Ulikuwaje Ulivyokuwa Mtoto? Hivi ndivyo nilivyokuwa!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
ULIKUWAJE ULIVYOKUWA MTOTO? HIVI NDIVYO NILIVYOKUWA!

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi!

Moja ya sababu kuu zilizonifanya nikiwa mdogo nisipende kusafiri Kwenda kwa Ndugu Mjini, ni sababu ya Uvivu wangu.

Nilikuwa mtoto mvivu wa kazi hasa za Kuosha vyombo😊, sipendi kutumwa tumwa hasa nikiwa na michezo yangu au nasoma, nilikuwa napenda kusoma vitabu ningali mdogo kabisa na kupenda kucheza mwenyewe mara kadhaa na wadudu pamoja na Kobe na kuku niliyekuwa nawafuga hao ndio walikuwa rafiki zangu WA utotoni, sikuwa mtu wa marafiki sana.

Mpole nisiye na maneno mengi. Kwa kweli mtu akisema nilikuwa mtoto Mbaya hatakuwa amekosea. Jirani kunituma ilikuwa nadra Sana na ngumu mno.

Kwani sikuwa mtoto wa kuonekana wakutumwa tumwa. Na Kwa wale walioniona ninafaa kutumwa basi habari wanazo, sikupenda mazoea ya kijinga jinga, kiufupi sipendi ujamaa na mambo ya bure, yaani unitume Burebure labda siku hiyo niwe na roho wa Mungu.

Labda nilichokuwa nawafurahisha Walezi wangu ni uaminifu, upendo, ufaulu Darasani na kutokuchagua chakula na msimamo.

Walezi wangu wakiacha maagizo basi waliamini yatafanyika vilevile pasipo kupungua wala kuzidi hilo liliwafanya waniamini sana. Kwa kweli hayo tuu waliyafurahia. Lakini linapokuja suala la kazi, hapo ndipo kero yangu inapotokea.

Nilikuwa Kavivu alafu kenye makosa ya uharibifu wa vitu, utundu wa kijinga. Haikuwa rahisi siku ipite bila kuchapwa Bakora. Taikon anaamini katika Bakora tena Bakora Haswa😊😊.

Na ukinichapa nilikuwa napiga mayowe mpaka majirani wote waje hapo😊
Nilipenda kwenda Shambani lakini sikupenda Kulima, Kwa kweli nilikuwa mzigo Kwa walezi wangu. Mungu awazidishie Kwa kuvumilia wao.

sikupenda kuwa mzigo Kwa Watu ambao sio jukumu Lao kuwapa mzigo. Hilo lilinifanya nisisafiri Kwa Ndugu.

Mimi ni Wale watoto ambao tupo Real, yaani Kama kitu sitaki nitakuambia sitaki. Kama sijisikii kwenda nitakuambia siendi!
Utanichapa nitalia lakini sitaenda!

Na ukiona nimeenda Basi umenipiga Sana na nitakuambia nimeenda Kwa sababu Umenipiga Sana. Na sio Kwa sababu nimeheshimu.

Tabia zangu hizo zilizopewa jina la Ujeuri ndizo zilinifanya nisiende Kwa watu hata Kwa likizo ya mwezi tuu. Niliogopa unafiki. Kuishi Kwa unafiki sikuweza.
Unajua ugenini hauna Uhuru, na Mimi ni Bora ugali mlenda na nguo moja kila siku lakini niwe Huru.

Ni Bora niishi kijijini na mashambani kwenye uhuru Kuliko niishi maisha mazuri mjini, nguo unabadilisha kila siku, na chakula lakini sipo Huru.

Taikon nilikuwa ni mtoto nisiyependa kuzingatiwa, hata Leo nipo hivyo, mtu simple. Sipendi attention, nilikuwa navutiwa zaidi na watu waliokuwa wananichukulia simple, kiukweli ninakuwa comfortable nikiishi na watu wanaonidharau kuliko wanaoniheshimu😊😊.

Wanaonidharau ninakuwa huru kufanya lolote Liwe zuri au Baya lakini wanaoniheshimu basi sitakuwa huru kufanya lolote isipokuwa nitakuwa makini kufanya mambo mazuri tuu Kwa ufanisi na weledi.

Wanaonidharau ninapenda kuishi nao Kwa sababu nikifanya vizuri wanaumia😂😂 alafu wanakereka. Lakini wanaoniheshimu na kunipenda nikifanya vibaya wanaumia Jambo ambalo nami linaniumiza.

Sio mtu wa kujidanganya ati ili niwaridhishe watu kuwa waniheshimu😊 Yaani nijifanye Nina hela au nivae vizuri ili niheshimike😀 Never ever! Mimi vyovyote mtu akinichukulia Fresh! Ndio maana hata hivi Leo nipo Simple Sana.

Ukiona nimevaa Sana ujue Shemeji yenu ndio kanilazimisha ili akawaringishie Rafiki zake au ati nisimtie aibu😂😂. Siwezi jipa Wadhifa,
Ni rahisi kunikuta sijachana nywele na zipo Varuvaru na nikaingia ofisi kubwa tuu au kwenye sherehe 😊😊.

Ninapenda tabia hii Kwa sababu ninajua watu wengi ambao hawanijui hawatanijali na kunizingatia. Hii itanifanya nione uhalisia wao, wale watakao ni Jaji Kwa Dharau Fresh, watakaonijali licha ya kuwa katika mwonekano usiovutia ndio ninawapa kipaombele na tunakuwa Jamaa/washkaji.

Hata Shemeji yenu alinikuta katika Hali hiyo. Fresh tuu! Kama angekataa Fresh tuu! Najua wapo wanawake WA type yangu, wenye akili na mtazamo Kama wangu. Siwezi jigeuza mtumwa kisa mtu mwingine 😀😀. Nipo huru bhana! Maigizo labda kwenye mahaba Niue😊

Wageni wa maana wakija home kwetu ilikuwa nipo ndani huko nimejifungia naendelea na mambo yangu. Mpaka niitwe, kiukweli sikuwa napenda kujipendekeza hasa Kwa wageni waliokuwa wanaheshimiwa pale nyumbani. Napenda kuzingatia wasiozingatiwa.

Nilianza kuandika Stori za hapa na pale tangu nipo shule ya Msingi. Ingawaje sikuwahi kufikiri siku moja nitakuwa muandishi wa RIWAYA au Makala. Nilitamani niwe Daktari au Mwanasheria.

Labda niseme kuandika na kusoma ndio Hobby yangu tangu zamani. Nikiandika najisikia Raha ya ajabu😊 mpaka najikuta nimeandika Andiko refu😂😂 linalokera baadhi ya watu. Lakini Mimi sio mtu wa kuzingatia Sana maneno ya watu, hasa watu nisiowajua au wasionijua😀.

Nilikuwa mtoto niliyehitimu Mafunzo ya kudharau Ujinga na umasikini, na watu wanaoukumbatia. Vitu hivyo tangu nikiwa mdogo nilikuwa sivipendi.

Hata hivyo nilikuwa sipendi Watu wenye uwezo au waliojaliwa Jambo Fulani wakadharau wale wasiojaliwa au wasio na uwezo Fulani. Hata hivyo sikuonashida mtu ambaye Kwa makusudi hataki kuwa na uwezo au kujaliwa akidharauliwa na watu.

Nilikuwa mtoto niliyekuwa na ndoto ya kujitegemea. Sikuona ni fahari kujivunia Mali au wadhifa wa mtu mwingine. Ninunuliwe nguo nisinunuliwe Sawa.

Nilichokuwa nataka ni kusoma tuu. Nimalize niendelee na maisha mengine.

Kwa kweli nilitaka nikiwa mtu mzima ni Msomi. Ninaupenda Usomi, na naipenda Akili na Hekima kuliko kitu chochote kile.

Sipendi kumtegemea Mtu na huo ndio msimamo wangu mpaka sasa. Hata waliokaribu yangu huwaga kila siku nawausia wasinitegemee Bali wamtegemee Mungu na wao wenyewe.

Nilipokuwa mdogo nadra kuomba pesa, hata leo hii ni ngumu Sana kuomba pesa Kwa mtu. Tena burebure.
Kiufupi Taikon Hakuwa mtoto wa kudeka deka.

Mimi kila kitu Fresh tuu! Napenda kupambana mwenyewe, nikishinda nikishindwa Fresh. Na kamwe siwezi kumlaumu mtu.
Hata chakula kipikwe vibaya vipi huwezi msikia Taikon akilalamika au akitoa Shit.

Zaidi Sana nitampa pole mpishi kwani najua hakukusudia.

Taikon akiumwa tangu akiwa mtoto anajihangaikia pekeake. Kudekadeka Hakuna, nitajitahidi nisiwe mzigo Kwa wengine. Nitatengeza dawa zangu za Moto Shamba nitahangaika mpaka nitakapo Recovery, Kama nitakufa Fresh! Kifo ni rafiki wa kweli Kwa Taikon. Ingawaje wale wanaonipenda nazionaga jitihada zao, jinsi wanavyohangaika Kwa ajili yangu, na wakati mwingine wanaona ninawakera Kwa kujitesa ilhali wao wapo.

Taikon alianza kuvutiwa na Wanawake tangu akiwa shule ya Msingi, nilikuwa napenda Wadada ingawaje sikutaka mazoea nao. Si unajua nilikuwa Kuhani mtumishi wa Mungu.
Niliwapenda wanawake Kwa sababu walikuwa wazuri wa Sura, maumbile Yao teketeke, rangi za kushangaza, sauti zao za ajabu, Na vitabia vyao vya maringoringo, kujishaua, kisirani n.k.

Taikon hakuwahi kucheza Kibabababa na kimamamama, sikucheza michezo mingi ya kitoto Kwa sababu nilikuwa najiona Mkubwa 😀😀.
Moja ya madhaifu ya Taikon ni pamoja na kujiona Mkubwa kiumri hilo nitatizo linalonisumbua mpaka hivi leo. Hata sasa ni nadra Sana Taikon kuwa karibu na vijana wa umri wangu. Na Wale wenye umri wangu nao wanatabia hizohizo za kujiona Wakubwa. Yaani kijana wa miaka 28 anajiona Kama yupo miaka 40😀😀.
Hii faida yake ni kuwa unakuwa na utulivu na una-act as Mtu mzima.
Watu kadhaa waliowahi kukutana na Mimi walibaki midomo wazi wakishangaa walivyoniona😊.

Nilivyokuwa mdogo nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo ya Kidini, vitabu vingi vya Kidini nilishasomaga nikavimaliza, Biblia ndio Kabisa. Hivyo ninauelewa WA kutosha kuhusiana na Dini.
Nilianza kuona Dini ni Kama Club za mpira au Vyama vya Siasa nilipofikikisha miaka 13 tuu. Nikajua kuwa Dini ni taasisi za kibinadamu tuu ambazo hazina uwezo wa kumpeleka mtu Mbinguni.
Hivyo niliamua kuzichukulia Kama shabiki tuu WA mpira au jumuiya ambazo zinatukutanisha binadamu pamoja kufanya mijadala ya kiroho na sio zaidi ya hapo.
Hiyo ilinisaidia Kupenda watu wa dini zingine na kuwaona Kama Ndugu tuu. Kama vile mashabiki wa Mpira Kama Man United na Liverpool. Lengo ni kufurahia Burudani ya mpira. Na kwenye Dini lengo ni kujifunza mambo ya kiroho na kujifunza tabia njema.

Mambo niliyokuwa naogopa ni kujiona Mjinga na kutojikubali,
Unajua nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa naongea na Ulimi, yaani ulimi mzito Kama Nabii Musa. Hivyo nilivyokuwa naongea nikawa nashangaa watu wanacheka, nika-note, nikajikubali, kumbuka Mimi ni mtu wa kutozingatia maneno ya watu, nilipenda Sana kujifunza kwani niliogopa kujiona mjinga. Kumbuka ujinga siupendi na ninaudharau Sana.
Hasa kujua mambo madogo madogo.

Tuishie hapa! Hivyo ndivyo nilivyokuwa.
Je wewe ulikuwaje?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
yes kila mtu na tabia yake tangu anazaliwa
ila kwa tabia ulizoandika hapo inaonekana unachembechembe za uchoyo ila ni mtu usiyependa majivuno japokuwa kuingia kwenye ofisi za watu bila kuchana nywele huo ni uchafu tu hakunaga mwanaume anasifiwa kwa kuwa hovyohovyo
 
yes kila mtu na tabia yake tangu anazaliwa
ila kwa tabia ulizoandika hapo inaonekana unachembechembe za uchoyo ila ni mtu usiyependa majivuno japokuwa kuingia kwenye ofisi za watu bila kuchana nywele huo ni uchafu tu hakunaga mwanaume anasifiwa kwa kuwa hovyohovyo

Mimi ni Bepari. Kama huo ndio uchoyo ni Sawa. Mambo ya bure sinaga na wala sipendagi vya Bure.

Kuhusu uchafu no comments
 
Basi mie nilizidi kuwaza mnoo! nilipokuwa ntoto! nilikuwa nawaza mambo makubwa tuuuuu!! hii ilinifanya kuwa mkimya sanaaa miongoni mwa watu wengi!!

Ajabu nilikuwa nawaza kuwa Rais wa nchi hii! na kweli imekuwa km nilivo wazaga! hali hii ilianza kuanzia miaka 10 mpaka leo niko hivo!....kipindi cha miaka ya kati nilianza kudhania huenda mie ni namana ya kichaa!

kwa nini nawaza hivooo tuuuu hakuna kupumzika?...hata nikiwa chooni ivovivo tu!...mkimyaaa ajabu! kumbe ni kawaida ya Binadamu mwenye kismarti kuwaza sana!
 
Back
Top Bottom