Jamani mi niko serious, ninyi mnaleta siasa. Hii ni mada inayoweza kutusaidia na kumsaidia rais tukiondoa ushabikiKuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....
Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.
Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....
HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!
Angalau wewe umejaribu kujibu, mkishakusanya fedha hizo zinaenda wapi? Halimashauri zinalia na mitaani ndo usisemeTunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu. Elimu bora no.
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .
Hivi mkuu makusanyo ya mwezi April yalikuwa trilioni ngapi? Na za mwezi May je?Tunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu na Elimu bora .
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .
Nashauri moderators kama wapo na wanahitaji mijadala makini kwa maendeleo ya jukwaa wafanye kazi yao kwa kuondoa hizo hoja za nje ya mada na kebehi ili watu makini tujadiliane uelekeo wa nchi yetu.Watanzania tuna akili fupi sana ndo maana hatusonge mbele kama taifa na mtu mmoja mmoja, maada ni nzuri inawweza kutusaidia kuibua njia mpya za kumsaidia rais kama ushauri, mtoa mada hana nia mbaya na rais bali anajaribu kutushirikisha tuangalie mwelekeo wa sisi kama taifa, kwa hiyo tuache kumkebehi tuchangie mada kwa mtazamo chanya kwa kutoa michango na ushauri wa kujenga taifa.
Haya wanayajua haya unayosema?Hivi mkuu makusanyo ya mwezi April yalikuwa trilioni ngapi? Na za mwezi May je?
Zamani tulikuwa tunatangaziwa mapato na matumizi ya serikali lakini kwa sasa ni kimya kabisa. Pia ukiongea na watumishi serikalini watakwambia hakuna hela ya DEVELOPMENT imetumwa mwezi wa nne na wa tano, pia hata hela ya kuendesha ofisi maarufu kama OC haijatumwa kwa miezi miwili. Hii ni dalili kuwa nchi haina muelekeo mzuri kiuchumi ingawa sisi wengine tunampa muda huyu nahodha wetu hadi atakapoanza kutekeleza bajeti yake mwezi July
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifaMuda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
Good point umeelezea vizuri.Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike