Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Vivi, ulifanikiwa kujaribia watu engine?

Na vipi waliendana/kutokuendana na tabia zao Kwa asilimia Kama ngapi?

So umeona kuna uhusiano? au ni tunabahatisha tu? maoni yako tafadhali
Mpk J3 nitakua nimeleta feedback hapa mkuu.
 
Ni unaweka mkono hivi halafu unaangalia kidole gumba kilicho juu ya vingine ni cha upande gani. Ni cha mkono wa kusoto ama KULIA? simple

Fanya chap halafu naomba jibu lako brother
Mimi kwangu ni cha kushoto

Haya lete maneno sasa
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hata mimi ni hivyo hivyo ila kwenye tv Huwa napenda Habari,majadiliano basi..

Mziki ni ule niliouchagua mwenyewe..

Mimi hata kujinyenyekesha kwa Mwanamke Kisa nataka k huwa siwezi kabisaa yaani demu aoneshe any sign ya dharau sijui kutaka kujibebisha saana huwa siwezi endelea nae..
 
Mi ntaweza kukaa hata mwezi usijue Kama nipo au mwaka mzima nisiende mtaa wa pili Mimi kazini nyumbani nisikilize mziki masaa yote mi na simu nichat niwasiliane na watu saa sijui ndo mnaitaje hii
Kwa kuwa sinywi pombe wala sipendi mambo ya kuchangamana Sana basi hupenda sana vacations kama ndio starehe yangu..

Kama sina ishu naweza funga safari nikaanza kuzunguka Mji maeneo mbalimbali au nikasafiri Mji mwingine basi husikia raha Sana.😂😂
 
Kwa Hali inavyoenda mtakuja kubadilika mpaka mjishangae! Baadhi yenu ndo wale waliokuwa wakiponda watu mawe kule Arumeru ati mwajiita mizimu..[emoji23]
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Unataka ukawatest mtakaoparty nao weekend hii nini mzeebaba!?[emoji23][emoji23]
Daah mkuu mimi sijui nina shida gani Nina ego sana na hasira za karibu

Hapa nilipopanga sisalimii mtu niko mimi tu na mambo yangu kuingia na kutoka

Sasa leo natoka nikavuka wamama wawili wanafua nikajibanza sehemu nikawasikia wanaanza kunisema sisalimii mtu kabisa wakanisema weeh

Nikarudi nikawafata nikaanza kuwaashia moto nikawaambia salamu hailazimishwi

Mmoja akaanza kusema unajua sisi sote ni binadamu blah blah nyingi

Nikamwambia salamu hailazimishwi nikasepa zangu
 
Mimi kwangu ni cha kushoto

Haya lete maneno sasa
Ni wewe kujikagua na kupima kama je upo extroverted zaidi? au introverted zaidi ndiyo tuikusanye hiyo data kama imekubali au imekataa. Tunaomba jibu......

Lakini kama umeweka kushoto nadharia etu inasema kwa asilimia kubwa unafikiri tokea kushoto kwenda kulia..... hivyo utafavour tabia za kiintrovert

Tunaomba uconfirm kama hilo ni sahihi au la?
 
Daah mkuu mimi sijui nina shida gani Nina ego sana na hasira za karibu

Hapa nilipopanga sisalimii mtu niko mimi tu na mambo yangu kuingia na kutoka

Sasa leo natoka nikavuka wamama wawili wanafua nikajibanza sehemu nikawasikia wanaanza kunisema sisalimii mtu kabisa wakanisema weeh

Nikarudi nikawafata nikaanza kuwaashia moto nikawaambia salamu hailazimishwi

Mmoja akaanza kusema unajua sisi sote ni binadamu blah blah nyingi

Nikamwambia salamu hailazimishwi nikasepa zangu
Wahuni wote peponi 😂😂😂😂

Mi mtindo wangu ni huwa nawaangalia machoni nikiwa napita hivi..... akiniangalia namsalimia vizuri mnoo.

Asiponiangalia najisemeaga tu moyoni najiambia 'kuwa na heshima, heshimu maamuzi yake ya kutotaka kukuona wala kuinteract na wewe' basi na mi napita kimyakimya.

Nachukuliaga ndo heshima eti, ivi kwa mfano kung'ang'ania kumsalimia mtu anayeongea na simu ni heshima? au si-heshima? anayechati je??
 
Ni wewe kujikagua na kupima kama je upo extroverted zaidi? au introverted zaidi ndiyo tuikusanye hiyo data kama imekubali au imekataa. Tunaomba jibu......

Lakini kama umeweka kushoto nadharia etu inasema kwa asilimia kubwa unafikiri tokea kushoto kwenda kulia..... hivyo utafavour tabia za kiintrovert

Tunaomba uconfirm kama hilo ni sahihi au la?
Kwanza kabisa mimi sitofautiani sana na mtoa mada ila kwa kuongezea ni mtu wa movies na mziki kwa sana bila kusahau kuperuzi mitandaoni katika kujifunza mambo mapya nisiyoyafahamu...

Yaani siyo type za watu wa mitoko sijui nini hapana...

Yaani zile pigo za ku kucheal magetoni siku nzima kwangu ni kitu cha kawaida sana, shobo na watu nisiofahamiana nao kwangu ni big no... ila nimcheshi sana ninapopata fursa ya kuwa karibu na watu wachache niliowazoea...

Mambo ya kupigiana simu sijui na kuchatishasha kwangu haipo kabisa yaan sina mzuka nao kwa upande huo.

Kwa ufupi sana nipo hivyo.
 
Anhaa basi ndivyo upo zaidi upande wa introversion

Wewe ni mtu wa 14 kujibu na 12 kati ya 14 imeendana na prediction

12/14 * 100 = 85.7%

Bado najiuliza je hii ya watu kufavour upande fulani inaanzia umri gani, je inabadilika? mfano wanandoa walioishi miaka mingi je wanaambukizanaga? Maswali ni mengi nataka kujua yaani sema tu sina bado liresearch facility la mamilioni ya kuchezea kutafuta data kama hizo
 
Sipendi kukaa vijiweni kubishana napenda kuijua dunia zaidi hasa internet kuliko kitu chochote lkn nikinyimwa ndatu gubu lake litazuiwa na nato
 
Wahuni wote peponi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mi mtindo wangu ni huwa nawaangalia machoni nikiwa napita hivi..... akiniangalia namsalimia vizuri mnoo.

Asiponiangalia najisemeaga tu moyoni najiambia 'kuwa na heshima, heshimu maamuzi yake ya kutotaka kukuona wala kuinteract na wewe' basi na mi napita kimyakimya.

Nachukuliaga ndo heshima eti, ivi kwa mfano kung'ang'ania kumsalimia mtu anayeongea na simu ni heshima? au si-heshima? anayechati je??
Hiyo ya simu ni sawa inaeleweka hata usipomsalimia

Ila hii yangu niko kwenye personality conflict akili moja inaniambia niko sawa nyengine inaniambia siko sawa

Inshort I have no clue

I can't believe I'm saying this but I think I need therapist
 
Hiyo ya simu ni sawa inaeleweka hata usipomsalimia

Ila hii yangu niko kwenye personality conflict akili moja inaniambia niko sawa nyengine inaniambia siko sawa

Inshort I have no clue
Hapo ni changamoto

Lakini mda mwingine inasaidia kuamua kukubali kwamba mitazamo ya watu tunatofautiana. Unakuwa mkweli tu na nafsi yako.

Mfano mi ingenitokea hiyo ya wamama ningewaambia tu kwamba 'mi niliona mpo bize mnapiga stori na mnafua nikaona nisiwasumbue'

Au sababu yoyote tu. Ila kama ukikaa wewe ukaona sio sawa basi unawaomba msamaha. Eaasy tu.

Kuhusu wao kuielewa sababu yangu au kuikataa hiyo tena sio juu yangu maana binadamu tunatofautiana uelewa. Ndo maana hata wewe upande wako unaweza ukawaelewa ukawaomba msamaha au usiwaelewe ukawamaindi kufuatilia vitu visowahusu
 
But binadamu tunategemeana tusiwe selfish kuangalia upande wetu tu
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tafuta hela kijana,
Tafuteni heeeeeee....laaaaaa
Acheni ubabaifu,
Antisocial au umaskini huo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom