mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,843
- 3,128
Pointlesskwamba uongozi wa nchi umekushinda? Kwanini kupambana na ufisadi kuwaathiri Watanzania walio wengi ambao si mafisadi?
Kama ufisadi mbona nawe unaufanya!? Hujasema lolote kuhusu rushwa ya milioni 10 kwa kila mbunge wa MACCM iliyotolewa October 25, 2016 pale lumumba?
Mbona unaendeleza ubadhirifu kwa kuchota trillions kutoka hazina bila idhini ya Bunge?
Kujenga chato Airport ni ubadhirifu mwingine unaofanya. Hivyo achana na uongo wako sema kweli tu uongozi wako wa nchi umeshindwa na utaendelea kushindwa kutokana na sera MUFILISI, kukurupuka na kuendesha nchi kama vile una hati miliki.
"Licha ya ukweli kutokana na hatua tunazozichukua za kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma, wapo wananchi wa kawaida ambao si wezi wala mafisadi wanaoathirika, hili ninalifahamu, lakini kama kweli tunataka kupambana na wizi na ubadhirifu pamoja na kuleta maendeleo kwa nchi yetu, athari hizi hatuwezi kuzikwepa, mabadiliko ya aina yoyote ile lazima yana athari kama hizi, lakini jambo la kututia moyo ni kwamba athari hizi mara nyingi ni za kipinzdi kifupi", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba..."Mabadiliko ni magumu mwanzoni, yatakuwa machungu yanapofikia katikati, lakini mwishoni matokeo yake ni mazuri au ni matamu, hivyo nawaomba wananchi na watanzania tuvumile katika kipindi hichi cha mpito, baada ya muda mfupi mambo yatakuwa mazuri, lakini hata kama hayatakuwa mazuri hivi karibuni, watoto na wajukuu zetu watanufaika, na huo ndio uzalendo".