % kubwa tuliamini we have a chance mara zote 2 nafikiri mpaka msimu ujao tutakua na imani hiyo dhidi ya City pia.

Yule jamaa aliyedai kwamba atajitoa JF nasikia JF wenyewe ukiripoti wanamban
 
Usijidanganye sana Arsenal ya msimu huu kuna utofauti ukilinganisha na msimu uliopita kuanzia squad depth na upambanaji na bado tutasajili tena january aisee msimu huu tutaona mafanikio Zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yan game ya jana mzee yan team inaanza tu

Martinell Off

Saka Off

Partey Off

Tommy Off

Kai Off

Alfu pila lilipigwa vile sio kitu kidogo aisee
 
Mwanzo ulidai tukipata injury ya Saka ulivyoona Jesus kafanya kitu ambacho hakuna aliyemmis Saka ule upande umeamia kwa Jesus,
Pambana na Nyumbu kwanza nafasi ya 13 uko
 
Lile tobo la White kwa doku uliliona?
 
Mimi wote siwakubali, ila naona Kai alichomzidi Eddie ni urefu tu. Pia supendi jinsi jamaa hana Nia ya kuprogress mipira Kwa mbele. Hata akiwa most advanced na amepewa long ball na Raya akabeat offside trap Bado atageuka na kurudisha mpira nyuma mpaka urudi Kwa Raya tena. Kai Bado ana kazi ya kujifunza mpira, siyo tu mpira wetu, bali mpira tu in general Kwa position tunayotaka acheze, ndiyo nitaanza kuona faida yake
 
Unasemaje?
 
Manchester city jana tulitakiwa kucheza nao 2nd half nzima wakiwa 10 uwanjani ila walibebwa na marefa waliokataa kumpa Kovacic kadi ya njano ya pili. Ile mechi ingechezeshwa fairly, wangekula 3 wale.
 
Milangomitatu aliibuka jana akitarajia tupoteze, kapotea hana wa kumtupia lawama
 
Yan game ya jana mzee yan team inaanza tu

Martinell Off

Saka Off

Partey Off

Tommy Off

Kai Off

Alfu pila lilipigwa vile sio kitu kidogo aisee
😆😆 hapo Kai umemuongeza tu ila hata asingekuwepo hakuna ambaye angelalamika. Ila Tomi jana sijui aliingia kucheza kama beki ama forward maana nakumbuka kumuona mbele tu anafanya machambulizi ila sikumnbuki kumuona nyuma akikaba
 
[emoji38][emoji38] hapo Kai umemuongeza tu ila hata asingekuwepo hakuna ambaye angelalamika. Ila Tomi jana sijui aliingia kucheza kama beki ama forward maana nakumbuka kumuona mbele tu anafanya machambulizi ila sikumnbuki kumuona nyuma akikaba
Arteta anasema alipoona Pep kamuingiza Doku upande wa Zinny akamleta Tomiyasu kumkabili, ila alipohamia upande wa White akampa Tomi majukumu ya kwenda mbele
 
Me nimesema Nketiah Hana finishing ya kustaajabisha, anaachwa mbali sana na Trossard. Hata Chamack alikua anafunga

Kuna chance aliipata akapiga off target, ile angeipata mtu kama Trossard tungekuwa tunaongea mengine sasa hivi. Kuna move nyingine alikuwa na odegard, Odegard alijua jamaa ameotea akawa anauwahi mpira, Nketiah naye kauwahi ikawa offside (ameua shambulizi)

Kitu ambacho nadhani kamzidi Trossard labda nguvu tu. Lakini pia Nketiah siku hizi namuona anawahi sana kuchoka tofauti na game za nyuma kidogo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…