Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

niliweka thread wazi kama wazanzibar mtapokea mtakuwa mmejizaalilisha sana awakutahamini watu wakiwa aherawaje kuthamini kutoa michango kisa rais kaelekea huko shame on them

nakubaliana na wewe lakini pia una taarifa kuwa CCM nao walizindua kampeni wakati janga hili limetokea? je mchango wao ukataliwe, au kuna suala la kafanya fulani huyo awajibishwe, huyu mwingine aachwe

Kama mfanya biashara makini lazima ufikirie na utenge dharula. Je kama ingetokea Rais au waziri mkuu kafariki na nchi ikatangaza maombolezo na kusimamisha shughuli zote za michezo na burdani . Ungefanya nini?

Nafikiri hiyo ni dharau dhidi ya Mamlaka ya nchi na kejeli kwa Taifa.

Pesa ni mali kuliko uhai.
mimi naona propaganda tu hapa, mjadala umehamia VTL kama vile wao ndo wanahusika na uzembe uliopelekea ajali. Wao wanahusika katika kuomboleza tu, wamekiuka taratibu za kiutamaduni na kiungwana katika msiba.

ni kwa nini hakuna mjadala wa kitaifa ndani ya jf na nje ya jf kuhusu zababu za msingi za ajali?
Hli sio taifa la kuomboleza, ni taifa linalohitaji ustawi wa watu wake na ulinzi.

nakubaliana na wewe lakini pia una taarifa kuwa CCM nao walizindua kampeni wakati janga hili limetokea? je mchango wao ukataliwe, au kuna suala la kafanya fulani huyo awajibishwe, huyu mwingine aachwe

hili hawaliangalii ila wanaangalia miss vodacom .. mbona TFF na Mkap hawazungumziwi ... mbay zaidi televisheni ya taifa haikutoa taarifa yoyote mbona hawalaumiwi

Kuilaumu VODAOM ni makakati mahasusi wa idara ya usalama wa taifa kuwapumbaza watanzania wasiweze kujadili chanzo halisi cha ajali ya mei yaani uzembe wa mamlaka na Serikali kushindwa kuchukua hatua za dharura kuwaokoa maisha ya abiria hao tokea saa saba usiku ilipopigwa SOS hadi asubuhi.

TISS walimtumia Zitto kuanzisha mjadala huu dhidi ya Vodacom kwa kutegemea kuwa watu wengi watashabikia. Hata ukisoma msg ya Zitto utagundua iliandaliwa maalum k.m kuisifia Serikali ya Mapindizu ya Zanzibar kwa jinsi ilivyoshughulikai tatizo hilo. Zitto na ninyi vibaraka wa TISS mnaweza kutuambia SMZ ipongezwe kwa kitu gani kuanza shughuli za uokoaji Saa mbili asubuhi badala ya Saa usiku mara tu ajali ilipotokea.

Zipo taarifa zinzoonyesha kuwa ilikuwepo news black off kuhus ajili hiyo iliyoratibiwa na TISS kwa lengo la kuepusha aibu kubwa kwa Serikali zote mbili endapo vyombo vya habari vingewafikia walionusurika mapema na wakaeleza hali halsi ilivyokuwa kabla na baada ya ajali hiyo. Ndio vyombo vyetu vya habari viliendelea na shughuli kama kawaida.

Hata wavuvi wa eneo la Nungwi waliohijiwa na vyombo vya habari jana wamethibitisha ya kuwa zilikuwepo hatu za makusudi za kuficha idadi ya watu waliokufa katika jali hiyo kwa Serikali kuelekeza utafutaji maiti jua linapochomoza au kutua badala ya upande uliostahili kwa mujibu wa uzoefu wao. Pia wamelaumu kitendo cha watu kuzuiwa kuendelea kutafuata maiti upande sahihi.

Zoet hizi ni njama za kuficha ukweli wa idadi kamili ya watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hii ya kizembe. Hivyo kuitupia lawama Vodacom ni muendelezo wa njama hizo. Wanaostahili kulaumiwa ni Viongozi wetu wa kitaifa ambao wameugeuz msiba huu kama sehemu ya kutafuta umaarufu kupitia vyombo vya habari kwa kusifia vitu vya hovyo kabisa kama muungano wetu, badala ya vyombo hivyo kutuhabarisha habari muhimu kuhusu walionusurika, majeruhi na kupoteza maisha. Wengine wanaopaswa kubeba lawama kubwa ni CUF hususan Maalim Seif kwa kukubali kushiriki mchezo huu wa kuigiza wa kuficha uzembe wa Serikali.

Hii inathibitishwa na kauli ya mbunge wa CUF mmoja kuonekana kwenye runinga jana akilalamikia kitendo cha wahanga wa Pembe kutopatiwa kipaumbele kabisa katika shughuli zote zinazohusu ajali hii licha ya ukweli kwamba wao ndio wahanga wakubwa na ndio waliopoteza maisha na ndugu zao kwa kiwango kikubwa. Viongozi wa CUF walithamini sana ndoa ya CCM/CUF badala ya maisha ya wananchi. Ni lazima Waziri wa Miundo mbinu wa SMZ kutoka CUF ajihudhuru ili kuonyesha ya kuwa yale wapinzani waliokuwa wakiyadai miaka yote ya watu kujiuzulu yanapotokea majanga kama haya. Ikiwa Waziri huyu atashindwa kujiuzulu na kisha CUF kunyamaza basi tutambua kuwa madai hayo ya CUF yalikuwa ni unafiki mtupu.

Naam, wewe ndiye umeleta hoja ya msingi. Kwa hakika pamoja na blah blah nyingi zilijaa humu JF kuhusu hili suala, ukweli unabaki palepale kwamba hii ngoma ni ya SMZ. Watu kwa kutotumia logic wanarusha lawama Vodacom. Nimeuliza awali kwamba mbona Vodacom haijalaumiwa kwa kufanyika kwa mechi ya ligi kuu siku hiyohiyo? Au mbona hakuna anayezungumzia kumsusia Bakhressa kutokana na timu yake kushiriki kwenye hiyo mechi? Wengine wamehoji kuhusu CCM na Orijino Komedi Igunga lakini hakuna anayejibu.
Inaweza pia ikawa hizi lawama kwa Vodacom pia ni vita inayoratibiwa dhidi ya gamba la kwanza kujivua Bw. Rostam Aziz!

We uko wapi? tangu jana watu wanailaumu TBC1, kwa sababu ni chombo cha taifa na Vodacom kwa kuwa ndio imebeba jukumu la taifa, VODACOM MISS TANZANIA na sio CLOUDS MISS TANZANIA.

Auwezi kuilaumu star tv, hivyo ni vyombo binafsi vya habari, tunalaumu vyombo vya umma.

KUWA MUELEWA.

Mkuu umenisaidia na mimi kuwa muelewa!! KUMBE VODACOM NI CHOMBO CHA UMMA!!! Sasa nimekuwa muelewa kama wewe...

Hivi leo serikali ndio inauwezo wa kukataa msaada kwa kigezo hicho?
Upuuzi wangekuwa makini kwanza wao kwa kuhakikisha meli ile inasafiri kwa masharti husika yaliopelekea ajali lakini watu wasamehe hawakuisusia serikali kwa uzembe wao, leo wanafanya hivyo kuwahamisha watu kutoka katika uzembe wao na uonekana ubaya wa Vodacom.
Vodacom ni wadhamini tu wa shindano lile ingawa nao wanakasehemu kao lakini waliopanga kama wameamua au wameona kuhairisha ni kusababisha hasara unategemea Vodacom wangefanya nini?.
Nchi hii bana kila kitu siasa
ZIlikuwa ndogo,trust me kama wangetoa msahada wa lets say billion 5 jamaa wangezichangamkia fasta kwani kwa watendaji wengine wasio muogopa Mwenyezi Mungu huu ni msimu wa kuneemeka,

Hatimae kilio cha wengi kimesikika kwani ule msaada uliotolewa na Vodacom kwa wale wahanga wa kuzama kwa meli Zanzibar umekataliwa

kwani pale watu wa Jamhuri ya muungano wakilia na maafa yaliyo wakuta hawa wenzetu kutoka SA Walikuwa wakisheherekea miss Tanzania

hongera serikali ya zanzibar

habari hii ni kutoka redio ujerumani kiswahili

Wameona msaada hautoshi ndo wanjifanya kuukataa, ingekuwa ni cash kama 200billion ungewasikia wakiisifia Vodacom. Nani kakwambia wabongo hukataa misaada????????.

"@JMakamba: Siku ya msiba, CCM ilizindua kampeni kwa shamra Igunga, Ligi Kuu iliendelea, mabaa yalijaa, but kuna watu wamekomalia shughuli ya vichupi!"

January,

Kama kweli umeandika labda ufafanue wenye baa yepi waliendelea kufanya biashara? Maana navyojua baa za kilimani, ngome kongwe na bwawani zote zilifungwa na maduka ya biashara darajani yalifungwa. Pia tufafanulie hao wenye baa uliowanukuu wanamiliki baa au wana wateja zanzibar? Pia je Vodacom wana wateja zanzibar au hawana? Nafikiri ungeliendelea kumpa pole dada yetu Mwami kwani amechemka vibaya sana na pengine ungelimkaribisha katika siasa kwani katika makampuni inaelekea hana ethics wala kuwa na sense of responsibility to know the right decision at the righ time.

Hivi jamani mbona Voda tu bado kuna Redds na wale media moguls like TBC, ITV. Voda wanayo makosa ila sio wao pekee na hawa pia wanabeba msalaba wa makosa yao. Bila ya kusahau serikali ya SMZ pia.

Jaman vodacom walikuwa kazin nan kasema walikuwa wanasherehekea..watu walikuwa kazin eti kwa sababu kuna msiba watu wasiende kazin miss tanzania ni kaz halal kama kaz nyingine emu achen kudharau kaz za watu.SMZ waache unafki wakat bar na makanisa yanachomwa walikuwa kmya
kWELI BWANA HAKA KATABIA SIO KAZURI

ni wataalamu wa kutoa rambirambi kama ilivyokuwa

mbagala,gongo la mboto,happy nations...................................!
matatizo ya kutokuwa serious na jambo lolote isipokuwa uchaguzi.

Wale wapumbavu kina Lundenga eti wameomba radhi

Hapa vodacom wamekosea jamani. Hata hao LINO pia wamekosea kabisa. Unaju hata kama vodacom walitishia kutowapa udhamini basi LINO wao wangeonyesha msimamo wao. Hapa inabidi tuchukue hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kutomtambua mshindi wa hilo shindano.

Mimi nitashangaa kabisa eti huyo mlimbwende anajihusisha katika shughuli za kusaidia jamii. Ni jamii ipi hasa anilenga wakati tangu mwanzo hakuwa na huruma kama hiyo? Huyu pia yapaswa tumkatae kwa sauti kuu, tumwambie hatukutambui na pia hatutaki misaada yako. Iweje utukumbuke leo wakati ulitudharau siku tulipopatwa na majonzi makuu ya taifa letu?

Hapa ili vodacom wajisafishe kwa jamii ni lazima wafanye haya mambo yafuatayo
1.Kwanza inatakiwa kuwafukuza kazi wale wahusika wa moja kwa moja na jamii(Mkurugenzi wa mahusiano ya jamii, hapa ni Mwamvita Makamba), pia meneja mahusiano bwana Salumu mwalimu.

2.Wasitishe huduma kwa huyu mshindi wa miss Tanzania kwa kipindi chake choote atakachokuwepo katika taji lake.
3.Wafute udhamini kwa mashindano ya miss Tanzania kuanzia mwakani.
4.Waombe radhi hadharani kwa kitendo chao cha kukosa utu.
5.Wajitathimini upya mahusiano yao na jamiii kwa sasa na penye tatizo walishughulikie mara moja. Hapa waje na sura mpya kabisa kwenye safu ya uongozi na si kuwaona tena Mwamvita Makamba na Salum Mwalimu.

Vodacom chukueni hatua vinginevyo mtaangamia kibiashara. Ninyi ni kampuni achaneni na mambo ya kuwabeba watu waliosababisha muwe katika hili zogo.

Kama sherehe ya harusi inaombewa kibali cha serikali,vyp miss Tanzania? Mashindano yalikuwa na kibari cha serikali na hayakufanyika uchochoroni,polisi walilinda mashindano' kama ndivyo serikali ilishindwa nin kuyazuia?! Kama mnailaumu Voda kwa kosa gani? Vyp wenye ukumbi mnawachukuliaje? Vyp kuhusu watazamaji?...

ADHABU KWA VODACOM IPO PALE PALE!JF walishatahadharisha mapema kuwa kama mashindano ya u miss yatafanyika siku ile vodacom watakua punguani!mkakaidi sasa radhi mnaomba ya nini kama sii unafiki

Vodacom wana makosa gani hapo? Wao ni wadhamini tu lakini mashindano yanaandaliwa na Lino Agency.

Hii iwe fundisho kwa kejeli waliyoionyesha Vodacom
Mkuu waliokosea ndio walioomba msamaha na sio Vodacom

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba . Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo. Kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .

• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.

• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.

• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo.

• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo. Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza "TUNAOMBA RADHI"

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,

Hashim Lundenga

Mkurugenzi

Hii iwe fundisho kwa kejeli waliyoionyesha Vodacom
Mkuu waliokosea ndio walioomba msamaha na sio Vodacom

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba . Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo. Kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .

• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.

• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.

• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo.

• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo. Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,

Hashim Lundenga

Mkurugenzi

VTL Kama wadhamini wakuu wa hili shindano walitakiwa kufanya tafakuri makini katika hili. Mapicha ya Vituko vya mwanamasoko mkuu wao na mdada wa blogu ya katakona kwenye safari ya limo mlimani site ni msumari mwingine katika taswira ya VTL

Wasalaamu,

Shadow

VodaCom yakataliwa "ubani" wao Zanzibar
13/09/2011
0 Comments

Serikali ya Napinduzi ya Zanzibar imeukataa msaada wa maafa uliokuwa utolewe na kampuni ya simu za mikononi ya VODACOM kufuatia wananchi kuilalamikia kampuni hiyo kuendesha mashindano ya miss Tanzania wakati Wazanzibari wapo katika msiba wa kitaifa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, ndg. Mohamed Aboud alithibtisha kuwepo kwa taarifa hizo za SMZ kukataa msaada wa maafa uliokuwa utolewe na kampuni ya simu ya mikononi ya VODACOM.

'Ni kweli tumekataa kupokea msaada huo ingawa hatujuwi ni kiasi gani cha fedha... unajuwa wananchi wengi wametoa malalamiko yao na kukerwa kwa wafadhili hao wa mashindano ya urembo kuendelea na unesho lao wakati huku taifa limepatwa na msiba mkubwa,' alisema Aboud.

Alisema wadhamini hao walikuwa wanatakkiwa kufahamu wajibu wao kwa jamii zaidi wakati inapokutwa na maafa kama hayo ya kuzama kwa meli na wananchi zaidi 197 kupoteza maisha yao.

Aboud alisema haielekei hata kidogo kwa kampuni hiyo iliyodhamini mashindano hayo kuendelea wakati huku Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete pamoja na rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein wametangaza msiba wa Kitaifa

Wananchi wengi wa Zanzibar walikerwa na kitendo cha kuendelea kufanyika kwa maonesho ya urembo ya kumtafuta Miss wa Tanzania katika kipindi ambapo taifa lipo katika msiba mkubwa.

[habari via Beda Msimbe/Lukwangule blog]

source: VodaCom yakataliwa "ubani" wao Zanzibar - Wavuti

Saafi saana hii inaitwa Keep hammering, Never over until it’s over. Thread kama hii hii imeshatiwa kwenye furushi huko habari mchanganyiko kusikosomwa sana kama hapa siasa forum.

INVISSIBLE Mkuu wangu sikuelewi unavyoonyesha kuguswa na hizi thread za VODACOM kwa mtazamo hasi, na umeamua kwenda kuzisokomeza huko Habari mchanganyiko kama takataka kwenye thread ya Bingmen mpaka imevunja Rekodi ya Post hapa JF haijawahi kutokea kwa namba ya michango na Views.

Unatutia shaka Mkuu, Unatushawishi kujiuliza VODACOM wamekupa nini? Maana unachokifanya ni kuuwa passé ya move wakati hoja imefika kwenye kina, mbona unaminya Uhuru wa Mawazo? Wacha watu waseme kupitia mijadala hii kwa kukubaliana kutokubaliana nidhamu itapatikana kwa watendaji wetu na somo kwa wazembe wengine.

Sifurahishwi na haka katabia kako Mkuu katika thread hizi kuhusu Mkasa wa VODACOM na Ajali ya Spice Islander huko Nungwi Pemba, au kama policy za forum zimebadilika tupe taarifa tutazingatia tu kuliko mchezo huu ambao kwa hakika unatia maudhi sana na kukatisha tamaa, tutasemea wapi sasa Tanzania hii kama na hapa napo tetenasi imeingia? Najua baada ya Muda itakuwa Kapuni na hii thread wala sitashangaa.

Mie binafsi sipost tena juu ya jambo hili maana Starter Pack yangu ilikuwa the right shot na imejibu na kitaeleweka tu, si wanasiasa kwa viongozi wa Dini wote wameamka na wanapaza sauti zao kila kona kuhusu kadhia hii… ntakuwa nadandia treni kama hivi kufikisha ujumbe wangu.

Wakatabahu

Mwanafamilia

GR

Back
Top Bottom