OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,244
- 103,932
Kwa maoni yangu na namna ninavyomtathmini Rais Magufuli ni wazi upepo wa URAIS umemkataa kabisa.
Tathimini hii nimeifanya kwa kujaribu kulinganisha mwenendo wake kama Rais kwa miaka miwili na nusu na mienendo anayotakiwa kuwa nayo kiongozi ngazi ya Rais.
Ni wazi kwamba kiongozi huwezi kuwa kamili na kuwezi kuridhisha kila mtu lakini Magufuli kazidi. Yapo mambo kadhaa anayafanya ya kawaida sana japo yeye anayachukuliwa kama mambo yasiyo ya kawaida na kutaka kulazimisha apongezwe. Mbaya zaidi Rais Magufuli yeye binafsi anajiona ni rais bora na wa kipekee na anataka watu wamchukulie hivyo japo kiukweli anajidanganya.
Ukiweka vigezo vya Rais bora kulinganisha na mwenendo wa Rais wetu ni wazi hawezi fika hata asilimia 10 ya vigezo hivyo. Rais Magufuli ameshindwa kuifanya nchi itulie angalau iwe na uelekeo fulani,kila kukicha ni vurugu na matukio ambayo yanafanya nchi kukosa mwelekeo.
Kibaya kingine ni yeye kuvuruga mfumo badala ya kuipeleka nchi kwenye taasisi imara zenye uwezo wa kujisimamia yeye amejilimbikizia kila kitu. Matokeo yake mambo hayaendi au yanaenda kusiko uelekeo sahihi. Jambo hatari ambalo amekuwa nalo Rais ni ubabe wa kujigeuza mmiliki wa nchi badala ya kiongozi. Amekuwa sio mtu wa kutafuta muafaka,mfano mdogo ni ugomvi wake na vyama vya upinzani na maaskofu. Ugomvi huu kila mtu anajua hauna afya kwa nchi.
Rais anaona kukaa meza moja na wapinzani ni aibu kwake kwamba ataonekana dhaifu. Hii ni kama sawa na mtu anayenuka majasho badala ya kuoga anahipaka marashi kutoa harufu,huwezi kutoboa.
Mambo kama haya ndio huzaa madikteta wa kung'ang'ania madaraka. Ni dhahiri rais inakuwa ngumu kutoka madarakani kwa sababu ya uadui aliojitengenezea kwa wananchi. Anajishtukia kuwa anaweza kufanyiwa kitu mbaya akiwa sio Rais.
Sina mengi namtakia busara sana Rais wetu Mungu ampe hekima