Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwa matukio haya

Kupotea kwa
1.ben saanane
2.Azory Gwanda
3.Lisu kupigwa risasi
4.Nape kutishiwa bastola
5.miili ya watu kuokotwa ufukweni mwa bahari
6.Ansbert Ngurumo kuomba hifadhi nje
7.viongozi wa upinzani kuwekwa ndani
8.Abdul nondo kutekwa
9.Akwilina kupigwa risasi
10.watu kufunguliwa kesi za uchochzi
11.biashara nyingi kufungwa
12.kuminywa kwa democracy na uhuru wa kujieleza
13.utitiri wa kodi usiondana na hali halisi ya biashara
14.Watu kufukuzwa kazi kiholela
15.Manunuzi yasiyofuata utaratibu za manunuzi
16.Kuzorota kwa hali ya elimu nchini
17.Watanzania kuishi kwa vitisho
18.Kukosekana kwa ajira kwa wanafunzi wengi wanaohitimu vyuo
19.Polis kubambikizia raia kesi
20.Kejeli dhidi ya viongozi wa dini
21.kuvunjwa kwa katiba na kukosekana kwa utawala wa sheria na mengine mengi
JE NI NANI ALIYE SALAMA?
Haya alipaswa kujibu dereva la lorry
 
Kwanini wewe mwenye kichefu chefu usitapike mambo mengine masafi unayohisi kwa uelewa wako ili watu wajadili?
watu wenye kitambi kama hicho chako si wazuri kwa majadiliano wataishia kunilisha matango pori tu.
 
tangu rais John Pombe Magufuli aingie madarakani taifa la tanzania halijapata utulivu katika sekta zote! naam wote tunaimba wimbo mmoja hatujatulia. inakua kana kwamba tuko kipindi cha mpito tunataraji mwaka fulani tutapata utulivu kamili baada ya kupata utawala kamili. hii sintofaham itaondoka lini??

kuna watu wanakua kama hawaoni lakn huku wanaona hali tulionayo. yaan wanaziba masikio na kujifanya mambo ni shwali. hivi ni katika utawala gani tulipitia kama katika utawala huu??

kisiasa kila pande ni kelele kana kwamba tuko kipindi cha kampeni na uchaguni ni siku mbili zijazo . yaan kila upande unaponda upande wa mwingine.
rais wetu hajapata kutulia yaan ni kiguu na njia huku na kule kuonyesha kwamba yeye anafaa na kuonyesha kwamba anafanya kazi. yaan muda wote ni kuwaambia watu yeye ni rais tena anaongezea kwa kusema anajiamini. unajiuliza nani kasema wewe sio raisi!??


viongozi wa dini wamelisemea hili .

asasi mbali mbali mbali zimelisema hili.

mashirika ya kimataifa wamelisema hili.

ni kweli hatupigani vita sisi kwa sisi ila ni kama kuna maandalizi ya kupigana maana ni kama tunatunishiana vifua sisi kwa sisi na muda wowote tunaingia ulingoni.

kwa hali hii tutalijenga taifa letu??
hatujatulia tangu tufanye uchaguz 2015.
mwakani uchaguz wa serikali za mitaa.
na uchaguz wenyewe siku hizi ni vita tupu. mwaka unaofata uchaguz mkuu !!!
lini tutakaa na kusema tumepata uongoz na tutatulia na kujenga nchi?? na ni nani wa kututuliza

wenye dola ni mwendo wa kamati yule , hoji yule funga huyu, kemea yule yaan ni mwaka wa tatu toka tufanye uchaguz lakn ni kama tuko kwenye kampeni.huku mtaani ni mwendo wa kujadili mambo ya kusiasa na maisha kwa ujumla tena maisha yenye hali ngumu. lini tutatulia??
 
mzee anahubiri kuhusu nchi ya viwanda, na hata sasa viongozi wadini wameambiwa waombee kuhusu viwanda, bado unauliza tunakwenda wapi kama nchi....? kweli....!??
 
Kuna jarida nimesoma limeandika Tanzania haina rais tangu Oktoba 2015. Bado natafakari ili kujua mwandishi alimaanisha nn.
 
Kwa matukio haya

Kupotea kwa
1.ben saanane
2.Azory Gwanda
3.Lisu kupigwa risasi
4.Nape kutishiwa bastola
5.miili ya watu kuokotwa ufukweni mwa bahari
6.Ansbert Ngurumo kuomba hifadhi nje
7.viongozi wa upinzani kuwekwa ndani
8.Abdul nondo kutekwa
9.Akwilina kupigwa risasi
10.watu kufunguliwa kesi za uchochzi
11.biashara nyingi kufungwa
12.kuminywa kwa democracy na uhuru wa kujieleza
13.utitiri wa kodi usiondana na hali halisi ya biashara
14.Watu kufukuzwa kazi kiholela
15.Manunuzi yasiyofuata utaratibu za manunuzi
16.Kuzorota kwa hali ya elimu nchini
17.Watanzania kuishi kwa vitisho
18.Kukosekana kwa ajira kwa wanafunzi wengi wanaohitimu vyuo
19.Polis kubambikizia raia kesi
20.Kejeli dhidi ya viongozi wa dini
21.kuvunjwa kwa katiba na kukosekana kwa utawala wa sheria na mengine mengi
JE NI NANI ALIYE SALAMA?
22.Wakulima.kukosa pembejeo za kilimo
23. Hospitalini hali tete kwa kukosa madawa na vitendea tiba.
24. Kuundwa kwa kikosi maalu.cha wasiojulikana.
25. Ndugai kugoma kusaini pesa za Lisu za matibabu na badae nae kuumwa karibu kufa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom