mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 919
- 2,007
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.
(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]
(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.
(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.
Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.
NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]