EPL yarudi kwa kishindo: Arsenal yaanza utetezi wake leo

EPL yarudi kwa kishindo: Arsenal yaanza utetezi wake leo

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Ligi Kuu England (Premier League) 2026/27 inaanza rasmi leo, Ijumaa Agosti 21, huku mabingwa watetezi Arsenal wakifungua msimu dhidi ya Coventry City kwenye Uwanja wa Emirates.

Mchezo huo unatarajiwa kufungua msimu wenye ushindani mkubwa, huku Arsenal ikilenga kutetea taji lake dhidi ya wapinzani wakubwa kama Manchester City, Liverpool, Manchester United na Chelsea.

Baada ya mchezo wa ufunguzi wa Arsenal dhidi ya Coventry, ratiba ya wikendi itaendelea Jumamosi na Jumapili, huku baadhi ya michezo inayotarajiwa kuvuta hisia ikiwa ni Hull City dhidi ya Manchester United, Brentford dhidi ya Tottenham, na Newcastle United dhidi ya Liverpool.

Kwa mashabiki wa soka, msimu wa 2026/27 unaahidi ushindani mkubwa kuanzia siku ya kwanza, huku swali kubwa likiwa kama Arsenal itaweza kutetea taji lake au mmoja wa wapinzani wake wakubwa atafanikiwa kulichukua mwishoni mwa msimu.

1787303884338.png
 
Back
Top Bottom