Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
1.nipo na jirani yangu mpaka leo hata jina langu hanijui japo amehangaika mpaka basi kunizoea coz naweza shinda siku 2 nzima nisitoke nje kwa weekend

2.Sipendi watu totally na hata ukinipigia simu ikifika dakika 2 nzima hujataja sababu ya kunipigia nakata zangu simu.

3,naweza kukaa na njaa hata siku nzima ila kamwe siwezi kuomba kwa mtu hata kama nina njaa ya kufa.
 
Ina maana prediction ilisema wewe kwa uelekeo wako wa extroversion tunategemea kidole gumba cha juu kilichofunika kiwe cha KULIA ila majibu yapo tofauti. Sio mbaya data kadhaa kwenda tofauti tukipata majibu mengine tutathibitisha kama kuna uhusiano wa asilimia kadhaa au la.

Bado kura zinaendelea jamani naomba mreply post 90 au 104 mniambie mkiweka vidole kama picha hizo kidole gumba cha mkono upi kinawafunika wenzie wote juu?
Cha kulia.
 
Cha kulia kipo juu ya vingine.
Asante, umeweka just as predicted wacha niupdate data hapa ntaleta matokeo.

Wewe ufikiri wako unaanzia kulia kwenda kushoto katika ubongo wako na ndiyo maana unaona ni confortable zaidi kuishi kama unavyoishi🤭
 
Cha kulia.
Asante kwa majibu

Kukamilisha utafiti tupatie na data ya kuonesha upo ki extrovert zaidi?[kinyume na mtoa mada] au upo kiintrovert zaid [sambamba na mtoa mada]

Prediction kwako inakuwa ni extrovert, naomba thibitisha au pinga ili nirekodi hapa
 
Cha kushoto kipo juu ya vingin
Asante kwa majibu

Kukamilisha utafiti tupatie na data ya kuonesha upo ki extrovert zaidi?[kinyume na mtoa mada] au upo kiintrovert zaid [sambamba na mtoa mada]

Prediction kwako inakuwa ni introvert, naomba thibitisha au pinga ili nirekodi hapa
 
Asante kwa majibu

Kukamilisha utafiti tupatie na data ya kuonesha upo ki extrovert zaidi?[kinyume na mtoa mada] au upo kiintrovert zaid [sambamba na mtoa mada]

Prediction kwako inakuwa ni extrovert, naomba thibitisha au pinga ili nirekodi hapa
Watu ambao hawanijui wanasema siongei sana,wanaonijua wanasema naongea sana/mchangamfu kishenzi.Najichanganya Sana na watu lkn Kuna Muda hua nataka kua mwenyewe kwa kipindi flani hata mawasiliano ya Simu hua nayapotezea.Starehe zote nafanya tena nikiwa na nyomi ya watu lkn vitu Kama harusi/sherehe sipendelei.Nadhani nafiti zaidi kwny Extrovert mkuu.
 
Asante kwa majibu

Kukamilisha utafiti tupatie na data ya kuonesha upo ki extrovert zaidi?[kinyume na mtoa mada] au upo kiintrovert zaid [sambamba na mtoa mada]

Prediction kwako inakuwa ni extrovert, naomba thibitisha au pinga ili nirekodi hapa
Sijajua sifa za extrovert. Mimi sipendi kuongea na simu, napenda ku chat. Naongea tena kwa kujiamini, nikiamua. Mara nyingi napenda kusikiliza na kukaa kimya. Sipendi mazoea ya hovyo na watu wengi. Sina rafiki ila nipo peace na watu wote.
 
Watu ambao hawanijui wanasema siongei sana,wanaonijua wanasema naongea/mchangamfu kishenzi.Najichanganya Sana na watu lkn Kuna Muda hua nataka kua mwenyewe kwa kipindi flani hata mawasiliano ya Simu hua nayapotezea.Starehe zote nafanya tena nikiwa na nyomi ya watu lkn vitu Kama harusi/sherehe sipendelei.Nadhani nafiti zaidi kwny Extrovert mkuu.
Asante, just as predicted😊

Unapendelea zaidi kuyachakata mambo kichwani kutokea kulia kwenda kushoto
 
Sijajua sifa za extrovert. Mimi sipendi kuongea na simu, napenda ku chat. Naongea tena kwa kujiamini, nikiamua. Mara nyingi napenda kusikiliza na kukaa kimya. Sipendi mazoea ya hovyo na watu wengi. Sina rafiki ila nipo peace na watu wote.
Kutokana na hiyo kauli tunasema ni introvert

Na ndiyo prediction inavyosema wewe bro ubongoni mwako unayachakata mambo kuanzia kushoto kuelekea kulia👊.

Hivyo namna unavyoishi ndiyo confortable zaidi kwako
 
Asante, just as predicted😊

Unapendelea zaidi kuyachakata mambo kichwani kutokea kulia kwenda kushoto
Hahah kesho nitafanya zoezi Hilo kwa watu ninaowajua then nitazidi kupata majibu sahihi zaidi.

Ila hapo kwny kuchakata Mambo kichwani kutokea kulia kwenda kushoto ndio sielewi hata 😄😄😄
 
Kutokana na hiyo kauli tunasema ni introvert

Na ndiyo prediction inavyosema wewe bro ubongoni mwako unayachakata mambo kuanzia kushoto kuelekea kulia[emoji109].

Hivyo namna unavyoishi ndiyo confortable zaidi kwako
Ila hapo juu prediction yako ilisema mimi ni extrovert!
 
Data hizo mbili za obrien daniels na @ wa kupuliza zinatufikisha hapa.

Idadi ya kura 11, zilizoendana 10

10/11*100 = 90.1%

Nadharia ya kwamba maisha tunayochagua na kuyaona confortable whether kuwa introverted au extroverted zaidi yanatokana na ufikiri wetu [ambao dalili ya nje ni hiyo experiment ya uwekaji wa vidole]imekubalika kwa 90.1%
 
Ila hapo juu prediction yako ilisema mimi ni extrovert!
Sasa hapa naomba tuaminiane, ukisoma hizo meseji/reply mbili nilijibu nikakopi na kupaste nikasahau kubadili[nishabadili tayari kabla hata hujatuma hii meseji] kuandika kwako introvert.

Ili kuthibitisha ni makosa/error za harakaharaka tazama: haimake sense nimwambie aliyesema kulia ni extrovert na wewe tena ulosema kushoto tena extrovert. KUSHOTO=Introvert na KULIA[L]=Extrovert
 
Hahah kesho nitafanya zoezi Hilo kwa watu ninaowajua then nitazidi kupata majibu sahihi zaidi.

Ila hapo kwny kuchakata Mambo kichwani kutokea kulia kwenda kushoto ndio sielewi hata 😄😄😄
Hii explanation yake inatokana na kitu fulani wanabaiolojia wengine wanakikubali, wengine wanakataa.

Suala la kuwepo kwa ubongo wa kulia na ubongo wa kushoto

Ni kwamba wote tunazitumia pande zote mbili, ubongo mzima kuchakata taarifa na kufanya maamuzi

Ubongo wa kushoto una logics na mahesabu mengi[black and white zaidi] wakati ubongo wa kulia una ubunifu na hisia na [marangirangi mengi]

So ile hali ya kuvibe na kuflow na vitu ipo zaidi kulia na anayefikiria kuanzia kulia atatumia sana hii kwenye maamuzi ya harakaharaka so anajikuta outgoing. Inakuwa ni kama maji yanapokuwa mengi ndiyo unaflow nayo vizuri zaidi. Au rangi zinapokuwa nyingi ndiyo ubunifu unaongezeka. In short wanapenda kuvibe/kuparty flan ivi

Lakini huku kushoto kunakuwaga na kuchakata sana details na facts na malogic sasa unakuta huyu mtu kwanza ukimuoverload mambo/watu mengi inakuwa usumbufu. So anayefikiria kuanzia upande huu atapenda mazingira yenye vichache vya kuchakata ili achakate kwa raha. Anapata vingi vya kufanya kazi katika vichache vinavyomzunguka- Details

Mwisho mwishoni unakuta hawa watu wanakuwa na ka mtiririko fulani/continuuum inayoegemea upande anaoufavour zaidi. Anaojihisi confortable nao zaidi kulingana na yeye.

Kama ambavyo huwezi kumfosi mtu mwingine kwamba kuweka hicho kidole cha kulia tu, au kushoto tu ndio confortable way, ndivyo ambavyo hutakiwi kumfosi mtu kwamba kuwa na watu wengi au wachache ndio confortable way. Kila mmoja anaona vile anavyoona. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa jinsi mbalimbali ili tutumikiane na tukamilishane hapa duniani✌

Hint: Maelezo nahisi yanachanganya zaidi ili uchanganyikiwe na wewe ukatafute taarifa zaidi. 'I believe the process of going from confusion to understanding is a precious, even emotional, experience that can be the foundation of self-confidence.- Brian Greene
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom